BONGO FLEVA: Sababu zilizopelekea muziki wa bongo fleva kukosa mvuto tofauti na zamani

homeless1

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
427
948
Wiki hii niliamua ku download nyimbo mpya za bongo ili zinifariji kwenye hichi kipindi kigumu cha maisha sababu na amini burudani ya muziki ni rahisi kukupunguzia mawazo, Nilikosa radha halisi ya bongo na sikupata hata nyimbo ya kunifariji nikahisi labda sababu ni mimi kua na mambo mengi lakini baada ya kufikiria nikagundua muziki hauna radha kama zaman na hizi ndo sababu ninazoona zimetufikisha hapa

1. Production, producers wa sasa hivi wanaleta midundo inayochosha kuisikiliza imagine huwezi ukapata producer ambae ameliteka soko sababu ya midundo yake mikali,Zaman tulikua na p funk majani baba paula ,Master J,Mika mwamba,Nahreel na wengine kibao wakali hawa watu walileta midundo mikali ambayo msanii hata akiimba vibaya bado inambeba, chukulia mfano nyimbo za Mr nice midundo yake au hata mpenzi ya Dudu Baya aliyoandaa mika mwamba,Fagio la chuma,au hata Pico kikongwe nyimbo wasanii wanaimba kawaida ila midundo iliwabeba,,,Huwezi amin P funk aliandaa midundo mikali kwa vifaa vya kawaida tena ghetto kwake hili kathibitisha kipindi kajala anawekwa kinyumba kwa siri akiwa mwanagunzi alisema kua alikua analala na kujifunika blanket kuogopa aibu ya kuonekana mwanafunzi mzinzi wakati kina Juma nature wanatengeneza hits zao

2. Ideas na Melodies, Idea za sasa ni nyepesi mno na melodies ni za kawaida sana,yaani wasanii wa sasa hawajui kuumiza kichwa,Idea karibu zote ni za mapenzi utawasikia wasanii jinsi gani wanaumizwa,au jinsi gani wanapenda,au jinsi gani wanajua kufanya mapenzi ,au jinsi gani mademu zao wazuri na wana maumbo au hata wanawafikishaje kileleni, kuna muda wasanii walikua na idea za mapenzi nyingi zilikua tofauti na melodies zilisimama,mfano kipind kina linah na Barnaba wanatoa wrong number au Diamond anatoa kamwambie,mbagala..na idea zaman ziligusa kila angle za maisha na zilikua na melodies Kali sana

3. Uandishi, wasanii wa sasa sio waandishi wazuri na hata wanaowaandikia wasanii sio waandishi wazuri imagine eti Foby ni moja ya waandishi bora kabisa Tanzania na kawaandikia wasanii wengi lakin hata yeye hajiandikii vizuri,et chin bees nae mwandishi na ana jikubali ila Kila siku anaandika vilevile,Siamin bongo kwa sasa kuna msanii ananunua daftari kwa ajili ya kuandika tu kitu cha lazima kabisa kwa wasanii wa zamani

4. Matusi: jamani wasanii wa sasa wanajua kutukana nlikua nasikia All night ya harmonize mmakonde kaja na Nyimbo Kali sana alinikata maini aliposema anahamisha pale nilipozoea anataka niweke kwenye mtaro,nikasikia Baikoko ya Mbosso nikaishia pale Diamond aliposema demu anataka anipeleke kwetu pekupeku akamalizia kunduchi juu anifikishe kwetu,Yaan mondi afiki akila mbele mpaka nyuma,nikaacha nikatazama trace mziiki nikaskia bonge la mdundo na melod nikafungua shazzam kuupata wimbo ulikua Baila ya Malaika jaman ile nyimbo ni kali lakini huwezi kaa ukaimba au ukataman yaan uwekezaji wa ovyo kabisa,,,inaanza tu anaimba inapoingia pekupeku yan mpaka inazama.

5. Media conflicts: Hapa sasa ndo unaweza kuchoka kuna wiki niliskia top ten ya redio moja nikakuta Nyimbo namba moja haipo kwenye top 20 ya redio nyingine daaa yan kila redio ina Nyimbo zake bora mpaka kwenye chart zao ,matamasha yao Kila redio na wasanii wake

6. Kukopi ideas na beats toka nje, Saizi tofauti na zamani hatuna identity ya muziki wetu inaweza sound kama naija au hata south ,nakumbuka bongo fleva zamani tulipata radha halisi kabisa ya muziki wetu saizi tupo kuigaiga tu na ni kwa wote wasanii na producers

7. Upcoming Artist,: zamani tulikua na ma underground hata watatu wanaokuja kubadilisha game,saizi ma underground wanasaound kama wasanii waliopo kwenye game ,hii inauma sana underground wa nchi kama Nigeria wanawatoa kabisa wazoefu kwenye game nje ya reli chukulia mfano Tens,Tems,Simi,Omah Lay,Rema,Fireboy Dml,Ckay,niniola,ransome uje ufananishe na underground wetu mbingu na Ardhi

8. WCB, ni ngumu kuamini WCB empire mbali na kufanya vizuri lakini wamechangia sisi kutopata radha halisi ya muziki,sababu ni kua kwa sasa hawana Nyimbo Kali Lava Lava wa bora tuachane na ni huyuhuyu wa walewale,Mboso na Rayavan hawabadiliki tena afadhali na walivokua zamani ,Diamond yupo mbali sana kum Judge jamaa anajua,Zuchu ni upcoming nimuache,Queen hajui lolote, japokua wana peleka mziki international ila wanamadhaifu makubwa naliona hili hata kwa KM music na NLM

9. Bifu za wasanii, Bifu za wasanii was sasa zipo personal sana zamani zilikua bifu za kazi mfano East Coast na TMK, Fid Q na Joh Makini na wengine walifanya bifu kulingana na muziki wao,,Mfano wa bifu ya sasa ni Rayvan na Harmonize ipo too personal na zingine mnazijua

10. Kiki ,mziki wa sasa unakuja na kiki kubwa sana kupita wimbo yaani inakuja kiki hata unawaza ni Nyimbo gani itakuja kufunika hio kiki, zamani kiki ya Juma na Sinta ilileta inaniuma sana na sitaki demu,WCB na konde inaleta Vibaya, hakika wasanii mpo kutuonea

NB: pamoja na yote hongereni kwa video production mnakuja na videos Kali na zinavutia kutazama
 
,,,Huwezi amin P funk aliandaa midundo mikali kwa vifaa vya kawaida tena ghetto kwake
Acha masihara mkuu, P funk alikuwa anasoma shule ya IST ada zake zipo juu, kwa sasa ada zinafika hadi milioni 60 kwa mwaka, P funk alipenda mziki kuliko shule, wazazi wake wakakubaliana na uhaisia wakampeleka uholanzi kusomea mziki na aliporudi alipewa mtaji wa takribani milioni 100 zinazoendana na thamani ya hela ya sasa.

Pia watu wanachokoseaga ni kudhani p funk alikuwa anatembea na biti lote, HAPANA!! pfunk kamtumia sana bizman kwenye kinanda, kamtumia mzungu kichaa kwenye gitaa kwenye ngoma kama she got a gwayne, kasaidiwa na kina soggy doggy, n.k hii ndio ilikuwa maana ya kuandaa muziki.

Maproducer wa siku hizi yani kila kitu wanafanya wao hata kama kifaa flani cha muziki hawajui kutumia, matokeo yake hata biti linakosa mvuto

Ila yote kwa yote jamaa alikuwa mkali
 
Daaah sijui nmecheka
Pia wanabana sana pua, wimbo unakosa mvuto... Zamani ilikua ukiskia nyimbo kwa mbali unajua huyu msanii gani.
Wasanii wa saivi sauti karibia zote zinafanana
 
Wewe ndio unamatatizo, sio kweli kwamba umekoswa nyimbo kali za kukufariji ila wewe ndio umefata nyimbo ambazo unaona hazikufai ilihali kuna nyimbo nzuri tu, labda Kama ukitaka kuongelea generally feature nzima ya muziki wetu ila sio kwamba umekoswa kabisa nyimbo nzuri, halafu hiyo point ya wcb sijui yann? Bora ungeandika LABELS generally..
 
Kaka sio masihara na nikwel simfaham vizuri P ila niliskia hayo maelezo nloyaongea juu kutoka kwa kajala masanja kwenye kipindi cha salama na marafiki zake alisema kua alikua analala kwa kina p funk bila wazazi wake kujua na P alikua na studio kwenye ghetto lake
Acha masihara mkuu, P funk alikuwa anasoma shule ya IST ada zake zipo juu, kwa sasa ada zinafika hadi milioni 50 kwa mwaka, P funk alipenda mziki kuliko shule, wazazi wake wakampeleka uholanzi kusomea mziki na aliporudi alipewa mtaji wa takribani milioni 100 zinazoendana na thamani ya hela ya sasa.

Pia watu wanachokoseaga ni kudhani p funk alikuwa anatembea na biti lote, HAPANA!! pfunk kamtumia sana bizman kwenye vibanda, kamtumia mzungu kichaa kwenye gitaa mfano she got a gwayne ya Mangwair (RIP), kasaidiwa na kina soggy doggy, n.k sio kila mziki katengeneza biti yeye

Ila yote kwa yote jamaa alikuwa mkali
 
Kaka mi nmeanza kupenda miziki ya aina tofauti toka 2000 na mziki wa bongo nna uwezo wa kuulezea vizuri toka kipindi hicho na nmeamua kusema bongo fleva pekee,

Naomba nitajie ngoma kali 10 za kipindi hichi ntakutajia 20 before 2010 alafu tufananishe unganisha kila aina ya mziki bongo


Kuhusu WCB nmewasimia kwa sababu hakuna hata lebo inayawakaribia kimafanikio lakin kwa sasa hakuna wanacho offer kwenye mziki taja ngoma zao 10 kali kwa sasa nkutajie 20 walipoanza na tufananishe
Wewe ndio unamatatizo, sio kweli kwamba umekoswa nyimbo kali za kukufariji ila wewe ndio umefata nyimbo ambazo unaona hazikufai ilihali kuna nyimbo nzuri tu, labda Kama ukitaka kuongelea generally feature nzima ya muziki wetu ila sio kwamba umekoswa kabisa nyimbo nzuri, halafu hiyo point ya wcb sijui yann? Bora ungeandika LABELS generally..
 
Tuliambiwa tutengeneze misingi na taasisi imara na siyo watu imara (Juma Nature, Mr Nice)
 
Kuna kitu kimoja tu miziki yote inatoka inafanana sana na hata uimbaji unafanana sana na mbaya zaidi hata wasanii wakubwa uimbaji ni kama wa nyimbo A hapa ndio kuna shida kidogo na ndio sababu mziki hauishi sana tuko katika views sio ubora wa nyimbo bali ubora wa video na views. Yanga anaweza kuwa sio team bora lakini ana views wengi na labda Azam wako vizuri sana lakini hawana views wengi ndio kama mziki hatungalii ubora ila nani ana washabiki wengi ndio maana kupata wanamuziki wapya shida sana hata akitoa ngoma nzuri sababu tumeunda Yanga, Simba, Azam katika muziki pia yale maafa katika soka ndio tumepeleka katika miziki. tuhukumu ubora wa kazi.
 
Isikie Elimu Dunia ya Daz Baba,unapata melody,beat Kali,ujumbe uloshiba na radha asili ya bongo aisee nyie acheni
Tuliambiwa tutengeneze misingi na taasisi imara na siyo watu imara (Juma Nature, Mr Nice)
 
Isikie Elimu Dunia ya Daz Baba,unapata melody,beat Kali,ujumbe uloshiba na radha asili ya bongo aisee nyie acheni
Chief ni ladha siyo radha.

Daz Baba nilimuona mkali sana kwenye Kamanda, Barua, Nipe 5, Wife na Namba 8.

Kulikua na jamaa anaitwa Snoop Lee ngoma yake na Mr Blue ilikua nzuri sana. Noorah on fire, kipindi hicho mabishoo wawili tu Bob Lee na Mr Blue, mshkaji wa Nimechezea Bahati alijaribu akashindwa.

Muziki ulikua kila sehemu FA na Jay Mo wanauliza Ingekua Vipi huku Sista P anatoa Hey Dj na ndani anajibu diss ya FA. Walume ndago wanatoa Ingekua Poa kujibu ngoma nzima ya FA.

Mabaga Fresh wakasababisha kila mwenye ulemavu aitwe Mabaga ngoma yao Tunataabika ilikua inachezwa redio kibao. Wagosi wa Kaya walifanya rap katun huku ina ujumbe mzito.

Ila naamini kuna ngoma hazitakuja kuzeeka kuna Nilikupenda Nakupenda ya Abby Skills ft Dully na Mtazamo ya Afande Sele ft Solo Thang na Profesa Jay.
 
Asante umetisha kinoma
Chief ni ladha siyo radha.

Daz Baba nilimuona mkali sana kwenye Kamanda, Barua, Nipe 5, Wife na Namba 8.

Kulikua na jamaa anaitwa Snoop Lee ngoma yake ni Mr Blue ilikua nzuri sana. Noorah on fire, kipindi hicho mabishoo wawili tu Bob Lee na Mr Blue, mshkaji wa Nimechezea Bahati alijaribu akashindwa.

Muziki ulikua kila sehemu FA na Jay Mo wanauliza Ingekua Vipi huku Sista P anatoa Hey Dj na ndani anajibu diss ya FA. Walume ndago wanatoa Ingekua Poa kujibu ngoma nzima ya FA.

Mabaga Fresh wakasababisha kila mwenye ulemavu aitwe Mabaga ngoma yao Tunataabika ilikua inachezwa redio kibao. Wagosi wa Kaya walifanya rap katun huku ina ujumbe mzito.

Ila naamini kuna ngoma hazitakuja kuzeeka kuna Nilikupenda Nakupenda ya Abby Skills ft Dully na Mtazamo ya Afande Sele ft Solo Thang na Profesa Jay.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom