PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Aug 17, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Kila nipatapo fursa, sipendi kabisa kukosa kipindi cha Maswali na Majibu ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni, ambapo Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza, Peter Pinda, hujibu maswali ya papo kwa papo, ile leo nilikikosa kipindi hiki.

  Lakini kupitia taarifa za habari, nimemsikia Mhe. Pinda, akisema kuwa ni jukumu la wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote ili CCM iendelee kutawala milele!.

  Naombeni wajuzi wa masuala ya utawala, mnirekebishe if I'm wrong!, kuanzia kwa rais JK na wanasiasa wengine wote ambao japo wamechaguliwa kwa tiketi tuu za vyama vaya siasa, lakini walio wachagua sio wanachama wa vyama vyao, bali wamechaguliwa na umma wa Watanzania, rais, mbunge, diwani au wenyeviti wa mitaa, ukiishaguliwa, japo unabaki kuwa mwanachama wa chama chako lakini unageuka ni mtumishi wa umma, paid by taxpayers money, jukumu lako kuu sasa ni kuutumikia umma na sio kukitumikia chama chako!.

  Hii inamaanisha rais JK, japo ameshinda kwa tiketi ya CCM, kuongoza serikali ya JMT, kwa kutumia ilani ya CCM, ambapo kwa wakati huo huo yeye ndiye Mwenyekiti wa CCM, hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na Watanzania wote kuiongoza Tanzania na Watanzania na sio amechaguliwa na wana CCM, kuongoza serikali ya CCM kwa ajili ya wana CCM!, hapana!, JK na serikali yake, japo ni CCM, lakini amechaguliwa kuongoza serikali ya Tanzania kwa niaba ya Watanzania wote na kwa manufaa ya Watanzania wote, na sio kwa manufaa ya wana CCM!. (Of the people, by the people and for the people).

  JK ndiye rais wa Chadema, ndiye rais wa CUF na ndiye rais wa wasio na vyama kama sisi!. Yeye ndiye rais wa Dr. Slaa, yeye ndiye rais wa Prof. Lipumba, yeye ndiye rais wetu sisi wote kama Watanzania, ni rais wa waliomchagua na pia rais wa wasiomchagua, anatakiwa kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya chama chake cha CCM!.


  Kauli ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda bungeni leo kuwa Wakuu wa wilaya na mikoa, wako pale kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote ili itawale milele, haiwezi kupita bila kupingwa!. Hi inamaanisha kuwa viongozi hawa, wako kwa ajili ya kuilinda na kuitetea status quo ya CCM ili iendelee kutawala milele!. This is very wrong kwa tafsiri sahihi ya Public Servants!. Kwa kauli hii ya Pinda, it goes without saying kuwa wakuu wa majeshi yetu, Polisi wetu, mahakama zetu na wakuu na vyombo vya dola, na vyombo vya kiserikali, wanateuliwa ili wahakikishe CCM haishindwi na inaendelea kutawala milele!.

  Public Servant, ni mtumishi wa umma, ma RC na ma DC ni viongozi wa serikali, kwa maana hiyo ni viongozi wa umma, na watatimiza majukumu yao kwa maslahi ya umma na sio kwa maslahi ya CCM. Ndio maana Mhe. Tundu lissu aliwakataa hawa wasihusishwe ile tume ya katiba na juzi akasisitizwa hawapaswi kuwamo bungeni!.

  Hata wabunge wa kuchaguliwa, ni watumishi wa umma, japo wanateuliwa kwa tiketi za vyama vya siasa, wanachaguliwa na wananchi na sio na vyama vyao, hivyo wakishashinda ubunge, wanakuwa ni watumishi wa watu na sio watumishi wa vyama vyao, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao ya kibunge kwa maslahi ya wananchi na sio kwa maslahi ya vyama vyao!. Kama ni kweli, majukumu ya ma RC na ma DC ni kuhakikisha CCM haishindwi, hii ina maana kubwa zaidi katika mustakabali wa mabadiliko halali ya serikali!.

  Binafsi yangu, nimesikitishwa na kauli hiyo, and to be honest, nilikuwa na very high hopes kuhusu Pinda, lakini sasa nimeamini, he is good for nothing!, a very disapointing PM!. Kwa vile CCM ni chama tawala, hivyo public servants wana jukumu la kuhakikisha CCM inashinda na kutawala milele!.

  Hii inamaanisha hata kama 2015, Watanzania wataamua kuivote out CCM kupitia njia halali ya ballot box, hao public servanys wenye jukumu la kuitumikia serikali mpya ya chama kitakachoshinda, wako kwenye mind set ya kuhakikisha lazima CCM inashinda, na jee ikitokea CCM ikashindwa, jee watakabidhi madaraka kwa mshindi halali?!, jee majukumu yao yatabadilika or what does Pinda exactly meant?!. Hii maana yake, hata ikitokea wapinzani wakashinda kwenye ballot box, lakini ushindi wa jumla ni CCM!.

  Kusema ukweli, civic education kuhusu multipartism Tanzania, inatakiwa kuanzia juu ndipo ishuke chini kwa wananchi wa kawaida!.

  Sasa ndio nimeanza kuelewa, no wonder kwa nini jina la Pinda, halitajwi kabisa kabisa katika presidential materials!. Maliza tuu term yako kwa amani, ukaiendeleza ile kampuni yako ya P & P, nami nitakutangazia sana ile asali yako, ila nakuomba Tanzania yetu utuachie kwa amani, hii sio Tanzania ya CCM, CHADEMA au CUF!. Tanzania ni ya Watanzania wote.

  Kiukweli, mabadiliko yakija, hizi nafasi za ma DC na ma RC ndizo ziwe za kwanza kufutiliwa mbali!.

  Very Disapointed!.

  Paskali.

  NB. Paskali ni Mtanzania mzalendo, Mwandishi wa habari wa kujitegemea ambaye sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mkereketwa wa maendeleo, mzalendo kwa kutanguliza mbele Utanzania kwa maslahi ya Taifa.
   
 2. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Huyu mzee sijui hata kwa nini alipewaa uwaziri maana saa zingine namuona kama hajui nini anafanya maana mambo yake tu anaoneken mfata upepo kutoka mjengoni....
   
 3. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,437
  Trophy Points: 280
  Pasco kakangu,

  Unajua fika kuwa watumishi wengi serikalini wanafanyishwa kazi kwa mtindo huu.

  Kwangu sishangai, na bado tunajigamba tuna demokrasia. Kauli hii wengi mliitarajia toka kwa Nape au Mukama, sasa ndio mjue tuna ombwe la uongozi kama taifa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  MKP Ameisha fikia ukomo wa kufikiria hawezi kuwa na jipya
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Tulisema hapa tangu anaapishwa, kwamba huyu jamaa bomu, watu wakaona tunaendekeza tahariri.

  Sasa mnaona.

  Na zaidi ya Pinda, tatizo ni system iliyomlea Pinda, maana huyu ni graduate wa UDSM aliyefanya kazi Usalama miaka mingi, akakaa kwenye corridors of power Ikulu huko, akagombea ubunge akapata, akapewa u PM.

  Sasa inaonekana institutions zetu zote hizi hazijaweza kumuandaa vizuri kwa kazi hii.

  Kuanzia elimu ya chini mpaka ya juu shahada ya sheria, usalama, Ikulu, bungeni, uwaziri, mpaka uzoefu wa miaka yote hiyo aliyokuwa PM, bado anacheza makidamakida mpaka leo.

  Pathetic.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa maana hiyo wakuu wa mikoa na wilaya wanatumikia chama cha siasa (CCM). Mashangingi, mishahara na posho zao zinatoka kwenye CCM au hazina?

  NB: From now on, wakuu wa mikoa na wilaya ni fair game, si viongozi wa serikali tena bali ni makada wa chama cha siasa. Hivyo, wananchi wana haki ya kuwasikiliza/kuwapuuza kama wanavyofanya kwa wana-CCM wengine i.e Nape & co. Naona giza!
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  CCM wana viongozi aina kadhaa wa kadhaa

  1,kuna wezi ambao ni wachapakazi kidogo

  2.wezi wazembe

  3.wachapakazi but uwezo mdogo


  sasa Pinda ndo group la mwisho
  na wanaonekana better kulinganisha na wengine
   
 8. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pasco
  Mh Pinda yuko sahihi kwa mfumo wa nchi yetu maana tumerithi ule wa chama kimoja.
  Ukiangalia kwa ukaribu, RC na DC ni baadhi ya wajumbe wakuu wa CCM kwenye maeneo yao ya kazi. lakini huwezi kuona wanakuwa wajumbe wa vikao vya opposition parties.
  Na hii ndo kazi yao kubwa honestly. Ameongea ukweli japo ni mchungu but in reality kama uko mikoani, utaona ndo ukweli.

  RC na DC hawatakiwi tena kwenye katiba mpya. Tunahitaji RAS na DAS na DED tu. Ukiingia kwa undani, hata DAS hana kazi ya muhimu.

  Pinda amewafungua masikio watu wengi na itasaidia kwenye maoni ya katiba watu kulijadili jambo hili.

  pole for being dissapointed Pasco, ila huo ndo ukweli. kama huamini toka da uje uishi kwenye mikoa mingine. Utauona huu upuuzi kwa uwazi kabisa
   
 9. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,437
  Trophy Points: 280
  FJM,

  Wapinzani wanatakiwa ku-capitalize katika hili. Hutuhitaji wakuu wa Mikoa/Wilaya. Binafsi sioni umuhimu wa watu hawa zaidi ya kuliingiza taiga ktk gharama zisizo na kichwa wala miguu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pasco, mkuu wangu hivi kweli wewe ulitegemea vinginevyo? Si afadhali huyu mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda kaweka wazi mjue kabisa kwamba mfumo uliopo ndio umetufikisha hapa tulipo na ndivyo itakavyokuwa hivyo jiandaeni..

  Mh. Pinda anaweza kabisa kusema uongo wowote kuwapaka mafuta, lakini ukweli unabakia kuwa kipenzi cha Mungu. Pinda kasema wazi nini wanakitaka hivyo ni kujumu la vyama vya upinzani kuzipata salaam hizo. Politically anaweza kuwa wrong lakini ndivyo inavyokuwa..Tujifunze mara ngapi mkuu wangu.
   
 11. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sikumbuki ni lini nilikubaliana na pinda kwa lolote!
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama PM anaelewa madhara ya hiyo kauli yake kwa CCM. Kwa bahati mbaya sana, viongozi wengi serikalini na hata ndani ya ccm wako nyuma sana. Sintofahamu inayoondelea ni kwa sababu wananchi wamepiga hatua lakini wakubwa wanazidi kucheza zilipendwa. Viongozi wanaonekana kufanya mambo ya aibu sana na unaposikia kauli kama hii ya Pinda you have to ask yourself kama alikuwa holiday sayari nyingine ambayo hakupata mawasaliano toka Tanzania au the 'dear leader' is simply out of it?
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Bitabo, hapa ndipo watu wanaona dhulma na matumizi mabaya ya kodi za walalahoi. Kwa miaka yote ishirini tangu mfumo wa vyama vingi viingie, tumeendelea kugharamia makada wa propaganda. Sasa hivi tuna wakuu wa wilaya 130 na ushee, wakuu wa mikoa 27 hapo kila mtu ana shangingi, anapata allowance kila kukicha. Tunapata faida gani?

  Huu uvundo ni wa kusafisha kwenye hii katiba mpya, but for now they should be treated kama makada wengine wa CCM!
   
 14. O

  Original JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kauli ya Pinda ina maana kwamba kuanzia usalama wa taifa, polisi, jeshi, mahakama vipo kuhukikisha ccm inatawala milele huku wakitumia pesa ya watanzania?, huo ni upumbavu uliopita kiasi.
   
 15. A

  Al Adawi Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Kiongozi Mkandara,
  Unafahamu hata yule Jemadari Jacki Zoka anahudhuria vikao vya juu vya CCM? Unaiona hatari ya kuwa kama alivyosema Mkuu Pasco kuwa wenye Nchi siku wakiamua kuipiga chini CCM, basi uwezekano ni mkubwa yakawa yale ya Kibaki na Wakenya,2008. Safari ni ndefu bado.
   
 16. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Nishaona dalili za kupasuana hapa! Kama wakuu wa mikoa na wilaya watapewa nafasi ya kupiga kampeni huku wengine wananyimwa vibali vya kukusanyika itakuwa ni sababu tosha ya amani kuanza kutoweka! Am worried
   
 17. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Watu husema, ukitaka kumuua mwendawazimu (unaweza kumuita silly, mzembe, dhaifu), usinyanyue mkono wako bali mpe kitanzi atajimaliza mwenyewe. Kamanda Lissu amempa kitanzi Pinda amejimaliza mwenyewe, ni suala la muda tu.

  Kwa kauli hiyo, ni kuwa zile ahadi zaviongozi wetu kuwa "nitawatumikia Watanzania bila ubaguzi" inakuwa ni uongo ndani ya kiapo kitakatifu. Ikiwa wakuu wa wilaya na mikoa, jeshi, polisi, mahakama (wote kama watumishi wa umma) wapo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa CCM inashinda Liwalo naliwe, na mbaya zaidi wapo hapo walipo kwa mishahara na marupurupu ya jasho la Watanzania, hii ni dhuluma na wizi wa mchana. Nani atakayekuwa na imani tena na watumishi wa umma, akiwemo yeye Pinda? IKO HAJA YA KUREJESHA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU HUYU.

  Ninachosema, kwa ithibati ya maneno ya Pinda (anayepindisha haki ya Watanzania kuwa dhuluma kwa Watanzania), CCM imezidi kukosa uhalali wa kuiongoza Tanzania.
   
 18. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hivi hawa ma RC na DC si ndio Anna Kilalgo aliwatetea kuwa wawemo katika uratibu wa katiba mpya? Fikiria sasa ni upendeleo kiasi gani kwa CCM watakao uonyesha! Vyeo hivi vifutwe kabisa ndani ya katiba
   
 19. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco you have a point. Mimi mchango wangu ni mfupi tu. Vipi kuhusu ukweli kwamba makamanda wa JWTZ nao huteuliwa kuwa ma-RC na DC? Kumbe jeshi pia hutumika kisiasa?
   
 20. M

  Magesi JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Serikali imechoka
   
Loading...