Nakuelewa sana mkuuSawa mkuu kama ulivosema kuwa inauma kuona mke/ mmeo anawasiliana sana na ex wake kuliko wewe, lakini ( km nlivosema wanaume) wanakuwa wazito kuwa na mawasiliano ya furaha na wake zao basi mke anaamua kuanza ama kama yalikuwepo basi ndo yanaongeza kasi kuwasiliana na wengine. Hii ni mbaya sana hata story mme hataki lkn akipigiwa sim anatia story hata zaid ya nusu saa. Kwa mkewe ni habari ya ada, chakula, fundi, msiba, uginjwa, mchango wa harusi na yanayo fanana...wanawake wameumbwa kupenda kusikilizwa akiongea kwa hiyo mtu akim ignore anaumia sn moyoni. Sasa relief inapatikana humo mitandaoni.
Mumeo ndo una uhusiano nae na sio michepuko so deal na mumeo ukijidai kudeal na michepuko unajishusia heshima na utaiua ndoa yakoKama matatizo ya ndoa yako ni michepuko ya mumeo, utaipigania vipi hiyo ndoa bila kugusa hiyo michepuko? Unless uwe unamaanisha huyo dada yako alikuwa happy tu uzinzi wa mumewe ila akawa anachukia michepuko yake tu
Teh mnyaki mimi kwanza pride+ego yangu hainiruhusu kupigania mwanaume kwa mdomo au ngumi, Never and and it shall never be my portion. Nilishashindwa zamani. Hili TuliacheYes if possible, sasa unataka kukaa tu unalia lia hapo wakati mwizi wako unamjua. Dili na mumeo lakini pia mchepuko wake vile vile
Umeongea vizuri Heaven Sent lakini mmh ila sista Mungu huyo huyo kasema anatupigania na sisi tunajipigania pia, so combine vyote. Yaani mlilie Mungu wako huku umeishaudunda mchepuko na mume wako udili naye kivyako, yaani peleka majeshi yote vitani, ndo point yangu
Malaya wa jinsia zote ndio wana advantage kubwa ya kuoa na kuolewa,
ukikutana na mwanamke anajua sana mapenzi, asilimia kubwa huyo ni malaya.
ukikutana na mwanaume anajua sana mapenzi, asilimia kubwa huyo ni malaya.
Binafsi nimeoa mwanamke anaye jua mapenzi
Heshima na nidhamu sikuangalia kabisa
Sawa dada,ila the pain of being cheated on Acha tu,na kila mtu anakuwaga na reaction yakeTeh mnyaki mimi kwanza pride+ego yangu hainiruhusu kupigania mwanaume kwa mdomo au ngumi, Never and and it shall be my portion. Nilishashindwa zamani. Hili Tuliache
Mke mwema, kitu chema, mke wa viwango, hapigani na michepuko ya mumewe. Anaanzaje kwa mfano, anajua thamani yake (ametoka kwa Bwana), anaanzaje kupigana na kahaba shimo refu? Tofauti ya mke na hawara iko wapi? Mumeo kashavutwa na kahaba shimoni, so mke relax, wewe ndo wakumtoa kule shimoni, ukimbwela na wewe unavutwa shimoni mchepuko unashinda. Keep in mind kuwa mumeo hana hofu ya Mungu au imepotea, hajamuogopa Mungu, atakuogopa wewe kwa sababu ni mkali sana? Afu ukute huo mchepuko ni wa kinyaki/ kikurya utakula nakozi na mume asirudi teh
Umeshajua mumeo ana mchepuko, and unataka kumkomboa mumeo, umeongea naye na unaona masikio kaziba, PIGA GOTI KWA MUNGU period (Vita vyetu si juu ya damu na nyama). Mungu akamuokoe dhidi ya mafisi Yenye udenda huko nje na ampige upofu wa kiroho asione wengine huko nje ila mkewe, above all akamtie ile hofu yake. Kuanza kupigana kama hutokaribisha kichaa cha ndoa sijui. Afu kupigana kunaweza kuwa temporary solution. Kesho hali ikitulia mumeo anahamia kwa mwingine unaanza tu ndondi, hujapata kichaa kweli? Au ataenda kuchepuka kwa siri na usijue, utajua siku ukiletewa watoto au magonjwa. Kuwe mke mwema kweli, mke wa ratiba( Mungu, Familia, Kazi) afu uone kama mume hajarudi na wewe kuepuka uchizi
Ujue michepuko haipo pale kunogesha ndoa yako bali kuharibu zaidi, unavyoishi kwa amani usidhani inapenda. Ndo maana unakuta mke hujui kama kuna lolote linaloendelea, lakini mchepuko utakutafuta hadi ujue kama ana-exist, ukichanganyikiwa ndo faraja yake ilipo. Wewe u ignore afu muoneshe kuwa wewe mke wa viwango. Kwanza imagine unamchokoza mtu wee afu hakujibu lolote, unamtukana still kakaa kimya. Kama una ufahamu mzuri lazima utashtuka. So kupigana na michepuko me kwangu sioni kama ni sawa mara nyingi. Kuna hata ile mume anarudi unamuwakia hatari (sometimes usijue kwamba mwenzio kapewa kinyama cha K huko teh), yani ukiongea tu ndo mume anahama na nyumba kabisa eti una makelele sana, kumbe ufahamu ushatekwa long maskini, umepata nini? Ulilipa gharama kuingia kwenye hiyo ndoa, lipa tena gharama kuhakikisha mumeo anarudi kwenye mstari.
Yes tatizo likitokea lazima u - shake kwanza. Ukiweza lia wee afu relax kwanza ili usije ukachanganyikiwa, na ukitulia ndo unafanya maamuzi ya busara sio kuanza kupigana huko na kukimbizana na michepuko. Usipokuwa makini utalose focus na maisha yako kabisa coz of michepuko, ile ipo kwa ajili ya uharibifu so wewe jipambanue kuwa ni wa viwango vingine. Kama ngumi zipige na mumeo basi, yeye ndo source ya hayo yote, si ndo kaifata michepuko nje.Sawa dada,ila the pain of being cheated on Acha tu,na kila mtu anakuwaga na reaction yake
Funzo zuri sana...NIMEIKUTA MAHALI NIKAONA NI VIZURI KU-SHARE
Kuna dada mmoja nikikuwa namfahamu miaka mingi sana. Kama miama 15. Kipindi hicho tukiwa ni wasichana wa miaka 25. Dada huyo ghafla akawa na mahusiano na mume wa dada yangu. Nilimchukia sana. Dada yangu alimchukia sana. Wote tulimchukia. Alikuwa mlevi. Malaya na anayependa kuvaa uchi. Hakuwa anajijali hata kidogo.
Mimi na Dada yangu tulikuwa tunatamani hata afe ama akatike miguu kwa namna alivyokuwa malaya na mshenzi.
Miaka ikapita. Kila ninapokutana na dada yangu haishi kunikumbusha Dativa. Kila siku tulikuwa tunamuongelea. Na kutamani tusikie hata kuna msiba kwao na amefariki dunia.
Baada ya miaka mitano kupita. Mimi nikiwa nimeahamaliza masomo yangu. Na sasa na niko kazini nafanya kazi yangu nzuri tu. Kijana mmoja akaniambia ananipenda na anataka kunioa. Miaka yote hiyo sikuwa na mahusiano kwani nilijua na mimi kina Dativa wataharibu ndoa yangu. So sikupenda ndoa kabisa.
Hivyo kijana huyo nikamkataa. Ni kijana kama wa 10 hivi kumkataa.
Siku moja nikampigia dada yangu simu. Akanieleza mambo hayo kwamba hana raha na ndoa yake kwani anajua Dativa bado wana mahusiano na mumewe. Japo hawaoni ila anajua wanafanya siri. Dada yangu alikonda. Ni mwaka wa 7 sasa Dativa hajamtoka akilini.
Nilikuwa naumia pia.
Maisha yakasonga.
Nilipata safari ya mwenda mkoani Arusha.Jumapili Moja nikasema ngoja niende kanisani kuabudu Mungu. Ni kanisa la karibu tu lakini sio kanisa la imani yangu.
Siku hiyo nilipata msukumo hasa. Tena baada ya kujua muimbaji maarufu wa nyimbo za injili yuko hapo.Nilivaa vyema. Kisha nikajipeleka kanisani.
Ibada ilianza.
Ilikuwa nzuri sana.
Mh...Baada ya muda kidogo nikasikia mtangazaji akisema Familia ya Bwana na Bibi Juventus inataka kutoa shukrani.
Bwana Juventus na mkewe na watoto wao wawili. Wa kike mwenye 4 yrs na wa kiume mwenye 2 yrs.
Walisimama mbele.
Mwanaume alikuwa kavalia suti nzuri sana na kapendeza hasa. Mrefu. Bonge la handsome.
Watoto nao walipendeza sana. Walivalia vyema hasa.
Kisha huyo mwanamke alionekana mrembo. Aliyevalia nguo za thamani na kupendeza pia.
Nilimtazama sana mwanamke huyo. Ni kama niliyekuwa namfahamu. Nilijiuliza je ni mtangazaji ama nimemuona wapi?Sura yake ilinipotea kidogo. Pengine ni kwa namna alivuopendeza zaidi.
Nilipuuza. Ila ni familia iliyonivutia sana.
Kisha Mume akamshika mkewe bega na kumpa kipaza sauti na kumwambia ashukuru Mungu.
Mwanamke yule alianza kwakusema...
mimi na mume wangu na watoto wetu wapendwa. Tunazo kila sababu za kumahukuru Mungu kwa namna anavyitutunza na kutupigania kila mara. Na leo tuko mbele zenu kutoa shukrani zetu mbele ya Mungu na mbele ya kanisa kwa maombi yenu pia.
Mungu ametubariki na mwezi huu tarehe 10 tutasafiri kwa ajili ya huduma nje ya nchi. Maombi yenu ni ya Muhimu sana.
Mimi Dativa na Juventus tunawapenda sana. Mungu awabariki.
Moyo wangu ulifanya paaaaa... ulinipasuka paaaaaa...
Huyu ni Dativa?yule kahaba.. malaya... niliyekuwa natamani afe hata kesho?Leo ana ndoa na watoto na maisha mazuri?Nimebaki nakataa ndoa kwa sabau yake... kumbe yeye anasonga mbele?
Dada yangu naye analia kumbe Davuta ni wa viwango vingine?.Nilichukia... nikajikuta naumia zaidi na ninawaza kwamba Mungu hayuko fair.
Niliwaza mpaka watu wakanisikia. Mama mmoja akaniambia mbona unaongea mwenyewe?Nimasema kwanguvu..Mungu hayuko fair. Ana upendeleo.
Huyo mama akanimbia kwanini?
Nikamwambia Davita alikuwa malaya sana. Na kaitesa sana ndoa ya dada yangu.
Yule mama alinitazama na kutabasamu kisha akasema...
SIKIA MWANANGU... HUJUI KAMA MAKAHABA WATATUTANGULIA KWENYE UFALME WA MUNGU?
Mh.. akili ilinirudi.
Kisha nikatoka nje na kuiacha ibada ikiendelea. Na kumpigia dada yangu simu na kumwambia...
Dada nimemuona Davita. Ni mwanamke wa viwango vingime. Sio yule kahaba tena. Ni ana mume na watoto na ameokoka.
Hembu acha kumuwazia mabaya kabisa. Mungu amempendelea.
Kuanzia hapo nikajifunza jambo.
Hatupaswi kuwawazia watu mabaya wala kuwaombea mabaya.
Hembu na wewe nikusaidie leo.
Acha kuuwaza mchepuko wa mumeo. Waza maisha yako..songa mbele. Usisimame kuwaza mchepuko ambao saa yoyote utatubu dhambi mbele za Mungu na Mungu wetu ni Mungu wa Kusamehe. Badala yake kaza buti katika maisha yako Mungu akuinue.
......The End..........
Afadhali kwa kwel achen kuwawaza wakin dativa nyie mtuombee tukimpata dativa nyie mnaenda church kupiga sala...

Hahaaaa duuuh eti kucheat ni nature yetu!! huku ni kujihalalishia uzinzi tu sista, hakuna mwenye kustahili kucheat. Wengi wetu tunaendekeza mihemko ya ngono na kupenda pesa sijui mali.Kujisaidia kwangu ni ile namlilia na kumkumbusha Mungu kwamba Mungu mkumbuke mume wangu, akaache njia zake potofu etc. Namkumbusha hapo na tunahojiana, sio kwamba nimekata tamaa.
Ngumi zitampa hofu yangu (of which I doubt pia) au hofu ya Mungu? Coz mwisho wa siku nataka mume wangu awe na hofu ya Mungu, that's it. Afu utapigana na wangapi, na wakati nyie kucheat ni nature yenu eti nimesikia teh? Na wengine miili yenyewe kama HS utaenda huko wewe ndo ubondwe sasa. Mishangingi/ Vibinti vyenyewe vya siku hizi, utarudi sura imechanwa viwembe + me naona ni Kujidhalilisha zaidi.
Eeh kila siku me nasikia eti kucheat nature yenu mtcheew. My kaka whether mtu awe tajiri au maskini (though kwa maskini kuna unaufuu maana hela ya kuhonga kushney), bila hofu ya Mungu, shughuli ipo. Afu mna excuse yenu kubwa siku hizi "no one is perfect", basi ndo tusiwaonye wala kufanya lolote tukiwafumania, kisa na sisi tu wadhambi pia. Ila nyie mkitufumania, hamkumbuki tena kama no one is perfect teh. Na jinsi siku hizi mnavyojihalalishia uzinzi, hamtaki ndugu wa mwanamke wakike majumbani kwenu, eti hamuwezi kujizuia khaa, soon mtahamia kwa kuku. Huwezi kuwaheshimu wa nyumbani mwako, hao wa nje ndo sijui utawafanyajeHahaaaa duuuh eti kucheat ni nature yetu!! huku ni kujihalalishia uzinzi tu sista, hakuna mwenye kustahili kucheat. Wengi wetu tunaendekeza mihemko ya ngono na kupenda pesa sijui mali.
BTW umeona kitu ya muheshimiwa wa zenji, wanaume rijali wenye pesa zao (wasio na hofu ya Mungu) hapo lazima anase,teh. Halafu wenyewe wanadai muwasamehe tu coz vitu vyenyewe hivi adimu afu vimenono hawezi kujizuia, ahaaaa akyanani mnalooo sista!!
Hahaaa hapo pekundu umesahau kumalizia kuwa tunakimbilia kutoa talaka, loooh!!Eeh kila siku me me nasikia eti kucheat nature yenu mtcheew. My kaka whether mtu awe tajiri au maskini (though kwa maskini kuna unaufuu maana hela ya kuhonga kushney), bila hofu ya Mungu, shughuli ipo. Afu mna excuse yenu kubwa siku hizi "no one is perfect", basi ndo tusiwaonye wala kuwasema tukiwafumania, kisa na sisi tu wadhambi pia. Ila nyie mkitufumania, hamkumbuki tena kama no one is perfect teh. Na jinsi siku hizi mnavyojihalalishia uzinzi, hamtaki ndugu wa mwanamke wakike majumbani kwenu, eti hamuwezi kujizuia khaa, soon mtahamia kwa kuku. Huwezi kuwaheshimu wa nyumbani mwako, hao wa nje ndo sijui utawafanyaje
Acha uchawi dogo, bado wanaishi pamojaImeishiaje?
Ndio sasa uache kutuombea mabaya sisi watu wa migombani... yani mahandsome flani hivi amazing. You know woram seyyying???Nimesoma mwishoni ila nimepata funzo.....asante kwa kweli