Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,184
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewashangaa viongozi waandamizi wastaafu serikalini na CCM kuacha kuzungumzia malalamiko yao katika vikao halali kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari. Vyama vina mifumo yao ya kuendesha shughuli zao vina maeneo ya kusemea mambo yao na huko ndiko kusaidia chama na kuweka mikakati ya kukiendeleza, alisema Waziri Mkuu alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana.
Alikuwa akijibu swali kuhusu viongozi wa CCM wakiwamo wastaafu, kulumbana na umoja wa vijana wa chama hicho hadharani badala ya kutumia vikao halali vilivyopo. Alisema kutoa madukuduku kwa kutumia magazeti kabla hata ya kukataliwa katika vikao halali vilivyopo, si dhamira nzuri. Kama malalamiko yako uliyatolea katika vikao halali na ukakataliwa kusikilizwa na hivyo ukaamua kutoka na kuyasema nje, hilo halina tatizo. Na hasa viongozi wastaafu. Hawa wana fursa ya ziada, wana uhuru hata wa kumwona Rais na kusema naye, wakitumia uzoefu walionao kumsaidia hata yeye, alisema Pinda.
Aliasa kuwa si picha nzuri kuona kana kwamba viongozi hao wanakataliwa kusikilizwa katika vikao na hivyo kuamua kuyasema hadharani. Msiwe waoga kusema ndani ya vikao halali kwani huko ndiko hasa pa kujenga na si kusemea kwingine huko ndiko kukisaidia chama na kupanga mikakati zaidi ya kukiimarisha, alishauri Pinda.
HabariLeo
Sangara Mambo!! Naona hiyo Avatar yako na kopa iliomo imeitoboa Libya Kabisa!!!hapa tunajadili watu au issues? hata kama mtu humpendi jaribu kusikiliza hoja yake.
hapa tunajadili watu au issues? hata kama mtu humpendi jaribu kusikiliza hoja yake.
hana hoja na hajaanza leo kushangaa na kulialiahapa tunajadili watu au issues? hata kama mtu humpendi jaribu kusikiliza hoja yake.
alishika kichwa tu mzee:ballchain:hakulia?
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewashangaa viongozi waandamizi wastaafu serikalini na CCM kuacha kuzungumzia malalamiko yao katika vikao halali kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari. "Vyama vina mifumo yao ya kuendesha shughuli zao … vina maeneo ya kusemea mambo yao na huko ndiko kusaidia chama na kuweka mikakati ya kukiendeleza," alisema Waziri Mkuu alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana.
Alikuwa akijibu swali kuhusu viongozi wa CCM wakiwamo wastaafu, kulumbana na umoja wa vijana wa chama hicho hadharani badala ya kutumia vikao halali vilivyopo. Alisema kutoa madukuduku kwa kutumia magazeti kabla hata ya kukataliwa katika vikao halali vilivyopo, si dhamira nzuri. "Kama malalamiko yako uliyatolea katika vikao halali na ukakataliwa kusikilizwa na hivyo ukaamua kutoka na kuyasema nje, hilo halina tatizo. "Na hasa viongozi wastaafu. Hawa wana fursa ya ziada, wana uhuru hata wa kumwona Rais na kusema naye, wakitumia uzoefu walionao kumsaidia hata yeye," alisema Pinda.
Aliasa kuwa si picha nzuri kuona kana kwamba viongozi hao wanakataliwa kusikilizwa katika vikao na hivyo kuamua kuyasema hadharani. "Msiwe waoga kusema ndani ya vikao halali kwani huko ndiko hasa pa kujenga na si kusemea kwingine … huko ndiko kukisaidia chama na kupanga mikakati zaidi ya kukiimarisha," alishauri Pinda.
HabariLeo
hapa tunajadili watu au issues? hata kama mtu humpendi jaribu kusikiliza hoja yake.
Angekuwa anacharuka namna hii anapoongea dhidi ya ufisadi uliokithiri nchini, basi ufisadi ungeshakuwa history katika nchi yetu.
THE Prime Minister, Mr Mizengo Pinda, stresses a point during a meeting with editors in Dar es Salaam on Monday. (Photo by Fadhili Akida)
Huyu bwana ni mnafiki ajabu!!!,ukiangalia kauli yake na matendo yake ni mwongo wa kufa mtu,hata maoni aliyoyatoa jana kwa kuwasema wastaafu naamini hakutakiwa kuyatoa zaidi ya kujibu kuwa yatazungumzwa kwenye vikao,au yeye ni tofauti!?,mfano angalia suala la magufuli kwa jinsi alivyoropoka jukwaani ni maajabu!kwani kikao cha baraza la mawaziri hakikuwepo?au yeye mwenyewe kwa nafasi yake anauwezo wa kumwita waziri yeyote na kumshauri,mbona hakufanya hivyo?hata kama alifanya hivyo hakusikilizwa na yeye kuamua kulipuka basi hana hekima,kuna njia nyingi tu za kistaarabu za kumshauri mtu,ukifatilia kwa makini pinda amechangia kwa kiasi kikubwa serikali kukosa mwelekeo kwani yeye ndiyo mtendaji wa serikali,siyo kwamba namtetea lowasa ila baada ya yeye (lowasa) kuondoka mambo yameenda hovyo zaidi,kazi yake kutaka kufurahisha kila upande,amekuwa mtu wa kulalamika na kuishi kwa kudhani!Unajua Pinda anapenda kuonekana Goodboy...mnafiki tu.Pinda ni mfano mbaya wa viongozi wa kizazai kilichopo madarakani,yeye ni muumini mkubwa wa siasa za kizandiki za CCM.Kazi anayo