Pinda: Serikali imepwaya

Nimechoka na hawa wababaishaji maana kila kitu hawana jibu...leo kuna binamu yangu mmoja kanipigia simu anahangaikia pension ya baba yake mwaka wa nne huu huku kila kitu walichoambiwa walete wameleta lakini visingizio tuu kama vya pinda ndio vimejaa ile serikali,bila kuwaondoa CCM umaskini ni halali yetu!
CCM jamani ndo TATIZO NA CHANZO CHA UMASKINI WETU..Period.
 
hata kama ukweli anauona kwake ni ngumu mno kuchukua action kwa sababu nchi haipo mikononi mwao, nchi wamesha kabidhi kwa mafisadi kwa hiyo kuwanyanganya WAZIRI HUYO MKUU ANAKWAMBIA NCHI ITAYUMBA
 
Kama hao watu hawafai kwanini bado wako madarakani na nyinyi mnapigia kelele kwenye vibuyu tu ???
 
Wasiwasi wangu ni kama hayo yote mnayasema kwa uchungu au to make the people just read it.

I'm serious kwa sababu naona huwa ni kulaumu lakini sijaona mtu anakuja na ufumbuzi, ni kulaumu na kuagiza. It doenst come in my sense. What I'm expecting from you guyz is a solution. Dont bring the problem/blaim without a solution. La sivyo utapata ziro, yaani utatoka kapa kwani yote mnayosema yapo siku nyingi. Na hizi hadithi za kama angekuwepo Mwl ni ukasuku, wale vijana njooni na mawazo mapya, achana na ya Mwl ilikuwa enzi zake ,tumkumbuke sawa wakati tuna mawazo yetu. Nkrumah, Mwl., na wengine walikuwa na yao, nahisi kama wangekuwa vijana sasa wangekuwa na mawazo mengine mazuri zaidi, sio yale ya enzi zao, lakini naona vijana wanayo ya wazee hao(Mola aweweke mahali pema peopni), ngojeni niwaulizeni swali kama wasingekuwepo hao wazee tungebaki mbumbumbu hatuna la kusema?. Tuna tatizo la fikra ndio maana hatuna jipya. Tunasubiri mtu aseme ndio tuwe na la kuongea, ni udhaifu mkubwa, udhaifu wa kufikiri lakini pia uwezo hafifu wa kuona mbali.Tunadhani hapo tulipo ndipo tunabidi tukae,sogea angalau kidogo basi!
Anza ukurasa mpya ,acha ukasuku.

Sasa hivi siwezi angalau kumnukuu kijana maana kila kijana ananukuu, ni uzembe wa akili zetu tukubali lakini naomba tuache ukasuku.

Jaribu kidogo kubadirika, dont try hard but the best.

Next time I'll come with a solution,

Nawapongez jambo forum nina ushauri kidogo" toa mwongozo mpya" yameandikwa yale yale mengi lakini hakuna ufumbuzi unaotolewa bila jazba wala karaha. Kwa mfano mtu anapotoa ushauri wa wapinzani kuingoa CCM atoe maelezo basi kwamba hao watakapoingia ana uhakika kuwa hawatakuwa wezi kuliko hawa waliopo, au atwambie tu kwa ufupi kwamba tujaribu

1.Hatua ya kwanza katika kulitatua tatizo ni kulielewa na kuliainisha, kwa hiyo kujua kwamba Pinda ni sehemu ya tatizo na wala si sehemu ya ufumbuzi wa tatizo ni hatua ya kwanza katika ufumbuzi wa tatizo.

2. Siyo lazima tuwe na ufumbuzi ili kuonyesha matatizo, tuna haki na wajibu wa kuonyesha matatizo hata kama hatuna ufumbuzi.Moja kati ya madhumuni ya bodi hii ni kupata ufumbuzi wa matatizo kwa mijadala, kuonyesha matatizo ni sehemu ya mjadala huu.

3.Wewe mwenyewe unasema watu hawatoi ufumbuzi na wanalalamika, lakini umeishia kukimbia na kusema utatoa ufumbuzi next time, sasa wewe una tofauti gani na hao unaowasema? Kama ni muhimu sana utoe ufumbuzi kwa kila tatizo unaloliona ili uweze kusema kwa nini hukusubiri mpaka uje na ufumbuzi ndipo uongelee matatizo haya?
 
Mimi simlaumu Pinda hata kidogo. Namlaumu bosi wake aliyemteua. Ninachojiuliza hapa ni kwa nini Kikwete alimteua Pinda? Je alidhani jamaa ni competent kwa kazi hiyo au? Au JK mwenyewe yuko bomu kiasi kwamba hawezi hata kutambua nani anafaa kwa kazi ipi?

wee unataka uambiwe mara ngp juu ya intelligence ya jk?? ina maana wewe ulikuwa hujui kama ni yeye ni bomu kwa selection ya wasaidizi wake hadi baada ya kumteua pinda??

Basi hata wewe ni bomu! hata uelezwe vp huwezi elewa, kama ulishindwa elewa uwezo wa jk kuteua viongozi hadi alipomteua pinda! bora unyamaze tu!!
 
Chama cha mapinduzi kimeshindwa kuijipindua ingawa pinda anakipindisha
 
du

samahan. kama kiongoz wa likampuni akisema kampun haiendi sawa hii si sawa na kusema yeye kashindwa kaz?

say Pinda akisema "Serikali imepwaya" hii si sawa na kusema "kaz imenishinda"?
 
Back
Top Bottom