Pinda abadili upepo wa CCM urais 2015

Pinda abadili upepo wa CCM urais 2015

Watanzania wanamuhitaji prof. Anna tibaijuka kuchukua urais na sio vinginevyo. Ana uadilifu mkubwa sana
Na wewe unavyohangaika na tibaijuka haya bana muombe mungu sana asikilize maombi yako.
 
Sishangai Pinda kujitosa kwani urais umekuwa kama mwenyekiti wa kijiji kama kina Makamba Kigwangalla Ngeleja Mwigulu Lityson Wassira na wajinga wengine wa aina hiyo wanajiandaa kuwania ofisi kubwa nchini,itakuwa yeye waziri mkuu asijione zaidi ya hao mbulula.
Kuelekea 2015 tutashuhudia wapumbafu wengi wakidhalilisha taasisi ya uraisi.
Of all the people,Pinda should not dream of becoming our next president,because even as PM he has failed to deliver.
 
Sasa jamani kama amekuwa waziri mkuu na ameshindwa kuwa active - maana ni kama alikuwa hayupo kabisa. mambo hayaendi na yeye yuko hapohapo; huo urais atauwezea wapi????? Watanzania hatutaki watu wanaofanya kazi kwa mazoea, tunataka watu active na creative. Huo uzoefu wa miaka 40 anaouzungumzia anajumlisha na ule wa kuandika hotuba za raisi? Tunataka watu active - hata kama hawana uzoefu - watu ambao wataipeleka Tanganyika mbele - sio kupiga domo tu. Tumechoka kujivunia amani tu - tunataka tuanze kujivunia uchumi sasa.
 
Kambi zingine kaeni mkao wa kuliwa, naona wanamtandao wanawachezesha mdundiko nanyi ni wabara tena milimani kulee.
Mpaka hii "shughuli" inaisha mtashtukia mwali kishajifungua.
 
Pole pole.......................................maumivu ya kichwa..................
 
Sidhani Kama Watanzania wanahitaji Rais anayelia wakati Albino wakiuwawa badala ya kuchukua hatua kwa wauwaji. Katiba mpya futa hii cheo Waziri Mkuu tusijepata Pinda mwingine. Kama kuna Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wa nini?

Wakati tunapata uhuru Rais wetu wa kwanza J.K wa ukweli alisema nchi Ina maadui wakuu wanne;Umasikini, Ujinga na Maradhi. Miaka hamsini baada ya uhuru mna kuwa na Waziri mkuu anayeona fahari kuwa maskini!
 
Wakati makada watano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakitumikia adhabu ya mwaka mmoja kwa kosa la kuanza kampeni za urais wa 2015 kabla ya muda, Waziri Mkuu Mizengo Pinda naye anadaiwa kutangaza kusudio la kuwania urais, Tanzania Daima Juamapili limedokezwa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Pinda alitangaza nia yake katika kikao cha wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kutoka mikoa sita ya kanda ya Ziwa, alichokiitisha juzi jioni Ikulu ndogo jijini Mwanza.

Katika kile kinachoonekana kama amepangwa rasmi kimkakati, Pinda aliwaeleza wajumbe hao kwamba hakuwa na nia ya kugombea lakini ameshawishiwa na baadhi ya maaskofu, masheikh, mkewe pia na anaungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete.

"Waziri Mkuu alituita juzi sisi wajumbe wote wa mkutano mkuu Taifa kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa. Tuliitikia wito tukakutana naye hapo Ikulu ndogo ya hapa Mwanza. Hakukomea hapo, bali aliutuambia kuna majina ya watu watano bora akiwemo yeye, Edward Lowassa, kijana, mwanamke na Mzanzibari kuwa ndiyo watakayopitishwa na Kamati Kuu kwenda NEC," kilieleza chanzo chetu.

Ingawa Pinda hakupatikana kwa simu kuzungumzia madai hayo, ila mtoa taarifa hizo ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe walioshiriki kikao hicho, alisema kuwa kada huyo wa CCM alijivunia utumishi wake wa mumrefu Ikulu tangu mwaka 1974.

Kwamba, alisema kuwa hatakuwa rais wa kutumia fedha chafu kuhonga wajumbe kama wanavyofanya baadhi ya wanasiasa wengine, bali atatumia fedha za marafiki zake kuwasaidia wale wote watakaomuunga mkono.

Inaelezwa kuwa kila mjumbe alipewa posho ya sh. 50,000 kwa ajili ya nauli, chakula na malazi kwa siku moja, kiwangoa ambacho hata hivyo kimelalamikiwa na wajumbe wakidai ni kidogo.

"Hadi makatibu wa CCM wilaya za mkoa wa Mwanza wamepewa maelekezo na kigogo mmoja wa mkoa ili wamuunge mkono Pinda katika safari yake ya kuutaka urais," alisema na kuongeza.

Pinda amelazimika kukutana na wajumbe hao ili kujenga ushawishi kwao, kwa sababu anahofia nguvu kubwa ya kukubalika Lowassa ndani ya chama katika mbio hizo za urais 2015.

"Tulipomaliza kikao na Pinda pale Ikulu na kutoka nje, wajumbe wengi walipuuza mpango wake huo wakidai hafai kuwa Rais. Walisema kwanza yeye mwenyewe hana nia ya kugombea ila ameshawishiwa tu. Pili, wajumbe walihoji Pinda ni mjumbe wa Kamati ya Maadili, NEC na Kamati Kuu ya chama, aliyeshiriki kuwafungia Lowassa, Stephen Wassira, January Makamba, Bernard Membe, Fredrick Sumaye na William Ngeleja kwa miezi 12 kutokana na kukiuka taratibu na kaunza kamapeni mapema, kwamba yeye itakuwaje," kilisema chanzo hicho.

Pinda aliingia jijini Mwanza juzi na kwenda kumhani Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga aliyefiwa na mtoto wake, Vedastus Kitwanga na jana usiku aliongoza harambee ya Taasisi ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, iliyofanyika jijini Mwanza.


Source: Tanzania daima


Maoni yangu

PINDA ANASEMA ETI ANAJIVUNIA KUFANYA KAZI IKULU KWA MUDA MREFU KUANZIA 1974 NDIO SIFA YA KUWA RAIS WA WATANZANIA MIL 45 NA ZAIDI.

-KWELI HIZI NDIO SIFA ZA RAIS?
-PINDA SI ATUAMBIE AMELIFANYIA NINI HILI TAIFA ZAID YA KUPALILIA RUSHWA NA UFISADI?
-PINDA HUYU ALIYERUHUSU RAIA WANAODAI HAKI ZAO WAPIGWE ETI KWA SABABU AMECHOKA ?
-PINDA ALISHASEMA AMECHOKA KUFANYA KAZI SASA ANATAKA KWENDA IKULU KUFANYA NINI?
-AU NDIO ANATAKA KWENDA KUPUMZIKA BAADA YA KUCHOKA AKILI NA MWILI?
-PINDA WATANZANIA HATUHITAJI WALIOCHOKA TUNAHITAJI WATU WENYE NGUVU WAKATUMIKIE TAIFA HILI.
-PINDA NA LOWASA WAKAE PEMBENI MAANA HATUHITAJI RAIS AMBAYE KILA SIKU WANAENDA UJERUMANI KUCHUNGUZWA SIKIO NA PRESHA KWA FEDHA ZA WALIPA KODI
-PINDA HUYU ALIYEJIBADILI NA KUWA MAHAKAMA KWAMBA WANAOKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUUA ALBINO WAUAWE HAPO HAPO, JE AKIINGIA IKULU ITAKUWAJE?
 
acha wivu wa kike,,,,,,,,,ni haki yake kikatiba.
 
Kumbe yeye nae ni miongoni mwa wale walio itumbukiza Tanzania na watu wake kwenye wimbi la umasikini!! Hata bure"
 
Pinda amekuwa legelege sana. Taasisi nyingi za serikali zimepwaya kiutendaji.
 
Back
Top Bottom