Pinda abadili upepo wa CCM urais 2015

Pinda abadili upepo wa CCM urais 2015

Ni haki yake kikatiba

Haki ya mmoja haiwezi kiwa zaidi ya haki za wengi!!!!!!

Albino wana haki ya kuwa salama na kuishi bila hofu lakini hali ikoje na wenye dhamana wanasemaje???!!!

Haki ya mtu huwa na nguvu kama anaweza pia kusimamia haki za wengine!!!!
 
Pinda kapinda kweli!!!!naomba ccm wampitishe ili chadema/ukawa washinde kiulaini
 
Rais wa sasa ameufanya urais kuwa nafasi ambayo kila mtu anaiweza...., kufanya teuzi ya watendaji mbalimbali ni jukumu kubwa zaidi.
 
na mimi nasubiri kuoteshwa nchi ya vituko...yaani ukilala ukiamka njozi njema poa
 
msimbeze mh pinda ana uzoefu wa miaka 40 ikulu sihaba,japo anayumbishwa na mfumo wa sasa wa jk,ni mtu mwajibikaji sana
 
Ma CCM Bwana,wote wanaoutaka U Rais ni wagonjwa,Ma mvi,Magufuli na sasa Pinda...
 
"Adaiwa kuanza kampeni, wengine walalamikia rafu, Kinana asema uteuzi bado!"

.. Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikihaha kutibu makovu yanayotokana na harakati za kuwania urais wa 2015, imethibitika kuwa waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameingia rasmi katika mbio za kuwania urais kupitia CCM, hatua ambayo imebadili mwelekeo wa kinyang'anyiro cha nafasi hiyo kubwa ya uongozi nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, ...

Chanzo: MWANANCHI JUMAPILI

huo uwaziri mkuu tu umemshinda ataweza urais
 
Jk alifanya uraisi kuwa rahisi mnoo.

Tatizo siyo JK.tatizo ni sisi watanzania hatujui haki zetu na wachache wanaojua ama wamezidiwa na wajinga wengi au waoga kupigania haki yao.Kwa nchi ya namna hiyo (YA WAJINGA) Duniani mtu yeyote anaweza kutawala na asipate shida.
 
nimefurah alivyotangaza ili kelele zipungue..
Ni mwiba kwa wengi.

Wengi wanamuona ni dhaifu,bila kujua kwamba yupo hivyo kutokana na MUKULU..
 
dah,tanganyika kuna vituko,hata pinda nae anagombea jaman,haya ni maajabu ya dunia....ila namshauri kama huwa anapita jf,aache nia hiyo maana hana uwezo wa kuwa rais.:hail:
 
Mmmh mbona naskia bi mkubwa anaanza kwanza kugombea ubunge jimbo la Lindi mjini?

Hilo ni kweli nia alikuwa nayo lakini mzee wa kaya kamwambia mwakani Bi. Clinton ataimba uteuzi wa chama chake, sasa watatumia vigezo vya kwanini marekani wameona mke wa rais mstaafu anaweza isiwe sie? Yes, we can! Kingine ni kwa kuwa bi mkubwa ameshiriki maamuzi mengi sana akiwa Magogoni basi anaijua nchi vizuri sana. Kubwa ni kuwa mzee wa kaya ameonesha maneno ya Nyerere kuwa Ikulu sio mahala pa mchezo kuwa si sahihi, kwani waTz wanataka elimu, ardhi, afya, barabara na sio nani ni rais
 
Waziri mkuu pinda ametangaza nia ya kugombea urais kwa kupitia ccm.adaiwa kujidai ana uzoefu miaka 4o ikulu.atumia wajumbe wa kanda ya magharibi kujinadi napia makanisani.tzdaima source

Mwanzoni nilifikiri Pinda anabusara ya kuona mbali!....

Hata hivyo bado sijaamini kama kweli katangaza nia hiyo.
 
nchi ilvo na matatzo hv c atakuwa analia mda wt
 
Saaana. Kigangwala, tibaijuka, migiro, na naskia mpaka John komba nae ndani ya Nyumba. Stay tuned.

Niliwahi kuandika uzi kutoka inner circles za CCM majina matano yatakayopendekezwa na CC ya CCM kwenda kupigiwa kura na NEC ya CCM jina la Pinda ni la kwanza. Kutokana na source hiyo Pinda kwasasa ndiyo chaguo la Ikulu.

Majina manne tayari yanafahamika kwamba yatapendekezwa na CC ya CCM. Jina la 5 bado ni kitendawili na litategemea na upepo wa kisiasa ndani ya CCM wakati huo.

Majina 4 ambayo yatapitishwa na CC ya CCM in chronological order in
1. Mizengo Pinda (current sitting PM)
2. Jina moja la Mzanzibari (kudumisha Muungano)
3. Prof Tibaijuka/Asha-Rose (gender balance)
4. Prof Mark Mwandodya (alifanya vizuri kinyang'anyiro cha 2010)
5 ................,.......... (???)

Jina la 5 ndipo wapoangukia wagombea wengi na ni moja tu atakayepita chekecheo hilo la CC ya CCM. Kati kapu hilo ndio tunawakuta

Edward Lowassa, Samuel Sitta, Benard Membe, Steven Wassira, Frederick Sumaye, January Makamba, William Ngereja, Pombe Magufuri, Harrison Mwakyembe, Kigwangalla, etc

Swali linalowasumbua wengi je ni jina gani kutoka katika kapu hilo litapitishwa na CC ya CCM kukamilisha idadi ya wagombea 5 watakaopendekezwa na CC ya CCM kwenda NEC.

Hii ni headache kwa CCM kama chama na kwa wasaka urais kupitia CCM as individual
 
Back
Top Bottom