Pikipiki za honda zinauzwa

Pikipiki za honda zinauzwa

WP_20160330_15_33_28_Pro.jpg
 
HONDA TUF 125. STOCK MPYA IMEKUJA. NI TOLEO JIPYA INA STARTER. BEI MILLION 3.8.
tuf 125.jpg
 
Honda 250 cc,hizo hamna kwa sasa. huwa zinakuja kwa oda maalum. kama mteja ambaye anahitaji tumwagizie kutoka nje basi tunampigia hesabu ya gharama na bei ya pikipiki. analipia kisha anasubiri mzigo wake.
 
Jokielias na mm naulizia bei ya VROX 125 bei na ubora wake pia
 
Jokielias na mm naulizia bei ya VROX 125 bei na ubora wake pia
VROX 125 HIZO HATUUZI. TUNAUZA HONDA DREAM 110 SCOOTER LAKINI STOCK YAKE IMEISHA. NI ZA KUSUBIRI. BEI MIL 3.1
 
Ipi Bora? mi nitakwambia Honda cg 110 ni bora kuliko boxer150. kwasababu;

Honda CG110, Sifa yake ya kwanza ni engine yake ni cc 110, ni nyepesi. Inatembea spidi mita 120 kwa saa. Honda cg 110 inakimbia kwa mwendo wa wastani. Ina mngurumo wa chini yaani silencer yake ipo chini Ina carrier ya kubebea mizigo isiopungua kilo 120. wadau wengi wamependa Honda cg 110 kwenye ulaji wake wa mafuta ni mdogo kuliko pikipiki zingine. inaweza kutembea km 70 kwa lita. kwahiyo kwa bajeti iko vizuri. kwa matengenezo yake utasahau gharama kwa maana spare zake kuisha inachukua miaka 2 mpaka mitatu ndio ubadilishe spare.

Kwa Boxer 150, ina engine cc 150 kwahiyo ni kubwa na nzito. hata kwenye ulaji wake wa mafuta ni mkubwa inatembea km 40 kwa lita. watu wanachopendea boxer 150 ni kwamba ina spidi na ina mwendo wa hatari kuliko piki piki zingine. na vile vile ina carrier kubwa ya kubebea mizigo mizito. tatizo la boxer ni kwamba gharama za kuitunza. ukinunua boxer mpya baada ya miezi mitatu utaanza kubadilisha gasket, mara spocket mara hiki nk. kwahiyo utajikuta unaingia gharama za kwa mara kwa mara kwenye boxer. lakini pamoja na hayo bado wapo wabongo wengi ambao hawajali hasara kwasababu wanaziona boxer zipo nyingi mtaani basi wanakua hawajui effect zake baadaye. kwahiyo shekhe nimeshakujibu hapo.

Hivi boxer bm 150 ina spidi ngapi maximum?
 
honda cb 125 cwez pata kwa mil 2.2?
Huwezi pata honda cb 125 kwa mil 2.2. Bei halisi ni Mil 2.8. Tunazo Honda CG 110 Bei Mil. 1.9 ni nzuri inafaa kwa matumizi ya usafiri. kama upo dar. njoo msasani ofisini kwentu au nicheki 07175182359, 0689866100.
 
Back
Top Bottom