Pinda aapa bila Msaafu wala Biblia

Pinda aapa bila Msaafu wala Biblia

Huyu ndo mkiristo hodari,sisi tuliopitia malezi Ya Seminari tunajua uzito wa kitabu kitakatifu. Kama unajua kuna ila zilitumika kuiba au kufanya kitu kinyume na maadili kamwe huwezi kuapa kwa kugusa kitabu kitakatifu la sivo yanakupata makubwa. Pinda ni mkristo safi,mlezi ktk kanisa katoliki la Hananasifu,anaielewa dini yake vilivyo. Kwa kuwa umelazimishwa uPM basi mzee Pinda uape bila mwongozo wa Mungu. Nakusukuru kwa kuisimamia Imani.
 
Hicho kiapo alichokula ni batili ama niseme aliapa kwa nafsi yake mwenyewe. Na hii itamsaidia kutowajibika kwa Mungu muumba pale atakapokwenda kinyume na wajibu wake. Anahukumika nafsini mwake kwa uovu aliotenda na hivyo inamlazimi kutafuta njia ya kukwepa hukumu ya Mungu moja kwa moja. Nina wasi wasi na tendo hili wanalolifanya lina mkono wa Yule nabii wa ccm Sheikh yahya. Kwa historia ya nchi yetu haikuwahi mtu kuapa bila kitabu. Siku zote viongozi wamekuwa wakiapa kwa kutumia misahafu au katiba(Kingunge's style). Hii ni ishara tosha kwamba sasa hivi taifa lina watawala na mamlaka haramu!
 
:bowl:mmesahau yaliyompata kaijage aliposahau cd ya wimbo wa taifa siku ya staz na moroko? sasa tumsake kaijage mwingine aliyesahau misahau chamwino!!!!:A S angry::smile-big:

kaijage hakuisahau, ilikuwa ya kuburn ikagoma
 
Katika nchi ya mafisadi kama yetu, kukubali kuwa utakuwa mkweli na Mungu awe shahidi, kwa mtu mwamnifu kweli kweli ni ngumu. Pinda anajua kuwa ni lazima atafuata matakwa ya mafisadi tu.
 
Pinda ni mtu ambae siku zote amekua na guilty consiousness kubwa sana..

Anaogopa kumhusisha mnyaazi mungu kwenye udhalimu na ghilba walizofanya. Anatambua uwepo wao madarakani hauna chembe ya baraka za mungu maana ni kinyume kabisa na mapenzi ya allah. Aanogopa adhabu kali zitazowaangukia kwa kuendelea kumdhihaki mola.

Mungu aliwapa watu nguvu na mgombea wetu na watu wote tulimchagua ila utawala huu kwa ghiliba, mabavu na hila, wameweka utawala wao. Wanajua fika kwamba mungu hakupanga wawe wao...

Pinda anahofu.. ingawa tunamjua ni mkristo, ameshindwa kumhusisha muumba kwenye kiapo chake maana anajua hajaipata hiyo nafasi kwa mipango ya mungu.

mkuu hapo napata picha kidogo..
 
huyu jamaa mbona nasikia ni mcha Mungu vilivyo? Mcha Mungu hawezi kufanya kitu bila ya kumhusisha Mungu. Jamani hii alichofanya mbona kinaleta maswali?
 
Nimeipenda hii kwani huwa wanaapa na vitabu vitakatibu kisha wanakuja kufanya kinyume chake
Siyo kweli kama Pinda ameapa bila msahafu. Ameapa akiwa ameshika biblia na imeonyeshwa kabisa

usipotoshe watu mkuu

source: TBC
 
Wakati wa kuapishwa wabunge alitumia kitabu gani? Na kama alitumia Biblia sasa kulikoni?
 
tujue kuwa anaapishwa!!! hajiapishi mwenyewe, anaapishwa!!, kwa kuzingatia hili Mwalimu katika hotuba zake alisisitiza juu ya kuapa unapopata manadaraka, aksema, kama ni Muislamu attapa kwa Quraan, ama ni Mkristo attapa kwa Biblia, kama hana dini tutatafuta utaratibu wa kumuapisha, lakini lazima aape ama kwa biblia ama kwa Quraan. sasa mzee wangu hakuwa na Biblia wala Quraan wala hatukuambiwa ni utaratibu gani umetumika kumuapisha.... hii ni kali ingine ya awamu hiii!!

asante mtoa mada
 
Kwa kumbukumbu zangu Pinda ni Mkatoliki (I am not very sure). Nadhani kama anasoma Biblia atakuwa ameukumbuka sana ule mstari unaosema ... dhambi zote zitasamehewa, lakini dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu haitasamehewa kamwe...
 
pinda apa.JPG
 
Huyu ndo mkiristo hodari,sisi tuliopitia malezi Ya Seminari tunajua uzito wa kitabu kitakatifu. Kama unajua kuna ila zilitumika kuiba au kufanya kitu kinyume na maadili kamwe huwezi kuapa kwa kugusa kitabu kitakatifu la sivo yanakupata makubwa. Pinda ni mkristo safi,mlezi ktk kanisa katoliki la Hananasifu,anaielewa dini yake vilivyo. Kwa kuwa umelazimishwa uPM basi mzee Pinda uape bila mwongozo wa Mungu. Nakusukuru kwa kuisimamia Imani.

aaah umenikumbusha sana KASITA SEMINARI..true mkuu anajua kura zimechakachuliwa sasa hawezi kuapa kwa kukidhihaki kitabu kitakatifu
 
Back
Top Bottom