Mtangazaji na msanii nani anambeba mwenzake?

Mtangazaji na msanii nani anambeba mwenzake?

sangujoseph

Senior Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
164
Reaction score
184
By Sangu J
.
Katika maisha yangu ya Kitaaluma nimekuwa nikijiuliza sana nani anastahili heshima kwa mwenzake kati ya Msanii na Mtangazaji ni swali ambalo leo nadhani
nimelipatia majibu.
.
Ni mara chache sana kuona Watangazaji wakiingia kwenye bifu au kupishana na wasanii kwa sababu mara nyingi ya uoga wa Wasanii kuhofia huenda akigombana na Mtangazaji bifu lake litaishia kwa yeye kwenye kuzimiwa ngoma zake kwenye kituo husika.
.
Tuje kwenye uhalisia wa sasa ambao kuna ushindani mkubwa wa media ambapo kunaClouds FM, Wasafi FM , EFM, EA Radio kila Radio inapambana kuwa namba moja, je nini media zinahitaji kwa wakati huu.
.
Rafiki mkubwa wa Media kwa sasa ni Wasanii, Watangazaji wengi wamekuwa wakawaida kutokana na uwepo wa ushindani wa maudhui, kwenye vituo vyao kwa hiyo inatokea media ambayo imefanikiwa kuwafanya Watangazaji wake kuwa wakubwa ndiyo inakuwa pendwa zaidi nje kuliko media nyingine.
.
Nimefurahi sana kuona ugomvi wa muda mrefu ukiendelea kati ya @divatheebawse na @diamondplatnumz ,lakini kwa Dunia ya sasa ya ushindani wa Media, @cloudsfmtz wanakuwa wamefaulu kutokana na ushindani media ulipo sasa.
.
Je ni sawa kwa Watangazaji na wao kuishi kama wasanii au kulazimisha umaarufu aliokuwa nao Msanii na yeye awe nao, kwa jicho la Kibiashara kwa sasa kwenye Media ni vitu ambavyo vinahitajika sana sana, kwa sababu ile ya Formula 'Anayetrend Ndiye Namba 1', anachokifanya Diva ni kitu kikubwa sana kwake na kipindi chake, na mara nyingi huwa tunavikosa kwenye media nyingi.
.
Moja ya matatizo makubwa ya media ambayo mimi binafsi nimeyaona kwa sasa ni kukosa 'Key Presenter' yaani hakuna mtu ambaye akisimama mahali unasema huyu ni mtu fulani kutoka sehemu fulani, kuanzia muonekano, matendo, mavazi, Brand Managing (ukimtoa Bdozen.)
.
Nakumbuka mara ya kwanza nilimfahamu Producer wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Grayson Gideion kwa sababu aliingia kwenye mrushiano wa maneno na mkongwe Ray C, kwa hiyo vitu kama hivi vikienda fairly bila kuingiza masuala ya Ofisi nadhani itatoa lifti kote kuanzia Msanii, Media, Mtangazaji na game ya Sanaa na game ya Utangazaji.
.
Mwisho pia nadhani pia tunahitaji kuona Watangazaji wakiingia kwenye Trending na Watangazaji wenzao, hii inachangamsha sana game ya Media ya Bongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom