BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,849
Pinda: Serikali imepwaya
na Rahel Chizoza, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kuwa, serikali ya awamu ya nne inapaswa kufanya kazi kwa bidii hivi sasa ili kuwarudishia wananchi wake imani ambayo imeanza kupotea.
Akiongea na waandishi wa habari jana bungeni mjini hapa, Pinda alisema kashfa ya Richmond, iliyosababisha baadhi ya viongozi wa serikali kujiuzulu ambayo imeikumba serikali hivi karibuni, imepunguza imani ya wananchi kwa serikali yao.
Maneno ya ufisadi yametawala sana vinywa vya Watanzania hali inayoonyesha hawana imani na serikali yao, hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni kujipanga kuhakikisha kwamba imani inarudi, alisema.
Alisema hivi sasa serikali inajipanga kupita mikoani kwa ajili ya kuongea na wananchi na kujibu maswali yao kuhusu masuala hayo, ili wananchi wapate picha sahihi.
Alibainisha kuwa tangu aingie madarakani, ameweka mikakati ya kuhakikisha kuwa serikali inatimiza wajibu wake badala ya kusubiri iwajibishwe na Bunge, ingawa ataendelea kutekeleza mipango iliyokwishaanzishwa na Waziri Mkuu aliyepita.
Alisema kuhusu kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na kamati teule ya Bunge kuhusu Richmond, serikali ilikwishaunda timu ya wataalam kwa ajili ya kupitia mapendekezo hayo ambayo tayari ilikwishakamilisha kazi yake na kuikabidhi serikali.
Kama Spika ataona ni vema kunipa nafasi katika Bunge hili, nitatoa taarifa ya baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa kwa hatua za awali, na kama nitakosa nafasi, Bunge lijalo taarifa yote ya mapendekezo inaweza ikatolewa ikiwa imekamilika, alisema.
Alisema baadhi ya mapendekezo hayo ni kuhusu swala la mikataba na kufanya maboresho katika eneo hilo, usimamizi wa manunuzi ya umma, uwajibikaji kwa viongozi wa serikali, uadilifu na kupewa uwezo zaidi kwa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa kuiondoa chini ya Wizara ya Fedha.
Alibainisha kuwa taarifa hiyo ya timu ya wataalam imetoa mapendekezo mazuri kuhusu hatua za kuchukuliwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika.
Alisema mbali na hatua hizo zilizopendekezwa, pia ofisi hizo zinapaswa kupewa nguvu zaidi, ili ziweze kufanya kazi kikamilifu kwani hata kama watendaji waliopo wakiondolewa wakija wengine matatizo yanaweza kujirudia kama tatizo ni mfumo wa uendeshaji.
Kuhusu suala la EPA, Waziri Mkuu alisema kuwa tume iliyoundwa na rais inaendelea kufanya kazi yake, hivyo kutolewa kwa taarifa zozote kuhusu uchunguzi huo itakuwa ni kuingilia kazi ya tume, jambo ambalo si zuri.
Alibainisha kuwa, fedha zinazorejeshwa katika EPA zitatajwa baada ya kazi ya tume kukamilika kuwa zimetoka wapi na kina nani waliorudisha na lengo la kuwataka watu hao warudishe fedha ni kutaka kupata ushahidi na faida.