Si mnafahamu maafande wakati wa kukupa mazoezi ya kijeshi ,utaona una afande shujaa ile mbaya kiasi ya kuamini kwamba ikitokea vita atakuwa mstari wa mbele na huyu Pinda inaonyesha anafuata nyayo za Kikwete maneno mengi vitendo kwa wanyonge tu.
Na pia bado Pinda ni mgeni kwa kiasi fulani hivyo bado anatafuta njia au hajaziona na kuzijua njia za kupita ili amege na kuchukua chake mapema ila muda ndio utakaotuwacha hoi.
Du hiyo kali, lakini sheria ya vyuo vikuu si inazuia masuala ya siasa vyuoni au wameshabadilisha? Maana isije ikawa anapinga ufisadi lakini analeta ufisadi mwingine wa kiCCM katika vyuo
Kuna ukweli ndani yake ktk maneno ya Pinda bado anawalia timing,nadhani angoja amri toka kwa bwana mkubwa, tusubiri.
Manenge labda tu utusaidie hapa kwamba tumpe muda gani kwa mujibu wako wewe unaye amini kwamba Pinda anaweza .Kabla hujasema kwamba ana uchungu na Nchi tupe rekodi yake ya kuonyesha uchungu .Amekuwa serikalini muda wote na hata waziri kule kwingine je alifanya nini labda tuanze kumpima kwa hilo ili tumoe imani .Tumpe muda gani?