Pinda na Vita tata ya Mashangingi

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Chanzo: Taarifa ya habari Star tv saa mbili usiku. Badala yake wanunue Hardtop. Hivi tofauti ya bei ya VX na Hardtop ni sh ngapi? Kama zoezi hili kweli likitekelezwa atakuwa ameokoa sh ngapi?
 

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
3,364
1,195
..Kwa vyovyote kuna kiasi kimeokolewa..
..Lakini tatizo la msingi
... Nani alipanga kununua hizo VX .. kwa nini yeye hakuona alichoona Pinda!!
Kwa nini watanzania wasiwe na moyo wa Pinda...?
 

superfisadi

JF-Expert Member
May 22, 2009
553
195
kwa kweli viongozi wetu majasiri wanatumia magari ya kifahari wkt ss tunaolipa kodi tunatumia tz 11 , kuna dc mstaafu huwa nikikutana naye huwa anaangalia chini manake kutoka kwenye vx sasa anamaliza soli
Viongozi wanaangalia leo kesho aiwahusu
 

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,232
1,500
Pinda hana lolote. Anatoa maagizo kupitia vyombo vya habari? kwani hana anuani za wakurugenzi wa wilaya? Kukataza ununuzi wa magari ya fahari ni kazi ndogo sana, serikali iandike waraka na bajeti za halmashauri isiwe na fungu la kununulia Vx. Kama uongozi umemshinda aachie ngazi tu. mara akate gari lililonunuliwa kwa ajili yake. Anatufanyia usanii tu.
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,528
2,000
hana akili hakuna wilaya yenye v8,v8 zipo serikali kuu na wakuu wa mikoa karibu wote wanazo,makatibu makamishna mawaziri wanayo.sasa huo si usanii kwa wadanganyika.kwa nini hajazuia huko anaenda kumwambia mtoto asile sumu huku wewe baba unakula?
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,164
2,000
He is Not Prime at all, Prime, Prime...........!!!!!!!!!!!!!!!! Def.= first in excellence, quality or value, first in degree or rank chief, if i was PM, natoa order
tu, then i look nani will misbehave, i don't trust Pinda kabisa jamani kiuongozi ila mwaminifu sana which is not enough
 

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,177
1,500
Bongolala, nadhani hujajua vizr mimi najua halmashauri zenye haya mav8, mfano hw mkinga, kilolo to mention 2!
 

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,578
0
Pinda naye anaropoka sana siku hizi! Hana washauri huyu?

Sasa hivi anajua kuwa ana miaka mitano kamili, refer hotuba yake siku ya kuthibitishwa. Nafikiri mwanzo alikuwa kama haamini vile kuwa yeye ni PM na kudhani Lowassa angerudishwa baada ya 2010 election. Ukweli unabakia kuwa yeye alikuwa wapi wakati ma VX yananunuliwa?, na kama anataka kuondokana na mashangingi basi wapeleke muswada bungeni upitishwe kuwa sheria. Ila akae akijua kuwa watu wanaweza hata kutumia bajaji cha msingi ni serikali kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami mpaka vijjijini. Hapo tutakuwa tumewekeza hasa kwa maendeleo ya mtanzania.
 

Sir Leem

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
576
225
Karibu halmashauri tayari wanatumia mashiungingi sasa anataka halmashauri ipi wasinunue
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,528
2,000
Tatizo watu wa procurement wanasema tender inatolewa na specifications za gari wakiangalia wanaona v8 ndiyo inaendana na specifications hivyo tayari mkanganyiko!
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,219
2,000
Rwanda pia wameweza cc tu kwani kuna wakuu wanalipa fidia walio walipia fedha za uchaguzi. bei ya hard top pick up $ 95000 pamoja nakodi hivyo station wagon itakuwa[ hard top ]$105000$ kulingana na toyota motors
 

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Bongolala, nadhani hujajua vizr mimi najua halmashauri zenye haya mav8, mfano hw mkinga, kilolo to mention 2!

Kwa wastani kila halmashauri Ina V8 tatu, zidisha mara halmashauri 133, zidisha mara Tsh 280.000.000. Tuchukulie maintanence kila quarter pamoja na kupeleka DSM kwa service ni Tsh 700,000 wastani, zidisha tena mara 3, zidisha mara halmashauri 133, zidisha mara quaerters 4 kwa mwaka.

Bado hapo hujapiga hesabu magari mengine ndani ya kila halmashauri

bado hapo hujaweka hesabu ya dereva kupiga nyoka, kuuza tairi na spear!

Vehicles are monsters in our councils!!!!
 

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Tatizo linalomfanya pinda atoe maagizo yasiyotekelezwa ni kwamba hapitii bajeti za kila wizara wala za halmashauri. Anategemea zaidi hotuba ambazo anaandaliwa na watendaji wake. Watendaji wake wanamuandikia jotuba tofauti na bajeti yenyewe. Changamoto ni kwa viongozi wetu kujisomea na kujiandikia hotuba wenyewe, kama alivyokuwa anafanya Nyerere.
 

jyfranca

JF-Expert Member
Oct 3, 2010
297
0
Which is better strategy, bottom up, or top down? Angeanzia na wizara na wawe mfano kwa Halmashauri, ila kama halmashauri zitatolewa kafara wakati matumizi wizarani ni yaleyale au yanaongezeka, basi ili zoezi halina maana. Mtoto wa mkulima aanze na kichwa amalizie mkia. Nyoka anaktwa mkia kwanza au kichwa?
 

mob

JF-Expert Member
Dec 4, 2009
2,270
2,000
hizi kauli za mheshimiwa pinda angalau zina matumaini katika kubana matumizi ya serikali kama sikosei juzi au jana katika gazeti la tanzania daima alikuwa ameagiza gari lake liuzwe.


waheshimiwa mjenge angalau hata mazoea ya kusoma angalau machapisho ya serikali na hata ngos. nimebahatika kugoogle ishu relating to alllowances ,nikakutana na machapisho ya shirika moja la Sikika nadhani liko dar wameandika vizuri sana hizi fedha zinavyolika na jinsi wachache wanavyofaidi .jaribu kuggoglle web site yao utaona hayo yote.
 

tbetram

Member
Nov 1, 2010
31
0
Mimi nashauri sera ya ununuzi magari ya serikali iangaliwe upya. Napendekeza kusiwe na magari ya serikali. Kila kiongozi anunue gari lake kwa fedha zake mwenyewe. Pia anunue fuel - petrol/disel na amlipe dereva kwa gharama zake.
Hakuna maana kodi za wananchi zitumike kuwanunulia viongozi magari ya kifahali, kununua fuel, kuwalipa madereva mishahara.
Kama ambavyo sisi wananchi tunavyojigharimia usafiri wa kwenda kwenye shughuli za ujenzi wa taifa, vivyo hivyo na viongozi wajigharimie. Hiyo ni ajira yao na wanalipwa mishahara mikubwa kwa kazi zao. Fedha zitakazo okolewa ziboreshe huduma za kijamii kama elimu, matibatu, miundombinu etc

Hebu watanzania tufanye utafiti, katika nchi hii ni watu wangapi wanatumia magari ya serikali, wanalipiwa gharama za mafuta, kulipa dereva na matengenezo ya magari, kulipia wafanyakazi wao wa nyumbani, kulipia gharama za matibabu etc. Ni fedha kiasi gani zinapotea? Viongozi ni watanzania wenzetu. Wanafanya kazi serikalini na wanalipwa mishahara, hawajitolei. Hivyo wanapaswa kujigharimia wenyewe kama ambavyo watanzania wengine wanavyofanya.

Hayo ni mawazo yangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom