Pisi kali, nipokeeni kwa mikono miwili.

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,480
40,491
Baada ya kuona warembo wetu, katika huu ukanda wetu, wengi wao ni omba omba, nikaamua nivuke mabara na mabara ili niweze kupata pisi kali matata, isiyokuwa omba omba.

Kwanza nilianza kwa kutafuta eneo zuri la kupigia picha; nikaamua kwenda kwenye maeneo ya miamba ili nionekane ni mtaalamu wa miamba.

Nikapiga kipara kichwa chote, kikawa kinang'aa; nikavaa jinsi yangu ya blue, pamoja na shati jeupe linaloonyesha vesti kwa ndani, nikawa nimechomekea; wakati mpiga picha ananichukua nilikuwa nimeshikilia jiwe kubwa nikijaribu kulidodosa kama kuna madini yoyote ndani (kumbe ilikuwa ni mazingira ya kuzugia tu).

Hiyo picha nikaenda kuipakia kwenye mtandao wa kijamii mmoja, nikaandika, ''Where is a queen, the king is here''.

Baada ya kama nusu saa hivi, hiyo picha ilipendwa kweli na warembo wa huko duniani, wengi wao wakitokea Marekani, wachache India, Ghana na South Africa.

Nikajua mtego wangu unakaribia kunasa pisi kali; nikaanza kupitia 'profile' ya mmoja mmoja, kwa wale wote walio 'like'; wengi wao wameachana na wapenzi wao, wengine walipeana talaka, na wengi zaidi wakawa hawa wanamitindo 'model'.

Kuna mmoja kutoka Texas alinivutia zaidi kwa ujumbe alioandika; ''niruhusu nikupende, hutojutia na wala sitakutenda''. Nikatafakari, nikaona nitakuwa muhongo kwa sababu mi natafuta tu mchepuko.

Wengine waliobakia, wengi wao wanataka matunzo, kuwatoa 'out' , kuwatumia tumia hela; katika kupiga mahesabu, nikaona hakuna unafuu; kwa mtu anayeishi kwenye nchi inayotumia 'dollar' ili umridhishe, itakubidi angalau kila wiki unamtumia dollar mia mbili; hiyo hela nitaipata wapi mimi?

Wengine wakaja 'inbox' wakitaka tufanye nao 'tour'; wakiamini labda mimi ni pedeshee, kumbe ni mwalimu wa shule ya msingi mwenye mikwara mingi katika hili bara waliloliita 'dark continent' miaka hiyo.

Baada ya kuona tabia za pisi kali za huko majuu, hazina tofauti na za huku, imebidi nirejeshe majembe kwa pisi kali za nyumbani ambazo ata kwa wiki unaweza kumpa 10,000/= na akashuru.

Wakuu nimeamua kurudi nyumbani,kwa ridhaa yangu mwenyewe bila kulazimishwa; pisi kali nipokeeni kwa mikono miwili.​
 
Kama utakosa pisi basi tafuta Mabwana wanaotindua kwa tindo
 
Back
Top Bottom