wakuu salaam sana.
_sikatai huyu baba yetu kuwania urais ila nachojiuliza na kama unaweza na wewe unijibu,amekuwa PM kwa miaka kumi amefanya mambo yepi kwa taifa hadi aitamani hiyo nafasi ya urais?
_Nilimtoa katika orodha ya viongozi siku ile alipolia bungeni kuhusu alibino na hadi leo hii alibino wanauawa na yeye bado ni pm huku vyote vya ulinzi na usalama vikiwa chini yake.
_zaidi siku ile aliposhidwa kumfuta kazi jairo.
_sasa huyu akiwa rais hii nchi itakuweje na hapo sijagusia upande wa maendeleo kama huko kwao sijui katavi watoto wanakaa chini darasani na raia wanakunywa maji kwenye madibwi na wanyama?
_naomba mnisaidie wakuu