Kiukweli tu, zile media houses kama EA Radio&Tv na Clouds, na hata huyu mfata mkumbo bw Millard Ayo wamesalimu amri kwasababu zifuatazo:
1. Ukuaji kimuziki ikiwemo kutoa hit songs kwa wasanii waliochini ya Label ya WCB, kumepelekea hizi media kupata pressure kwa wasikilizaji wao kwa nyakati tofauti kuomba baadhi ya ngoma za wasanii wa hii label kuchezwa ktk vipindi vyao
2. Uwepo wa Wasafi redio&Tv, ambao umechangia kupunguza uMungu watu kwenye hizi media IPP na Clouds, kwani hii media imepata mapokezi mazuri kwa halaiki ya watu hvyo kupelekea hata wasanii wa WCB kutotegemea tena media kama Clouds, EA Radio nk eti wapeleke nyimbo zao ndipo wasikike
3. Skendo karibu kubwa kubwa na zinazokiki zinahusu wasanii wa WCB, hvyo kuwafanya wasikilizaji wengi kuwa na shauku ya kutaka kusikia ishu zao ambapo fursa ya kusikia mambo yao utaipata kwenye Wasafi radio.
Na hii ilipelekea mpaka kipindi cha Shilawadu kupoteza watazamaji kwakuwa waliacha kuripoti mambo ya akina Diamond na wenzake ilhali hawa ndio gumzo la nchi kwa sasa.
Hizi ni baadhi tu ya sababu zilizopelekea hawa jamaa kusalimu baada ya kuwabania kwa kipindi kirefu wasanii hawa wakijua hawatotoboa, lakini mapinduzi waliyoyafanya hasa Diamond na uongozi wake kina Sallam Sk na Tale umewapa milleage kubwa sana kimuziki África na dunia