Pinda na Vita tata ya Mashangingi

Pinda acha usanii hata lile ulilolikataa si uliagiza litumiwe na idara nyinginezo? Sidhani hoja ya msingi hapa ni v8,gx,vx au kwa maneno mengineyo mashangingi swala la msingi ni matumizi sahihi ya fedha za mlipa kodi period!
 
hivi huyu jamaa anaongea tu bila kufikiria?
hata mwezi haujapita tumeona magari yakikabidhiwa kila wilaya, leo anatuambia kusitisha..mmh alikuwa wapi? sasa anasitisha nini wakati magari yalishanunuliwa tayari? anatuona watz bado ni vuvuzela? huyu kazi ya PM imemshinda kazi kulalamika tu bila ya kutoa AGIZO kama PM.
 
Pinda nae kazi kulalamika wakati ana mamlaka ya kuzuia hayo yasitokee!!! Hakuna kiongozi makini ndani ya ccm wameharibiwa na mfumo.
 
Kwanza, huu mwenendo wa viongozi wa serikali (hasa mawaziri akiwemo PM) kufanya kazi kupitia kwenye media ni ubabaishaji mtupu. Kazi halisi ya serikali inafanyika kupitia miongozo, kanuni na taratibu zilizowekwa pamoja na mfumo thabiti wa usimamizi (enforcement). Kama vina mapungufu, vinarekebishwa/imarishwa kupitia mfumo uliowekwa. Hii kutoa maagizo kwenye redio, TV na magazeti kuhusu mambo ama ya kisera, kimkakati au kiutendaji ni uswahili tu. Mara waziri kaagiza makandarasi wasiokamilisha kazi kwa viwango vinavyotakiwa kufutiwa leseni; wafanyakazi watoro kufukuzwa kazi, mabwana shamba waache kukaa maofisini, mashangingi kupunguzwa! Pure crap!

Kazi za makandarasi zinaongozwa na mikataba waliyosaini yenye maelekezo kamili ya nini kifanyike upande mmoja usipotimiza wajibu wake. Kila kazi ya Serikali ina malengo/mpango wake wa mwaka (au zaidi) ukijumuisha majukumu ya ofisini na ya field. Mahitaji ya rasilimali ikiwa ni pamoja na fedha, vifaa (ikiwa ni pamoja na magari) na huduma pia huainishwa katika mipango ya kazi serikalini. Na inabidi kutathminiwa mara kwa mara (periodically) ili kuhakikisha ufanisi wa shughuli za umma.

Hivyo uamuzi wa magari mangapi na ya aina gani yanunuliwe kwa kazi fulani si mambo ya kuamka na kupayuka tu hadharani. Au bwana/bibi shamba atumie muda gani kuwa ofisini na kuwa field inategemeana na masuala ya kazi yake (kuna wananchi wa kawaida hawaelewi kwamba hawa watu wana majukumu ya kiofisi pia). Hata madaktari kuna wakati inabidi wajifungie kuchambua mambo kabla hawajaja na jawabu la kutumia "field". Ni wao na wanaowasimamia ambao wanaelewa mpango kazi wao ndio wanaweza kupima kama wanatumiaje muda wao vizuri kutimiza majukumu yao. Kama kuna kasoro katika mpango mzima (kutokana na malalamiko ya wananchi) basi wafanye marekebisho badala ya kuwahi kwenye media kutoa kauli zisizo na msingi. Kwanza wananchi wengi wa kawaida hawaelewi mfumo wa kazi serikalini unaendeshwaje.

Kwa upande wa Waziri Mkuu anatakiwa atumie madaraka yake kuhakikisha mfumo mzima wa serikali unafanya kazi kwa ufanisi. Hii kutuletea hadithi vipande za mashangingi, suti, n.k. sijui inatusaidia nini ilhali mfumo wenyewe hauna tija. Waziri Mkuu kuwa na shangingi si tatizo hata kidogo. Labda, kama (obsessively) anataka tumuone yeye binafsi kama mtu asiye na makuu, tamaa na muadilifu, sawa. Lakini hiyo haijibu suala lililo mbele yetu la ufujaji serikalini. He has to take concerted action on wastage by helping put in place proper government strategies, rules and procedures. Sie tubakie kusikiliza/kuona matokeo tu.
 
amechelewa sana kwani tayari magari zaidi ya mia mbili yalinunuliwa mwaka jana 2009 na 2010 na yeye alikuwa waziri mkuu tayari. mbona hakuyazuia??
 
Maagizo yote aliyowahi kutoa huyu PINDA halijawahi kutekelezwa hata mojaTuyakumbuke1.Akiwa kigoma ziarani alisema ni marufuku madiwani kufanya ziara za mafunzo kwa fedha za halmshauri LAKINI hadi leo halijatekelezwa2.Akiwa Kagera/Mwanza ziarani alisema wanaoua alboni nao wauawe on the spot halijatekelezwa3.........................Haya maagizo ya watawala kwa watawaliwa yamnafuiata utaratibu huu au ni watawala wakubwa kwa watawala wadogo
 
Heri anayesema , siku moja ndoto yake itatimia. Kubadilisha mfumo ni kazi lakini huo ni mwanzo mzuri. Kenya mbona wameweza.

Hawa wanawapagaisha wananchi tu hawana lolote hata kidogo, Pinda alishasema na wakaendelea kununua je alifanya nini?.

Hatudanganyiki tena.
 
kuna vitu anatakiwa afanye kabla ya hayo yote. gari za halimashauri wamelazimishwa na serikali kununua wizara ya miundombinu pekee yake. ni marufuku kununua kwa dealers. kama kwa dealer hardtop ni m80 kule miundombinu ni 105m. 20m zinapelekwa wapi? sijui kama halimashauri wanalipa kodi au la, ila kama hawalipi then ingetakiwa iwe chini ya 50m. hardtop ni cc4090 kama sikosei. fuel consumption yake ni kati ya gal 1 kwa mile 20 hivi. ukiconvert kwenye kms utaweza pata lt 1 km 6.4. pia yaweza fika 7. wakati huohuo kuna magari kama toyota hilux na landrovers ambayo engine zake hazizid cc 3000 na consumption yake ni ndogo. kwa nini kama wameamua kuokoa hela za wachovu wa tz wasinunue magari madogo madogo na huko fields wanunue ma defenders. weaknesses ni nyingi na changamoto ni nyhngi pia. ukienda kwa madereva wao nao kichefuchefu jamani. gari mpya hardtop au lc standard utakuta inanunulhwa wheel rim sports na matairi makubwa. hapn tayari wanaharibu fuel consumption na kuongeza gharama zisizo za lazima. kingine ni service za magari hayo. kama gharama halisi ni sh 10 basi kuna chain itayoweka cha juu hapo juu na inaweza fika 100 .huo ni mfano. pm awaambie wanunue toyota hilux au defenders na si vimginevyo. na abane matumizi ya uendeshaji wa hayo magari.
 
kaka zipo, japo si vx. tena ni nyingi na zingine zishaanguka zikiwa mpya kama kule longido nk.
 
hana akili hakuna wilaya yenye v8,v8 zipo serikali kuu na wakuu wa mikoa karibu wote wanazo,makatibu makamishna mawaziri wanayo.
Mpwa yapo mbona? nilikua wilaya mpya ya Kilindi nikalikuta huko linatumiwa na mkurugenzi... yaani hata halina maana kwani sehemu yenyewe inahitaji bajaj au labda landrover sio dude ambalo hakuna hata anayelielewa!
 
Kwa wastani kila halmashauri Ina V8 tatu, zidisha mara halmashauri 133, zidisha mara Tsh 280.000.000. Tuchukulie maintanence kila quarter pamoja na kupeleka DSM kwa service ni Tsh 700,000 wastani, zidisha tena mara 3, zidisha mara halmashauri 133, zidisha mara quaerters 4 kwa mwaka.

Bado hapo hujapiga hesabu magari mengine ndani ya kila halmashauri

bado hapo hujaweka hesabu ya dereva kupiga nyoka, kuuza tairi na spear!

Vehicles are monsters in our councils!!!!
ur right bro.
 
hana akili hakuna wilaya yenye v8,v8 zipo serikali kuu na wakuu wa mikoa karibu wote wanazo,makatibu makamishna mawaziri wanayo.
Mpwa yapo mbona? nilikua wilaya mpya ya Kilindi nikalikuta huko linatumiwa na mkurugenzi... yaani hata halina maana kwani sehemu yenyewe inahitaji bajaj au labda landrover sio dude ambalo hakuna hata anayelielewa!
Hawana huruma, halafu huyu jamaa kawa mropokaji sana siku hizi...sijui kalishwa nini maskini
 
Chanzo: Taarifa ya habari Star tv saa mbili usiku. Badala yake wanunue Hardtop. Hivi tofauti ya bei ya VX na Hardtop ni sh ngapi? Kama zoezi hili kweli likitekelezwa atakuwa ameokoa sh ngapi?

Huyo kashari tu,ana ubavu wa kupiga marufuku?
 
Huyu mheshimiwa Pinda alikuwa wapi wakati wa Marehemu Nyerere the president ? Maana aliwambia watu wavae rubega na suti za bei mbaya ziwe mwiko ,sasa huyu mtu akiwa raisi kuna hatari ya watu kurudi miaka ile ya zamani usafiri kwa miguu au punda. Yaani ananiacha hoi kabisa :teeth:
 
Mnafiki tu. Kinachomsumbua ni kuzungukwa na wezi ambao wamemzidi nguvu na ujanja. Namshauri ajiuzulu kama hataki kushirikiana nao. Au anyamaze kimya siyo kuja na maagizo kila kukicha!
 
Jamani mimi sielewi kwani nani anapitisha yanunuliwe au la? Kama hutaki wanao wale mayai si una acha kununua? Sasa wewe unanunua, unaleta nyumbani halafu unapiga marufuku wasiyale. Those are fluffy talks any one could talk. If they dont want council to use V8 then they should not buy them!!! So Pinda should stop playing with our brains.
 
Jamani, tutambue kwamba siyo JK wala Pinda anayejua serikali hii inafanya nini. hawa ni watu ambao utendaji wao wa kazi siyo wa kushiriki kutenda bali kusimuliwa nini kimefanyika/kitafanyika. Hawasomi kabisa! Wewe muone JK anaposaini kitu kwenye TV anavyochukua muda kwanza kuona wapi asaini na anavyochukua muda kusaini. Huyu ndiye rais anayetakiwa asome mipango yote ya serikali, aifahamu na aelekeze.

Ndiyo maana aina yao ya utendaji ni kutembelea sehemu, kusikiliza hotuba, na kusoma hotuba waliyoandikiwa na wapambe wao. Hivyo wao ni robborts to siyo watendaji, kila kitu kinafanywa na wasaidizi wao ambao kwa bahati mbaya waliteuliwa kutokana na uswahiba na siyo uwezo wao wa kutenda, technically

Hivi hamjajiuliza ni kwa nini siku hizi ni kawaida serikali kuwasilisha bajeti bungeni halafu baadaye inagundulikwa kwamba imekosewa? Au waziri anawasilisha bajeti kwa wahisani ambayo ni tofauti na ile aliyowasilisha Bungeni halafu wapambe wake wanakuja kumdanganya atoa taarifa kwa media kwamba ile waliyopewa donors ilikuwa ni makadirio tu. Kwa mtu ambaye unayajua haya mambo na ambaye umeona version zote mbili na ulikuwa unafuatilia mchakato mzima, taarifa hiyo ilikuwa ni uongo lakini ili kuthibitishia umma kwamba ilikuwa ni uongo itakuwa kazi kubwa na unaweza kupoteza maisha.

so we need to discuss about a broad problem beyond and around Pinda and JK, serikali isiyojua kinachoendelea pande zote na ngazi zote. haya tunayoyaona ni ishara to za mulfunctional system. Ni jukumu la watz kujadili na kulishuhulikia hili.
 
hata mimi ninashangaa kwanini kwa halmashauri tu na ofisi zingine za serikali zainaendelea kununua magari ya kifahari.dah unapomnyooshea tu kidole nawe jiangalie uko vp
 
Tanzania Daima ya leo 22 December 2010



MAFISADI HAZINA WAMPIKU PINDA


Wakati serikali iktamba kwamba imejipanga kudhibiti matumizi, baadhi ya vigogo katika wizara na idara mbalimbali wamekuwa wakiuziwa mashangingi ya serikali kwa bei ya Sh 300,000 hadi Sh 2,000,000, Tanzania Daima Jumatano limegundua.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa siku kadhaa sasa umebaini magari yalyouzwa ni yale yaliyokuwa yakitumika kwa miradi ya DFP yaliyotolewa na Jumuia ya Umoja wa Nchi za Ulaya (EU). Habari za uhakika zinasema magari hayo yamenunuliwa na vigogo wa nje na ndani ya wizara hiyo.

Imeandikwa na Bakari Kimwanga (Unfortunately this story is not online although it is the cover story)
 
Mheshimiwa kwa kweli hapo kanena, yaani kwa kununua ma hardtop rand cruzer inaweza kusaidia kubana matumizi, hapo namuuunga mkono kabisa. unajua kama tatizo ni barabara landcruser zinachapa mwendo kupita maelezo. kwa mfano kutoka mpwapwa hadi Iringa kupitia mtera barabara ya vumbi linaweza kutumia masaa ma3 na nusu.


je?kwa huo muda viongozi wa serikali wanaotumia hayo ma landcruser watashindwakupita barabara za vumbi kama ilivyo barabara ya dodoma-iringa kupitia mtera?

ushauri mwingine ingetakiwa tukiacha mawazili na manaibu, viongozi wengine wote watumie ma hard top, hata wakurugenzi na viongozi wote vyuo vikuu watumie ma hardtop na pia wabunge wasikopeshwe magari ya gharama ili kuwepo na uniformity, hapo serikali itakuwa imebana matumizi ya magari.

Ikiwezekana wanunue land rover ONE TEN, zitachapa kazi vizuri tu.
 
Back
Top Bottom