Mimi nashauri sera ya ununuzi magari ya serikali iangaliwe upya. Napendekeza kusiwe na magari ya serikali. Kila kiongozi anunue gari lake kwa fedha zake mwenyewe. Pia anunue fuel - petrol/disel na amlipe dereva kwa gharama zake.
Hakuna maana kodi za wananchi zitumike kuwanunulia viongozi magari ya kifahali, kununua fuel, kuwalipa madereva mishahara.
Kama ambavyo sisi wananchi tunavyojigharimia usafiri wa kwenda kwenye shughuli za ujenzi wa taifa, vivyo hivyo na viongozi wajigharimie. Hiyo ni ajira yao na wanalipwa mishahara mikubwa kwa kazi zao. Fedha zitakazo okolewa ziboreshe huduma za kijamii kama elimu, matibatu, miundombinu etc
Hebu watanzania tufanye utafiti, katika nchi hii ni watu wangapi wanatumia magari ya serikali, wanalipiwa gharama za mafuta, kulipa dereva na matengenezo ya magari, kulipia wafanyakazi wao wa nyumbani, kulipia gharama za matibabu etc. Ni fedha kiasi gani zinapotea? Viongozi ni watanzania wenzetu. Wanafanya kazi serikalini na wanalipwa mishahara, hawajitolei. Hivyo wanapaswa kujigharimia wenyewe kama ambavyo watanzania wengine wanavyofanya.
Hayo ni mawazo yangu.