Pinda abadili upepo wa CCM urais 2015

Pinda abadili upepo wa CCM urais 2015


jk.gif

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipiga kura wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho huku akiwa jirani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Picha ya Maktaba
​


Na Neville Meena

Jumapili, Agosti 24 2014 saa 10:17 Asubuhi

KWA UFUPI
Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho alisema wingi wa wanaojitokeza kutaka kuwania urais ni njia ya kuunda mtandao utakaomwezesha mtu fulani au mmoja kunyakua tiketi hiyo.

Dodoma
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameingia rasmi katika mbio za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatua ambayo imebadili mwelekeo wa kinyang’anyiro cha nafasi hiyo kubwa ya uongozi nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.


Gazeti hili limethibitisha kwamba Pinda tayari ameamua kujitosa kuwania nafasi hiyo kupitia CCM ambayo tayari inawaniwa na makada wa chama hicho wasiopungua 15 na baadhi yao wameishatangaza nia zao kwa nyakati tofauti.

Habari kutoka ndani ya CCM zinasema uamuzi wa Pinda kuwania urais mwaka mmoja tu kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwakani, umesababisha kiwewe miongoni mwa wagombea na kunakifanya kinyang’anyiro hicho kuchukua sura mpya.

Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM aliliambia gazeti hili siku chache zilizopita mjini Dodoma kuwa: “Na sisi tumesikia kwamba PM (Waziri Mkuu) amejitosa na kama ni kweli atawasumbua wagombea wengi kutokana na rekodi yake hasa katika uadilifu.”

“Yeye (Pinda) ana faida tatu kubwa; kwanza hana kundi katika chama, anaelewana na watu wote, pili nafasi yake ya uwaziri mkuu inampa nafasi ya kufahamika kwa watu wengi na tatu rekodi yake ya uadilifu, hana kashfa za ovyoovyo, labda kama ataharibu dakika hizi za mwisho,” alisema kiongozi huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Wengine ambao wamekuwa wakitajwa kuwania uraia kupitia CCM ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na mtangulizi wake katika nafasi hiyo, Frederick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Wegine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta. Wengine wanaotajwa ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Katiba, Asha-Rose Migiro.

Pia wamo Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Balozi Ali Karume.


Wasomi

Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho alisema wingi wa wanaojitokeza kutaka kuwania urais ni njia ya kuunda mtandao utakaomwezesha mtu fulani au mmoja kunyakua tiketi hiyo.

“Watu wanapiga kampeni katika harambee kwa njia ya kutengeneza mitandao, kwani ukifika wakati wa chama kumpitisha mgombea, asiposhinda ataibuka na kuwaeleza kuwa mnaoniunga mkono mimi muungeni fulani,” alisema.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema kujitokeza kwa idadi kubwa ya wanaowania nafasi ya urais, kutatoa fursa ya wananchi kutambua udhaifu wa kila mmoja jambo litakalowezesha kupatikana kwa mtu sahihi wa kupeperusha bendera ya chama hicho.

“Wakiwa wengi, kila mmoja atataka kuonyesha umahiri wake na sisi ambao ni wananchi watawaliwa tutaweza kutambua upungufu wa kila mmoja, jambo litakalosaidia kupatikana kwa mtu sahihi,” alisema Mbunda


Kambi ya Pinda
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa siku kadhaa mjini Dodoma ambako vikao vya Bunge Maalumu vinaendelea umebaini kuwa kambi ya Pinda inaongozwa na Mwenyekiti wa Mamlaka za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi.

Inadhaniwa kuwa Dk Masaburi atatumia ushawishi wake kwa viongozi wa mamlaka za miji na wilaya zinazoongozwa na wenyeviti wa halmashauri na mameya wa miji, manispaa na majiji kumuunga mkono mgombea huyo ambaye pia hivi sasa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ziko chini ya ofisi yake.

Wiki hii kundi la wafuasi wa Pinda likiongozwa na Dk Masaburi lilikuwa mjini Dodoma likijaribu kutafuta kuungwa mkono na makada viongozi wa CCM ambao walikuwa wakishiriki kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho pamoja na wale walioko katika Bunge Maalumu. Habari zinasema mbali na Dodoma, tayari kambi hiyo imeshafanya vikao kadhaa jijini Dar es Salaam na Visiwani Zanzibar lengo likiwa ni kutafuta kuungwa mkono na makada wa CCM katika sehemu hizo. Hivi sasa nguvu za Pinda zinaelekezwa katika mikoa mingine nchini kwa lengo hilohilo. Kutokana na kasi ya kambi yake, wafuasi wa baadhi ya wagombea wameanza kufuatilia mwenendo wao kwa lengo la kukusanya ushahidi wa kile wanachokiita ‘rafu’ zinazochezwa ili kupata ushahidi unaoweza kutumika dhidi ya mgombea huyo wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM utakapoanza mapema mwakani.

Itakumbukwa kwamba makada watano wa chama hicho ambao ni Lowassa, Membe, Makamba, Wassira na Ngeleja wanatumikia adhabu na wapo chini ya uangalizi wa chama hicho baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kuanza kampeni za urais kabla ya muda kutangazwa.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema hivi sasa ni mapema mno kusema ni lini mchakato wa kupata wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama hicho utaanza na kwamba wakati mwafaka ukiwadia wananchi watafahamishwa.


Uwezo, udhaifu wake
Hata hivyo wakosoaji wake wanasema Pinda akiwa Waziri Mkuu hana cha kujivunia na kwamba amekuwa mzito kufanya uamuzi mara kadhaa kiasi cha kusababisha baadhi ya mambo muhimu ya nchi kukwama na kwamba kwa maana hiyo hastahili kuwa rais.

“Ni kitu gani ambacho nchi inakikumbuka kuhusu huyu bwana ambacho alikifanya katika miaka yake ya uwaziri mkuu, kama alikuwa kwenye nafasi kubwa kiasi hicho na hakuna alichofanya, atawezaje kumudu madaraka ya mkuu wa nchi?” alihoji mmoja wa makada wakongwe wa CCM.

Waziri mmoja wa sasa (jina tumelihifadhi), alisema Pinda hana uwezo wa kuongoza nchi, kwani wao wakiwa mawaziri ameshindwa kuwasaidia katika kero mbalimbali walizokuwa wakimfikishia kama kiongozi wao.

“Muulize waziri yeyote kuhusu uwezo wa jamaa, kila kukicha tunampelekea mambo tunayokutana nayo, lakini hakuna kinachowezekana kwake, atakwambia subiri leo, subiri kesho na hatimaye jambo linaishia hivyohivyo,” alisema.

Kwa upande mwingine, watetezi wake wanasema Pinda wanayemnadi ni yule aliyepata kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Tamisemi) kiasi cha kuonekana anafaa kuwa Waziri Mkuu.

Wanasema kushindwa kwake kufanya kazi ipasavyo ni matokeo ya sababu zilizomfanya mtangulizi wake, Lowassa kung’oka katika nafasi yake.


CHANZO: Mwananchi

mtapigwa mpaka mkubali tu.
 
Huu usanii tupu wa magamba kuchanganya watanzania wasahau mchakato wa katiba. Hatudanganyikiiiiii
 
Ingekuwa nchi za watu kitendo cha pinda kutangaza tu kuwania urais angelikuwa keshapigwa lisasi kadhaa kichwani tena hadharani. Jamaa ni lihaini na liuaji na lisilojali sheria za nchi na utu. Aliishaamuru raia kupigwa na kuuawa na imekuwa hivo. Jamaa linalialia hovyo tu.
Ila kwa kuwa tz ni kichwa cha mwendawazimu na urais ni majaribio basi si ajabu tukapata Mr.dhaifu mwingine zaidi ya kikwete
 
Jk alifanya uraisi kuwa rahisi mnoo.

Labda atakuwa amefyatuka tu. Baada ya vituko vingi pengine anataka kujua watz wamemuweka kwenye kundi gani. Naona anajua wamemuweka kwenye kundi la experienced comedians
 
Katika hao wooote waliojitangaza bora pinda,japokuwa nae ni conservative kweli.
 
Yaani huyu naye ameitwa muadilifu na ile skendo ya ardhi Sumbawanga ili ishajem Na uzembe alionao? Kweli urais umekuwa kama kuingis chooni hakuns usafi tena.
 
Nimeshangaa kuisikia hii kitu BBC na ktk magazeti mh Pinda nae kutangaza nia ya kugombea urais. Jamaa hafai kuwa rais wetu, hana maamuzi kama raisi. Apumzike tu na akistaafu itapendeza sana akifuga nyuki wa asali!
Kwa style hii viongoz wote wa CCM watatangaza nia sasa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nimeshangaa kuisikia hii kitu BBC na ktk magazeti mh Pinda nae kutangaza nia ya kugombea urais. Jamaa hafai kuwa rais wetu, hana maamuzi kama raisi. Apumzike tu na akistaafu itapendeza sana akifuga nyuki wa asali!
Kwa style hii viongoz wote wa CCM watatangaza nia sasa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

kama alikuwa PM akalia, akiwa raisi c atavua nguo?
 
mtoto wa mkulima kanogewa na madaraka,nadhan mizinga inamuitaj ,kuliko watanzania aloalalishwa tupigwe tu.
 
Nimeshangaa kuisikia hii kitu BBC na ktk magazeti mh Pinda nae kutangaza nia ya kugombea urais. Jamaa hafai kuwa rais wetu, hana maamuzi kama raisi. Apumzike tu na akistaafu itapendeza sana akifuga nyuki wa asali!
Kwa style hii viongoz wote wa CCM watatangaza nia sasa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums


Hebu rudia tena bbc wamesemaje!? Hii nchi imekuwa kichwa cha mwendawazimu kabisa.

Hivi BBC wamekosa kabisa habari za kutangaza mpaka wanafikia kutukejeli kiasi hicho?!

Ningepata tetesi mapema ningewahi mahakamani kuweka zuio hii habari isisomwe
 
Yaani hata huyu mzee nae anataka awe president wa nchi hii!!
 
Nimeshangaa kuisikia hii kitu BBC na ktk magazeti mh Pinda nae kutangaza nia ya kugombea urais. Jamaa hafai kuwa rais wetu, hana maamuzi kama raisi. Apumzike tu na akistaafu itapendeza sana akifuga nyuki wa asali!
Kwa style hii viongoz wote wa CCM watatangaza nia sasa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Huyu mwaka huu kasheherekea miaka 69 ..MWAKANI atakuwa 70 ...hakuna muda wa kuchagua Rais atakayeondoka madarakani na mkongojo wa miaka 80 .....Kama Nyerere kuondoka madarakani akiwa na miaka 62.... Mwinyi na miaka 72 kamaliza...Mkapa akiondoka na miaka 67 ...Kikwete anaondoka na miaka 63...
Rais atakayeingia maximum umri wa KUMALIZA umkute akiwa na miaka 65 hadi 75 mwisho .( yaani MWAKANI awe na miaka 55 hadi 65 mwisho )
 
Hebu rudia tena bbc wamesemaje!? Hii nchi imekuwa kichwa cha mwendawazimu kabisa.

Hivi BBC wamekosa kabisa habari za kutangaza mpaka wanafikia kutukejeli kiasi hicho?!

Ningepata tetesi mapema ningewahi mahakamani kuweka zuio hii habari isisomwe
Hawa jamaa wanatuona wa Tz vilaza! Labda team yake ije imtetee.
Huu uroho wa madaraka utatufikisha pabaya! China hakuna makitu kama haya. Mtu amealikwa mkutano wa dini au harambee then unalopoka nataka uraisi. Sijawahi kuikubali kazi ya Pinda!


Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
magufuli hawawezi kumpa nafasi anaweza kuwageuka!

kama huna 200 piga mbizi
 
Jamani! Anataka kuwa rais wa nchi gani kati ya tulizo nazo? Tanganyika au Tanzania? Kutangaza nia siyo vibaya ila kwake ni makosa na kututangazia sisi wapiga kura katukosea sana na inambidi kutuomba msamaha nasi kumsamehe ni kumtaka ajiuzulu nafasi aliyo nayo kwa sasa kwani hajaitendea haki hata kidogo. Kitendo chake cha kututangazia kuwa anaungwa mkono na rais mstaafu pamoja na kiongozi wa juu sana wa kiroho kama tulivyosoma kwenye magazeti ni kutuonyesha alivyo kinara wa udini hapa! Aliyemwambia watu hao wana ushawishi kwa wapiga kura kamdanganya mno. Na kukaa kwake ikulu kwa miaka 40 siyo kigezo cha kukubalika kwake kwani wapo waliokaa hapo zaidi yake na hawana hata sifa ya kuwa m/kiti wa mtaa. Sijamwona kama anafaa kwa nafasi yoyote kwani hata aliyo nayo hatoshi.
 
Back
Top Bottom