Pinda abadili upepo wa CCM urais 2015

Pinda abadili upepo wa CCM urais 2015

Pinda hana sifa ya kuwq kiongozi kwani hawezi kufanya maamuzi kwa ajili yaa masilai ya taifa
 
Duh!!! Eh!! Kwa kweli hata nami naona hafai kuwa Rais japokuwa ni muadilifu,hiki cheo ni kikubwa sana kwake.
 
To be honest Pinda hana uwezo wa kongoza nchi, hawezi.
 
Bora na yeye aweke jina. Kwani wote waliotangaza nia wana nini cha ajabu? Afterall Tanzania inaweza kujiendesha yenyewe. He will not be the first.
 
Hili la Panda kuonekana dhaifu linalalamikiwa sana ,pengine kweli pinda hawezi lkn hata Mheshimiwa aliyepo madarakani binafsi Sijaona maamuzi magumu aliyofanya......tukiacha Hayo kuna hili la kuwa pinda anashindwa kufanya maamuzi mengine kutokana na kutokuwa na sapoti kutoka juu......tujikumbushe ishu ya jairo na tetesi kadhaa kuwa pinda alikuwa anataka kujiuzulu.......binafsi ndani ya CCM ya leo sioni yeyote mwenye uwezo wa kuivusha hii Nchi hapa ilipokwama,ccm kazi yao imebaki kulinda kwa maovu yao.
 
Du! Pinda akiwa Rais nchi itakuwa inaendelea kwenda kinyumenyume!
 
Hili la Panda kuonekana dhaifu linalalamikiwa sana ,pengine kweli pinda hawezi lkn hata Mheshimiwa aliyepo madarakani binafsi Sijaona maamuzi magumu aliyofanya......tukiacha Hayo kuna hili la kuwa pinda anashindwa kufanya maamuzi mengine kutokana na kutokuwa na sapoti kutoka juu......tujikumbushe ishu ya jairo na tetesi kadhaa kuwa pinda alikuwa anataka kujiuzulu.......binafsi ndani ya CCM ya leo sioni yeyote mwenye uwezo wa kuivusha hii Nchi hapa ilipokwama,ccm kazi yao imebaki kulinda kwa maovu yao.

Huo ndiyo ukweli ila Watanzania wako kama vile wamelaaniwa. Wa kupewa khanga, tshirts na pilau basi wanagawa kura kama njugu.
 
Yaaani Pinda awe Rais? Duh

Why not? Uzuri wa Democrasia ni kuwa kila mtu anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Kama Mhe ataweza kuwashawishi Wapiga kura basi atakuwa. Duniani kuna maajabu mengi hivyo hata hilo lawezekana
 
Hatutaki rais anayelialia ovyo na mdahifu kiafya.
Pinda's got lots to settle with the Zanzibaris before they can consider him for the Presidency. Does Pinda still deem Zanzibar not to be a Sovereign Country despite the autonomy granted under auspices of their 2010 Constitution??
 
Hapa nikiandika nitaandika mno labda niseme machache tu.
Leo akiwa anahutubia kwenye harambee ya kuchangisha fedha nadhani za ujenzi wa Hospitali amenishangaza pale alipotoa takwimu kuwa daktari mmoja mikoa ya Ziwa anatibu watu takribani 20 elfu hadi 25 elfu.

Sasa nikashangaa kuwa Madaktari walipoomba vifaa na nafasi za kufanya kazi pamoja na wale mabingwa kutaka wawezeshwe zaidi ili waweze kuwapatia wenzao mafunzo zaidi si waliwanyanyasa mpaka nasikia wamehama nchi? Mpaka kutupwa mabwepande? Sasa serikali hiyo hiyo Waziri Mkuu huyo huyo anadiriki kusimama mbele za jukwaa na kulalama namna hiyo? sikuamini alivyoliezea kwa utashi. Au ndio kusema hayo hakuyajua mpaka leo? Kwamba anajiandaa kuja kusahihisha akishakalia kiti? Mhhhhhh! .......... niwaachie na wengine muendeleze.
 
Nini nyuma ya uvumi/taarifa hizi? Je Pinda hayumo kwenye wajumbe wa CC waliotoa adhabu kwa makada wa Chama waliokiuka taratibu za chama ambazo naye anazikiuka? Je yeye ni jeuri au mjinga kiasi hicho ikiwa kweli anauhitaji huo urais? Sidhani! Kama ni hivyo basi kuna kitu nyuma ya uvumi huu na tusubiri.
 
Hii nchi haiishi maajabu wallah,sasa naanza kuelewa kwa nini zile jitihada za kuchepusha ile barabara ya sumbawanga mpanda ipite kwake
 

jk.gif

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipiga kura wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho huku akiwa jirani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Picha ya Maktaba
​


Na Neville Meena

Jumapili, Agosti 24 2014 saa 10:17 Asubuhi

KWA UFUPI
Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho alisema wingi wa wanaojitokeza kutaka kuwania urais ni njia ya kuunda mtandao utakaomwezesha mtu fulani au mmoja kunyakua tiketi hiyo.

Dodoma
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameingia rasmi katika mbio za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatua ambayo imebadili mwelekeo wa kinyang’anyiro cha nafasi hiyo kubwa ya uongozi nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.


Gazeti hili limethibitisha kwamba Pinda tayari ameamua kujitosa kuwania nafasi hiyo kupitia CCM ambayo tayari inawaniwa na makada wa chama hicho wasiopungua 15 na baadhi yao wameishatangaza nia zao kwa nyakati tofauti.

Habari kutoka ndani ya CCM zinasema uamuzi wa Pinda kuwania urais mwaka mmoja tu kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwakani, umesababisha kiwewe miongoni mwa wagombea na kunakifanya kinyang’anyiro hicho kuchukua sura mpya.

Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM aliliambia gazeti hili siku chache zilizopita mjini Dodoma kuwa: “Na sisi tumesikia kwamba PM (Waziri Mkuu) amejitosa na kama ni kweli atawasumbua wagombea wengi kutokana na rekodi yake hasa katika uadilifu.”

“Yeye (Pinda) ana faida tatu kubwa; kwanza hana kundi katika chama, anaelewana na watu wote, pili nafasi yake ya uwaziri mkuu inampa nafasi ya kufahamika kwa watu wengi na tatu rekodi yake ya uadilifu, hana kashfa za ovyoovyo, labda kama ataharibu dakika hizi za mwisho,” alisema kiongozi huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Wengine ambao wamekuwa wakitajwa kuwania uraia kupitia CCM ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na mtangulizi wake katika nafasi hiyo, Frederick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Wegine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta. Wengine wanaotajwa ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Katiba, Asha-Rose Migiro.

Pia wamo Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Balozi Ali Karume.


Wasomi

Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho alisema wingi wa wanaojitokeza kutaka kuwania urais ni njia ya kuunda mtandao utakaomwezesha mtu fulani au mmoja kunyakua tiketi hiyo.

“Watu wanapiga kampeni katika harambee kwa njia ya kutengeneza mitandao, kwani ukifika wakati wa chama kumpitisha mgombea, asiposhinda ataibuka na kuwaeleza kuwa mnaoniunga mkono mimi muungeni fulani,” alisema.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema kujitokeza kwa idadi kubwa ya wanaowania nafasi ya urais, kutatoa fursa ya wananchi kutambua udhaifu wa kila mmoja jambo litakalowezesha kupatikana kwa mtu sahihi wa kupeperusha bendera ya chama hicho.

“Wakiwa wengi, kila mmoja atataka kuonyesha umahiri wake na sisi ambao ni wananchi watawaliwa tutaweza kutambua upungufu wa kila mmoja, jambo litakalosaidia kupatikana kwa mtu sahihi,” alisema Mbunda


Kambi ya Pinda
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa siku kadhaa mjini Dodoma ambako vikao vya Bunge Maalumu vinaendelea umebaini kuwa kambi ya Pinda inaongozwa na Mwenyekiti wa Mamlaka za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi.

Inadhaniwa kuwa Dk Masaburi atatumia ushawishi wake kwa viongozi wa mamlaka za miji na wilaya zinazoongozwa na wenyeviti wa halmashauri na mameya wa miji, manispaa na majiji kumuunga mkono mgombea huyo ambaye pia hivi sasa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ziko chini ya ofisi yake.

Wiki hii kundi la wafuasi wa Pinda likiongozwa na Dk Masaburi lilikuwa mjini Dodoma likijaribu kutafuta kuungwa mkono na makada viongozi wa CCM ambao walikuwa wakishiriki kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho pamoja na wale walioko katika Bunge Maalumu. Habari zinasema mbali na Dodoma, tayari kambi hiyo imeshafanya vikao kadhaa jijini Dar es Salaam na Visiwani Zanzibar lengo likiwa ni kutafuta kuungwa mkono na makada wa CCM katika sehemu hizo. Hivi sasa nguvu za Pinda zinaelekezwa katika mikoa mingine nchini kwa lengo hilohilo. Kutokana na kasi ya kambi yake, wafuasi wa baadhi ya wagombea wameanza kufuatilia mwenendo wao kwa lengo la kukusanya ushahidi wa kile wanachokiita ‘rafu’ zinazochezwa ili kupata ushahidi unaoweza kutumika dhidi ya mgombea huyo wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM utakapoanza mapema mwakani.

Itakumbukwa kwamba makada watano wa chama hicho ambao ni Lowassa, Membe, Makamba, Wassira na Ngeleja wanatumikia adhabu na wapo chini ya uangalizi wa chama hicho baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kuanza kampeni za urais kabla ya muda kutangazwa.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema hivi sasa ni mapema mno kusema ni lini mchakato wa kupata wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama hicho utaanza na kwamba wakati mwafaka ukiwadia wananchi watafahamishwa.


Uwezo, udhaifu wake
Hata hivyo wakosoaji wake wanasema Pinda akiwa Waziri Mkuu hana cha kujivunia na kwamba amekuwa mzito kufanya uamuzi mara kadhaa kiasi cha kusababisha baadhi ya mambo muhimu ya nchi kukwama na kwamba kwa maana hiyo hastahili kuwa rais.

“Ni kitu gani ambacho nchi inakikumbuka kuhusu huyu bwana ambacho alikifanya katika miaka yake ya uwaziri mkuu, kama alikuwa kwenye nafasi kubwa kiasi hicho na hakuna alichofanya, atawezaje kumudu madaraka ya mkuu wa nchi?” alihoji mmoja wa makada wakongwe wa CCM.

Waziri mmoja wa sasa (jina tumelihifadhi), alisema Pinda hana uwezo wa kuongoza nchi, kwani wao wakiwa mawaziri ameshindwa kuwasaidia katika kero mbalimbali walizokuwa wakimfikishia kama kiongozi wao.

“Muulize waziri yeyote kuhusu uwezo wa jamaa, kila kukicha tunampelekea mambo tunayokutana nayo, lakini hakuna kinachowezekana kwake, atakwambia subiri leo, subiri kesho na hatimaye jambo linaishia hivyohivyo,” alisema.

Kwa upande mwingine, watetezi wake wanasema Pinda wanayemnadi ni yule aliyepata kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Tamisemi) kiasi cha kuonekana anafaa kuwa Waziri Mkuu.

Wanasema kushindwa kwake kufanya kazi ipasavyo ni matokeo ya sababu zilizomfanya mtangulizi wake, Lowassa kung’oka katika nafasi yake.


CHANZO: Mwananchi

Pinda ni kiongozi bora sana na nichaguo la wengi nyie endeleeni kumponda lakini jueni ndie Rais ajae
 
pinda anatafuta tu kuombwa awe kambi gani na labda kuteuliwa uwaziri na rais atakayeshinda , hana lolote!
 
Back
Top Bottom