Kintakunte07
Member
- Aug 25, 2014
- 5
- 3
Kiongozi mzuri Tanzania yupo ila tu muda wake haujafika
Is this a joke?Huyu awe Rais......labda wa katavi!
Dr Slaa aliwahi kusema matatizo tunayopata kutokana na kila mmoja kujiona anafaa kuwa rais ni matokeo ya rais aliyepo kushusha hadhi ya urais. Baada ya Pinda kutumbukia kwenye kinyang'anyiro eti wazanzibar wanasema hafai kwa sababu aliwahi kusema Zanzibar siyo nchi.
Binafsi pamoja na kuamini Zanzibar siyo nchi lakini wako sahihi maana pamoja na kutoa kauli hiyo Zanzibar walivunja katiba ya Jamuhuri ya muungano kutamka kwenye ibara ya kwanza ya katiba yao kwamba Zanzibar ni nchi. Alikuwepo na aliapa kulinda katiba hiyo hiyo iliyovunjwa kwa hasira za kauli yake, alinywea kutoa kauli yoyote mpaka leo.
Ametoa kauli mbili za kuvunja katiba, pale alipotaka wanaoua albino wauawe na kauli kwamba wasiotii amri za polisi "wapigwe tu". Hatuwezi kuwa na rais asiyeweza ku-control mdomo wake. Hebu fikiria kauli hizo tata angezitoa akiwa rais na ukizingatia marais wetu Afrika huwa hawaombi radhi kufuatia kauli zao za hovyo ingekuwaje?
Tumeona bunge la katiba likivurugika tokana na kauli za Kikwete, sasa Pinda asiyeweza kupima kauli zake anautaka urais. Sasa nimeani rasmi Ccm hawana mgombea bora, Kigwangala! Ngeleja! Makamba! Lowassa!! Pinda! Mwalimu alikufa na Ccm hii ni Ccm akademia.
Kiongozi mzuri Tanzania yupo ila tu muda wake haujafika
Kiongozi wa kweli ndiye mteuliwa kutoka kwa Mungu,wale wenye Kumcha Mungu mtuambie ni nani kiongozi wa kweli na mtuthibitishie hilo bila ya kusitasita,awe ni wa ccm au Chadema.
Hakika hakuna mkamilifu hata siye tunaoandika humu hakuna mkamilifu.
CHADEMA mbona hamjisemi, au kwa kuwa chama chenu ni cna kifalme na kwa maana hiyo mgombea wenu anafwhamika?Watu hawatakiwi kumshangaa pinda kwani bado wengi watakuja na tutawasikia mpaka itimie ile idadi iliyotajwa na ritz.
Kitu cha msingi cha kujiuliza je kati ya hao wote wanaotajwa ni nani aliye msafi .Watanzania tumekaririshwa tu baadhi ya watarajiwa hao juu ya uadilifu wao .
Swali langu je kundi moja litakuwa tayari kuliunga mkono kundi jingine,au tutegemee mgawanyiko ndani ya ccm.
Kwa sasa hali ilivyo ni rahisi mno kwa chadema kushinda kiti cha uraisi kuliko hata kuongeza idadi ya wabunge . Kama itatokea hivyo basi waziri mkuu itabidi atoke ccm kwani ndiyo chama kitakacho pata wabunge wengi katika uchaguzi ujao ,ngoja muda uje tuone vioja hivyo.
Kiongozi wa kweli ndiye mteuliwa kutoka kwa Mungu,wale wenye Kumcha Mungu mtuambie ni nani kiongozi wa kweli na mtuthibitishie hilo bila ya kusitasita,awe ni wa ccm au Chadema.
Siyo kwa maana unayoijua ww! Hapa anajadiliwa mtu anaetaka ofisi kubwa kuliko zote tanzania na si mtu yeyote ndugu. Ni lazima wananchi wamjue vizuri kabla hawajamkabidhi hiyo ofisi na si vinginevyo.wanafiki ndiyo wanajadili watu ila jamii ya wastarabu inajadili ishu wala siyo watu.