greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 783
- 1,213
MAKALA YA 5
Karibuni katika Makala yetu ya kila wiki, leo tunaangazia kwenye kukabiliana na Baridi kwenye jengo.Kwa wale wa Njombe, Ruvuma, Mbeya, Kagera, Arusha, Iringa, Singida, Kilimanjaro, Lushoto, Dodoma na Tabora sogeeni karibu.
1. Hali joto stahiki kwenye jengo lenye kuupa mwili starehe ni 20⁰C hadi 25⁰C.
-Kuna njia kuu 2 za kushusha Baridi kwenye jengo.
-Njia za za Kimakanika na Njia za Umeme.
2. Njia za KIMAKANIKA
(A)Muundo wa Jengo: hapa muundo mzima wa jengo husika.
-Umbo la jengo/Vyumba,umbo la mraba ni bora zaidi kuliko mstatili
-mpangilio wa vyumba, mf.chumba cha kutumika usiku tu ,kikae upande wa magharibi,cha kutumika na wengi kikae kaskazini au kusini.
-floor plan iliyofungwa(closed floor plan);usiige ramani za Dar, ambapo sebure kwenda dinning hadi jikoni hamna kuta.
3. (B)Kuta
-Kuta Nene: Ukuta unatakiwa uwe na unene kuanzia MM 230.
Ukuta mnene hutunza joto.
-Matilio ya Kuta ,kuta za tofali za udongo ni bora katika kutunza joto kuliko kuta za mchanga
-Kuta mbili ,badala ya kuwa na ukuta mmoja ,ziwe zinajengwa mbili ambapo kutakuwa na nafasi kati.
4. (C)Madirisha-Matilio;madirisha ya frem za mbao na Panel za vioo ni bora kuliko ya Aluminium.
-Panel nyingi za vioo:vioo huzuia joto,panel zikiwa mbili au tatu husaidia zaidi.
-ukubwa wa Dirisha,lisizidi upana wa 1.5.
-uelekeo wa madirisha,mengi yawe upande wa kusini na kaskazini.
-Madirisha,vioo vishikwe kwa gasket kuzia baridi kupenya.
5. (D) Milango,kwenye milango hakikisha.-Milango owe ya mbao.
-Milango iwe na Jamb: hapa ni Milango ya kuingilia kwenye nyumba, chini kuwe na kimbao ambapo ukifunga mlango, iwe ina zina uwazi wa chini.
-Mlango ukiwa na panel ya kioo,basi kiwe kinene
6.(E) Sakafu-matilio ya mbao na Kapeti ni bora zaidi.
-Tabaka la matilio ;baada ya kujaza kifusi na kuweka mawe,ni vyema kumwaga zege nayo itasaidia baridi la ardhini kuchelewa kupanda juu.
(F) Finishing- -Vyema kuta zikapigwa plasta na Skimming
- -Rangi za joto: husaidia kumfanya mtu haisi kuna joto ndani ya chumba husika
- Mf.Rangi ya Orange,Njano au Nyekundu.
- -Rangi za mafuta ni bora kuliko za maji.