PM Confirm the New MPs Sitting Allowance

PM Confirm the New MPs Sitting Allowance

Dah imekula kwetu tena....kelele zoooote kumbe ilikuwa kazi bure!
Hivi nani serikali hii atasikia kelele zetu, mzee wa magogoni, JK the explorer alishasema kelele za mlango hazimzuii yeye kupata usingizi pale magogoni. Pigeni kelele mwisho wa siku wanaendelea na mambo yao.

Inauma sana jinsi watanzania tunavyodharauliwa na hawa viongozi wezi wetu. Yaani kuna mgomo wa madaktari na ndio hapo hapo wanaongezeana posho officially, hata soni hawana. :embarassed2:
 
The PM says, he was asked by the President to deal with the matter. It is against the law for a PM to approve new rates.
Sijaambua kitu hapo....Ufafanuzi please!!!!!

Ni hivi..PM kawaambia wana habari (Ma-editor) kuwa kaagizwa na mkuu wa kaya ashughulikie suala la posho ya watu wa mjengoni pale Idodomya...Sasa Kamanda Zitto ana-wonder, inakuaje Mkulima anashughulia suala hilo yeti kwanza suala lenyewe halipo kisheria lakini vile vile hata kama lipo, sio yeye anayepaswa ku-deal nalo!
 
Kumbe hela ipo,sasa kwanini deni la watumishi wa umma linazidi kuongezeka?Endeleeni tu siku raia uvumilivu ukiwashinda hapatotosha!!
 
The PM says, he was asked by the President to deal with the matter. It is against the law for a PM to approve new rates.

Ni hivi..PM kawaambia wana habari (Ma-editor) kuwa kaagizwa na mkuu wa kaya ashughulikie suala la posho ya watu wa mjengoni pale Idodomya...Sasa Kamanda Zitto ana-wonder, inakuaje Mkulima anashughulia suala hilo yeti kwanza suala lenyewe halipo kisheria lakini vile vile hata kama lipo, sio yeye anayepaswa ku-deal nalo!

kwahiyo viwango vipya vya posho havijapitishwa
 
Kama kilichoandikwa ni kweli, kuna vacuum kwenye presidency.
 
Mimi naona 200,000 ni kidogo sana kwa mbunge, unless uwe umeshawekeza kama Zitto kwenye ma biashara mengine.

Duh. Ila madaktari wakitetea maslahi yao kosa. Wanachuo nao kosa, utaambiwa wanashinikizwa na CHADEMA! Is inflation rate high to the MPs only? Pathetic.
 
Uikisikia nini maana ya kudhalauliwa, basi huko ni kudhalauliwa kweli kweli. wabunge ni kama nani hapa tanzania? kila kitu wapate wao tuu huku watoto hawali shuleni! magereza hayana TV!polisi wanatembea kwa miguu barabarani kulinda usalama badaya ya kuwa na magari! hakuna public shool bus kwa wanawetu!

umeme haujafika vijijini baada ya miaka 50 ya uhuru! kweli hili bunge linajenga nchi au linabomoa? jamani tuandamane kulipinga hili swala , la sivyo dunia itatudhalau kuwa sisi ni mandiyo ndiyo senti sabini, moja lako na moja langu!

wabunge wamegundua machimbo ya uranium, hivyo wanaila revenue hata kabla haijamfikia mlala hoi! kweli ujamaa na kujitegema hulea viongozi na bunge binafsi.
 
The PM says, he was asked by the President to deal with the matter. It is against the law for a PM to approve new rates.

Ni hivi..PM kawaambia wana habari (Ma-editor) kuwa kaagizwa na mkuu wa kaya ashughulikie suala la posho ya watu wa mjengoni pale Idodomya...Sasa Kamanda Zitto ana-wonder, inakuaje Mkulima anashughulia suala hilo yeti kwanza suala lenyewe halipo kisheria lakini vile vile hata kama lipo, sio yeye anayepaswa ku-deal nalo!

ukistaajabu ya Mussa...
 
Jamani serikali inatupeleka wapi/wananchi wa kawaida wanalalamikia maisha kuwa magumu,madaktari wanagoma hawasikilizwi ila wabunge wamepandishiwa posho tena kinyema na sheria uwiii tufanye mabadiliko jaman
 
Ndiya maana Madaktari wanaacha taaluma yao, wanakwenda kugombea ubunge.
 
Mimi naona 200,000 ni kidogo sana kwa mbunge, unless uwe umeshawekeza kama Zitto kwenye ma biashara mengine.
Kweli ni ndogo sana. tatizo ni kukosekana kwa justification ya kuongeza kwa kiwango wanachoongeza Vs malipo ya watu wengine
 
Bila shaka Posho zinawekwa ili nyie wenyewe wanasiasa muanze kuuana ktk uwanja wa kugombea ubunge ndani ya vyama na nje ktk kamati za bunge mkasahau mambo muhimu ya ujenzi wa Taifa. Vita inaanza baina yenu wenyewe.
Waswahili wanasema mwenye njaa mpe mkate! atakupa hata mwanaye..Mimi naamini kabisa huu mpango unafanywa makusudi ili kuondoa UZALENDO wa wabunge na wafikirie matumbo yao kwanza.
 
Kwani ubunge ni chanzo cha kujiongezea kipato? Wako pale kutumikia wananchi waliochagua. Maslahi ya wananchi kwanza,matumbo yao baadaye.

Hawa watu wanatakiwa wawe wanalipwa na majimbo yao kwa kuwa ndiyo wanaowatuma. Hiyo itasaidia kuwaamsha wapigakura wao na kuwa makini nao. Haiwezekani mtu kukaa akitimiza wajibu wake alipwe mihela yote hiyo. Itapunguza matumizi kwa kuwa halmashauri masikini hazitakubali upupu huo. No other way ya kuwaamsha wananchi kwa kuwa sasa hawajui kama zile hela zinatokana na kodi zao. Walipwe na wanaowatuma.
 
Wanachaguliwa na wananchi. Lakini wanafuata ilani ya vyama vyao. Posho wapewe na wananchi ambao hawasaidii kwenye shida zao. Mimi nachanganyikiwa na system ya representation kwenye bunge.

No problem can be solved from the same consciousness that created it.

Back
Top Bottom