PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

Nataka PM ajue kuwa kauli yake ni mbaya sana kwa mustakabadhi wa Taifa letu.

Sasa ni dhairi wananchi watakuwa wanasusia mikutano ya MaDC wakidhani ni mikutano ya chama cha siasa.

Sasa haoni utendaje wake utakuwa mgumu? Duh! hii nchi kunahitajika jitihada za makusudi ili kuweza kuleta Utawala bora.

Pinda alijisemea kama mtu aliyekata tamaa "Na liwalo na Liwe" hii ni hatari kwa mstakabali wa Taifa.
 
Pinda ni wa hovyo Siku zote kila wazo lake limefeli, kilimo kwanza, bajaji za wajawazito ujinga mtupu.

In fact Hana talent ya mamlaka, uongozi na hajui neno la kutamka anapokuwa bungeni. Alincha hio kipindi kile aliposhindwa kumwajibisha yule Katibu Mkuu wizara ya nishati na madini eti raisi hayupo anamsubiri, too bad for him.

Nimefurahi umesema wewe Pasco wangesema CHADEMA?
 
Nataka PM ajue kuwa kauli yake ni mbaya sana kwa mustakabadhi wa Taifa letu!! Sasa ni dhairi wananchi watkuwa wanasusia mikutano ya MaDC wakidhan ni mikutano ya chama cha siasa!! Sasa Haoni utendaje wake utakuwa Mgumu? Duh Hii nchi kunahitajika jitihada za makusudi ili kuweza kuleta Utawala bora!!
Pinda alijisemea kama mtu aliyekata Tamaa!! "Na liwalo na Liwe" Hii ni Hatari kwa mstakabali wa Taifa!!


Hapa la kufanya ni kwendakuwaambia wananchi wetu, mikutano ya madc na rcs wasiende Kwani ni ya ccm.
 
Pasco ur very right lakini huo alioeleza Pinda ndiyo ukweli we must face it that is why we need a New constitution ili kuondoa huu ujinga.
 
Hawa wakuu wa wilaya sioni kazi yao mm,wapigwe chini tuwe na wakurugenzi wa wilaya tu,maana ndo watendaji,sasa hawa wanawekwa kwa maslahi ya chama hawana wanachofanya,hawa wapo kwa maslahi ya mzee wa safari tu!!chandarua oyeeeee....!!
 
Pasco, this time umejitahidi kuwa na macho mazuri kuliona hili katika mtazamo sahihi. Pinda kalewa madaraka. Ni vizuri kuwa amezidi kuuonyesha umma wa Tanzania his true colours
 
Tulisema hapa tangu anaapishwa, kwamba huyu jamaa bomu, watu wakaona tunaendekeza tahariri.

Sasa mnaona.

Na zaidi ya Pinda, tatizo ni system iliyomlea Pinda, maana huyu ni graduate wa UDSM aliyefanya kazi Usalama miaka mingi, akakaa kwenye corridors of power Ikulu huko, akagombea ubunge akapata, akapewa u PM.

Sasa inaonekana institutions zetu zote hizi hazijaweza kumuandaa vizuri kwa kazi hii.

Kuanzia elimu ya chini mpaka ya juu shahada ya sheria, usalama, Ikulu, bungeni, uwaziri, mpaka uzoefu wa miaka yote hiyo aliyokuwa PM, bado anacheza makidamakida mpaka leo.

Pathetic.

How do we groom our future leaders? Do we have any breeding sites for the new ones who aspire to get into the system? Vinginevyo tutaendelea kuongozwa na jamaa hawa wanaojuana sababu ya kufanya kazi kwenye institution hizo za serikali. Wengine hawana sifa za kuwa viongozi...na wengine wana sifa za uongozi lakini hakuna anayejua potential yao.
 
umeteleza, pinda uwezo hana, amezoea kutumwa.
CCM wana viongozi aina kadhaa wa kadhaa

1,kuna wezi ambao ni wachapakazi kidogo

2.wezi wazembe

3.wachapakazi but uwezo mdogo


sasa Pinda ndo group la mwisho
na wanaonekana better kulinganisha na wengine
 
jibu hili litamkost sana Pinda na ccm kwa ujumla,Na nampongeza sana F.Mbowe kwa kuulizj swali hili
 
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, sipendi kabisa kukosa kipindi cha Maswali na Majibu ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza, Peter Pinda, ile leo nilikikosa kipindi hiki.

Lakini kupitia taarifa za habari, nimemsikia Mhe. Pinda, akisema kuwa ni jukumu la wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha CCM haishindwi ili CCM iweze kuendelea kutawala milele!.

Naombeni wajuzi wa masuala ya utawala, minirekebishe if I'm wrong!, Kuanzia kwa rais JK na wanasiasa wengine wote ambao japo wamechaguliwa kwa tiketi za vyama, ukishakuwa mtumishi wa umma, paid by taxpayers money, jukumu lako kuu sasa ni kuutumikia umma na sio chama chako!.



NB. Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida ambaye sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mshabiki wa Utanzania kwa maslahi ya Taifa mbele!............

Pasco mimi sikukiona, ila sishangai, mimi ni mwanachama haswa wa CCM, na hili ndilo tatizo kubwa la hawa viongozi wa "Serikali" wanaoingia madarakani kwa tiketi ya CCM, na CCM inaonekana kituko kwa tabia hii sijui kama wanasoma alama za nyakati.

Watu ni waelewa kupita maelezo, na hasa kundi hili kubwa mno la vijana wanaoelimishwa na darasa la ulimwengu kupitia media ambayo kila mtu anai-access.Kauli hizo zilifaa kipindi kile tunaingia kwenye vyama vingi.

Kutoa agizo la kuhakikisha wanashinda bila kutoa muongozo na kusisitiza misingi itakayowafanya washinde itapelekea muendelezo wa mbinu chafu za kijinga zinazokiletea chama aibu kila siku.

Hawa wanatugawa sijui kama wanajitambua, kwakuwa wanadhani wao ni CCM na wengine si wao wakati madaraka waliyonayo yanapaswa kuwa ya kuwatumikia watu wote bila ubaguzi wowote na hata kauli zao zisimame katka misingi hiyo.

Kauli kama hiyo alitakiwa atoe katibu Wilson au Nape kwa wadhifa wake. Mnakitia doa chama, na ndiyo mnakipeleka pabaya, hebu rejeeni misingi ya CCM mwanzo kabisa mwa katiba, yaani hiyo peke yake mkiihubiri, kwa vitendo, ni vigumu chama kingine kuwayumbisha. Mh Pinda, please!
 
Tangu Tanganyika kupata uhuru hutujawahi kuwa na WM bogus kama huyu. Sijui Mkuu wa Kaya aliona nn kwake hadi akampa kazi asiyoweza. Huyu alitakiwa aendelee na ile kazi yake ya umbea
 
Niliwahi kuandika tena hapa kuwa Pinda huwa ni mropokaji, kuna muda ambapo mdomo wake huwa unatangulia fikra ya anachotaka kukisema, nadhani wote tunakumbuka kauli juu ya wauwaji wa albino (alipokumbushwa kuuhusisha ubongo kwa shinikizo akarudi bungeni na kulia), kisha tukumbuke kuhusu posho za wabunge, kumbuka tena kuhusu kauli ya 'liwalo na liwe'.

Busara inaanza kusogea mbali nae jinsi muda unavyozidi kwenda mbele, eti CCM itawale milele?! hivi anajua analolimaanisha?! Au ndo wanataka kuturudisha kwenye chama kimoja?!

Kwa miaka aliyokaa kwenye uongozi wa taifa hili, naona ni mtu aliyevimbiwa madaraka, sasa amejisahau.

Lakini, kauli yake sio ya kuchulia kimzaha, sababu kauli hizi zitokazo kwa wakubwa huchuliwa na wadogo kama amri, na tukumbuke kwamba ukuu wa mikoa na wilaya ni nafasi 'wapewazo' watu kama kama 'ulaji' kwani kimsingi hakuna vigezo vilivyo wazi na madhubuti vya kuwapata, hivyo kulipa fadhila ni kitu kisichokwepeka, kwa hiyo tutegemee utekelezaji wa hili pia.

Ila cha muhimu 'watawala' wetu wajue tu kuwa hakuna chama kinachoweza kutawala milele, hakipo.
 
NB. Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida ambaye sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mshabiki wa Utanzania kwa maslahi ya Taifa mbele!.................[/QUOTE]
nimeipenda hii ya kwenye blue,uozo wa Pinda namuacha mwenyewe, pale bungeni wanapoteza muda tu hakuna tija.
 
Lakini Pasco wewe uliliona jana? Pathetic, Pinda hata migogoro ya UDOM imemshinda, alijichanganyaga na waziri Nahodha(HOME AFFAIRS) na Kawambwa(ELIMU) wakati wa migomo.

Seuze TAMISEMI, jamani Utawala ni mgumu sana tawala za mikoa na serikali za mitaa. Mkapa pekee aliimudu TAMISEMI, tena kwa kumpa uwaziri mkuu yule mchaga. Yule sikumbuki jina.
 
Kwa hili mimi namsifu sana Mheshimiwa Mizengo Kayanda Pinda kwa kuwa muwazi na mkweli kuhusu kile ambacho wakuu wa wilaya na mikoa wameajiriwa kukifanya.

Angesema vinginevyo angekuwa anadanganya na nisingemwelewa. Ukweli ni kuwa mawaziri, makatibu wakuu, makamishna, wakurugenzi, wakuu wa mashirika na taasisi za umma, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na watendaji wote wana kazi sawa kabisa na hizi za wakuu wa wilaya na mikoa linapokuja suala la kuhakikisha chama tawala kinashinda chaguzi zote.

Mfumo tulionao ni wa chama kimoja na wakati unajengwa hakukuwa na wazo la kukiondoa chama tawala madarakani.

Tulitapeliwa kuwa umebadilika pale serikali na chama tawala walipofanya kiini macho cha kuruhusu vinavyoitwa vyama vya upinzani bila kubadilisha misingi ya mfumo uliokuwepo wa chama kimoja ambao uliundwa kuhakikisha chama tawala haking'oki madarakani.

Maelezo ya ukweli na uwazi ya Mh. Pinda yatatusaidia sana kwenye mchakato wa katiba kuona kama bado tunahitaji wakuu wa wilaya na wa mikoa ambao ni wanasiasa wenye kazi moja kubwa ya kuhakikisha chama tawala kinashinda.

Hii haijalishi ni chama gani kiko madarakani kwani hata CHADEMA au CUF wakiingia madarakani chini kwa katiba hii ya sasa na mfumo huu wa sasa wa utawala watachagua makada wa vyama vyao kuwa wakuu wa wilaya na mikoa wenye kazi ya kuhakikisha vyama vyao havishindwi kwenye uchaguzi.
 
Tangu Tanganyika kupata uhuru hutuwahi kuwa na WM bogus kama huyu. Sijui Mkuu wa Kaya aliona nn kwake hadi akampa kazi asiyoweza. Huyu alitakiwa aendelee na ile kazi yake ya umbea................

ila aliyemteua,he's smart.
 
Kusema ukweli, civic education kuhusu multipartism, inatakiwa kuanzia juu ndipo ishuke chini kwa wananchi wa kawaida!.

Sasa ndio nimeanza kuelewa, no wonder kwa nini jina la Pinda, halitajwi kabisa kabisa katika presidential materials!. Maliza tuu term yako kwa amani, ukaiendeleza ile kampuni yako ya P & P, nami nitakutangazia sana ile asali yako, ila nakuomba Tanzania yetu utuachie kwa amani, hii sio Tanzania ya CCM, CHADEMA au CUF!. Tanzania ni ya Watanzania wote.

Kiukweli, mabadiliko yakija, hizi nafasi za ma DC na ma RC ndizo ziwe za kwanza kufutiliwa mbali!.

Very Disapointed!..............
wakati Yesu akisulubiwa wafuasi wake walisikitika sana lakini yeye alisema ilibidi hayo yatokee ili wokovu upatikana na unabii utimie.

Kwa maana hiyo wanaopinga vyeo vya RC na DC hapa pale walipokuwa hawajaeleweka sasa wanaanza kueleweka ni kwa nini wanataka nafasi hizi zifutwe. Na unaweza kuona zinafutwa baada ya kuliingizia taifa hasara kiasi gani!!!

"Hatutaendelea kupitia ujinga endelevu"
-
Jenerali Ulimwengu

 
Huyu mzee sijui hata kwa nini alipewaa uwaziri maana saa zingine namuona kama hajui nini anafanya maana mambo yake tu anaoneken mfata upepo kutoka mjengoni....

wamekamata,wameirarua na kuibaka katiba yetu.so kila mteule wa raisi yupo kwa manufaa ya rais na chama chao cha ccm.poor tanzania
 
Back
Top Bottom