PINDA: KAMA WEWE NI FISADI ni FISADI TU

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Haya jamani PM MP aendeleza kumkoma nyani giladi. Au ni maneno tu...

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema wakati umefika kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutooneana aibu katika kukisafisha chama hicho ili kifanye kazi iliyokusudiwa na wanachama wake. Kauli hiyo aliitoa jana katika mkutano wa hadhara baada ya ufunguzi wa tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini lililopo Kihesa nje kidogo ya mji wa Iringa.Pamoja na kuagiza wana-CCM kutooneana haya, alisema kumuita mtu fisadi kama kweli ni fisadi si mbaya, kwani ni njia ya kuondoa uozo uliopo kupisha sera za chama kufanya kazi zake. "Kama ni kweli umeiba fedha za umma, wewe ni fisadi tu hakuna haja ya kubadilisha jina..." alisema Waziri Mkuu huyo huku akiimbiwa wimbo wa “Sema Pinda usiogope, sisi vijana hatuogopi vibaraka
 
Actions speak louder than words, quit talking, do something.
 
Si mnafahamu maafande wakati wa kukupa mazoezi ya kijeshi ,utaona una afande shujaa ile mbaya kiasi ya kuamini kwamba ikitokea vita atakuwa mstari wa mbele na huyu Pinda inaonyesha anafuata nyayo za Kikwete maneno mengi vitendo kwa wanyonge tu.
Na pia bado Pinda ni mgeni kwa kiasi fulani hivyo bado anatafuta njia au hajaziona na kuzijua njia za kupita ili amege na kuchukua chake mapema ila muda ndio utakaotuwacha hoi.
 
tena tunataka aanze na very simple actions............ from mapendekezo ya RICHMOND Report iliyowasilishwa bungeni.....hatutaki mineno mingi
 
mimi Sijui Kama Ni Danganya Toto Lakini Ngoja Tusubiri Maana Naona Mda Unazidi Kwenda Na Wameisha Tafuniwa Na Mwakembye Lkn Kumeza Hawataki ............labda Tuone Yangu Macho
 
Si mnafahamu maafande wakati wa kukupa mazoezi ya kijeshi ,utaona una afande shujaa ile mbaya kiasi ya kuamini kwamba ikitokea vita atakuwa mstari wa mbele na huyu Pinda inaonyesha anafuata nyayo za Kikwete maneno mengi vitendo kwa wanyonge tu.
Na pia bado Pinda ni mgeni kwa kiasi fulani hivyo bado anatafuta njia au hajaziona na kuzijua njia za kupita ili amege na kuchukua chake mapema ila muda ndio utakaotuwacha hoi.

Pinda ni mgeni kwa lipi ? Kaingia serikalini kuanzia mwaka gani ? Mmeanza tena kama mlivyo kuwa mnatoa sifa kwa JK kwamba ni mgeni .hadi sasa mwaka wa 3 bado anatfuta njia pia kwamba how the Prez should react in case of uozo mbele yake ? Pinda si mgeni bali anaiga usanii .Hawana la kueleza wananchi maana yeye na JK they cannot act .Nashangaa hata hao wasomi wameshindwa kumuuliza maswali .Anajibu Risala ambayo alishapewa siku nyingi akawa anajua cha kusema ?
 
Du hiyo kali, lakini sheria ya vyuo vikuu si inazuia masuala ya siasa vyuoni au wameshabadilisha? Maana isije ikawa anapinga ufisadi lakini analeta ufisadi mwingine wa kiCCM katika vyuo
 
Du hiyo kali, lakini sheria ya vyuo vikuu si inazuia masuala ya siasa vyuoni au wameshabadilisha? Maana isije ikawa anapinga ufisadi lakini analeta ufisadi mwingine wa kiCCM katika vyuo

CCM watapinga tu kama Chadema ama CUF watafanya openly kama wao .Washiriki wote watamulikwa na kufukuzwa Chuo kwa madai ya vyeti na kuleta vurugu.Kwa sasa wao ni sawa tu kufanya mikutano .Wacha Vyama vingine vije viingie uone .
 
Katika viongozi tulionao wapo mafisadi lakini vile vile naamini kwa dhati kwamba wapo viongozi wasafi.Wapo ambao wanaona jinsi hali inavyokwenda wanakereka lakini hawakuwa na nafasi ya kusemea.Mmoja wao ni mh Pinda, tumpe muda, kwa sababu kuna asignment ameshapewa tutampima nayo.Lakini vilevile nampa ushauri wa bure kabisa kwamba UMMA WOTE ukiondoa mafisadi ambayo hayafikii hata 5% ya watanzania upo na yeye. Hivyo asiwe na wasiwasi.This is a high time for hon Pinda to give a dog (mafisadi) bad name and shoot them. Mungu mlinde na mpe ujasiri
 
Manenge labda tu utusaidie hapa kwamba tumpe muda gani kwa mujibu wako wewe unaye amini kwamba Pinda anaweza .Kabla hujasema kwamba ana uchungu na Nchi tupe rekodi yake ya kuonyesha uchungu .Amekuwa serikalini muda wote na hata waziri kule kwingine je alifanya nini labda tuanze kumpima kwa hilo ili tumoe imani .Tumpe muda gani?
 
Kuna ukweli ndani yake ktk maneno ya Pinda bado anawalia timing,nadhani angoja amri toka kwa bwana mkubwa, tusubiri.
 
Jamaa PM MP jana/juzi kapiga bao la nguvu,kapiga porojo pale kihesa na kuwalamba wanachama wapya 700, mimi nadhani muda ni jawabu la mambo mengi,hata mafisadi hawakujua kuwa siku moja wataambiwa kuiba sasa basi na mlichoiba kirudisheni,japokuwa suala la kurudisha nyumba ni dhaifu kidogo,lakini tayari matumbo yanawaka moto. ALICHOSEMA NI KWELI KUWA FISADI ASIBATIZWE JINA LINGINE, vitendo kwa serikali yetu ni lugha ya Kigiriki.
 
Kuna ukweli ndani yake ktk maneno ya Pinda bado anawalia timing,nadhani angoja amri toka kwa bwana mkubwa, tusubiri.

madaraka aliyonayo tosha kabisa, na kama atakalofanya atakuwa anaamini analitendea haki taifa na anatimiza wajibu unaompasa hilo la kusubiri amri linatoka wapi tena?
 
Manenge labda tu utusaidie hapa kwamba tumpe muda gani kwa mujibu wako wewe unaye amini kwamba Pinda anaweza .Kabla hujasema kwamba ana uchungu na Nchi tupe rekodi yake ya kuonyesha uchungu .Amekuwa serikalini muda wote na hata waziri kule kwingine je alifanya nini labda tuanze kumpima kwa hilo ili tumoe imani .Tumpe muda gani?

wana miaka zaidi ya 40 madarakani ila uharo ni ule ule, so haka sasa kanakuwa kama kamchezo, jitu likiharibu linajiuzuru kisha anakuja mwingine je hii mpaka lini?
hawakuwa wajinga waliosema "samaki mmoja akioza basi woooote wamechina".
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom