Pichaz: Dada Mage wa Tabora akitoa kikombe

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Wabongo wameniacha hoi na wala sina hata la kusema
picha ha habari kwa hisani ya keronyingiblog




Breaking news Uso kwa uso na Dada Mage!


DSC02997.JPG

Mimi na dada Mage (kati kati)

Baada ya kumaliza kutoa dawa kwa watu waliokwenda kwake tangu saa kumi alfajiri,jioni hii nilipata nafasi ya kumhoji Magreth Mutalemwa (40) mwenye Mume na watoto wanne,na mahojiano yetu yalikuwa kama ifuatavyo:


Keronyingi - Dada pole na kazi, unaitwa nani?
Magreth - Asante, naitwa Magreth Mutalemwa
Keronyingi - Unaweza ukaniambia pana nini hapa kwako mpaka watu wamejaa kiasi hiki?
Magreth - Mimi hapa natoa huduma ya maji
Keronyingi - Huduma ya maji kivipi?
Magreth - Nawapa watu wanaokuja hapa huduma ya kikombe cha maji
Keronyingi - Ili kiwasaidie nini?
Magreth - Kinawatibu magonjwa wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa mbali mbali
Keronyingi - Ni tangu lini na vipi wewe umejua unaweza kutibu watu?
Magreth - Tangu tarehe 21/March/2011
Keronyingi - Enhe nieleze ilikuaje?
Magreth - Nilikuwa nikipata msukumo baada ya kuoteshwa kabla ya tarehe 21 na kuidharau ndoto ile nilianza kupata matatizo lakini baada ya kuanza kufanya yale niliyotakiwa kufanya matatizo yakaisha ndio mpaka leo natibu watu.
Keronyingi - Dawa yako ina mchanganyiko wa vitu gani?
Magreth - Ni mti mmoja tu, ambao nauchemsha na kuwapa watu wanywe.
Keronyingi - Je umepata kuwasikia watu wengine wanaotoa tiba kama wewe ambao ni Mchungaji Mwasapila, Babu dogo wa Mbeya?
Magreth - Ndio nimewasikia
Keronyingi - Unawazungumziaje?

Magreth - Ah ninavyoona mimi huu ni uwezo wa Mwenyezi Mungu tu, kwani katika uoteshwaji wangu nakumbuka sauti iliniambia tupo watatu na tumetunukiwa roho safi kufanya shuhuli hii ya kutoa tiba. Kwa hiyo naamini hao ni wawili na mimi ni wa tatu na ndio tuliotunukiwa.
Keronyingi - Pole kwa kazi na nashukuru sana
Magreth - Asante, karibu tena.

Mpendwa mdau nataraji kuendelea kukuletea habari toka kwa Magreth Mutalemwa mpaka nitakaporejea jijini Dar. Endelea kufutilia maendeleo ya dada na tiba yake toka urban quarter, Uzunguni,Tabora
DSC05411.JPG
 
Kwa mtindo huu, watanzania tunakazi ngumu huko tuendako. Hivi hawa wote walikuwa wanasubiri Babu wa Loliondo aanze kutibu ndio na wao wajitokeze? Kuna yule aliyejitokeza kule Moshi na yeye sijui ameishia wapi!!! Lakini hapa kuna ujumbe muhimu kwamba serikali imeshindwa kuwapatia watu huduma ya matibabu matokeo yake watu wakisikia tu mahali wanapoweza kupata ahueni, basi wanakimbilia huko. Huwezi kuamini watanzania ni wagonjwa kiasi hiki!!!!

Tiba
 
kuna siku tutanyweshwa sumu nchi nzima

Kuna wale wajapani wanaojenga barabara, mwanzoni walikuwa na ofisi zao Jangwani..KOnoike!!???.wale walisema kama kuna Mungu basi kweli "head quaters" zake zipo Tanzania.

Lakini pia tukae tayari, wenye kampuni za kutengeneza madawa ya binadamu watawatuma serikali zao za france, UK, US waje watushambulie ili wazuie watu kuja TZ kupata hizo "sumu".

We wacha tu... uchumi wa TZ utatoka kwenye nakisi karibuni, tutatoa tiba kwa dunia yote, hela za utalii wa tiba zinakuja, TRA na Hazina na BOT wajipange vyema.
maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana atiii!
 
kuna siku tutanyweshwa sumu nchi nzima

Mkuu.
Serikali imeshindwa kupiga vita maradhi, umasikini...sasa ni vyema wametokea hawa watu wa kutokomeza maradhi!!!
Tujipange kuondoa umasikini sasa.
Hata nguvu kazi ambayo ndio ilikuwa inapotea kwa maradhi sugu sasa inakuwa-replenished!!!
 
...... kila mkoa sasa kutakuwa na mtoa kikombe cha uponyaji, ilianza Arusha, ikaja Mbeya na sasa Tabora.
 
Kuna wale wajapani wanaojenga barabara, mwanzoni walikuwa na ofisi zao Jangwani..KOnoike!!???.wale walisema kama kuna Mungu basi kweli "head quaters" zake zipo Tanzania.

Lakini pia tukae tayari, wenye kampuni za kutengeneza madawa ya binadamu watawatuma serikali zao za france, UK, US waje watushambulie ili wazuie watu kuja TZ kupata hizo "sumu".

We wacha tu... uchumi wa TZ utatoka kwenye nakisi karibuni, tutatoa tiba kwa dunia yote, hela za utalii wa tiba zinakuja, TRA na Hazina na BOT wajipange vyema.
maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana atiii!
Mkuu nimeipenda hii hahahahahahaaaa!!!
 
kuna siku tutanyweshwa sumu nchi nzima

ndiyo hivyo tayari watu wanakunywa. kila mkoa na wilaya na pengine kitongoji na hata kila mtaa utakuwa na kikombe chake. Na serikali inabariki tu.
 
Mwanzo na Mwisho wao utakua ka kampuni ya "dec" ambayo iliacha watanzania wengi waliokua na tamaa, solemba. Sasa hawa cjajua wataachwa kwa style ipi.? Ye2 macho na masikio.
 
Kuna wale wajapani wanaojenga barabara, mwanzoni walikuwa na ofisi zao Jangwani..KOnoike!!???.wale walisema kama kuna Mungu basi kweli "head quaters" zake zipo Tanzania.

Lakini pia tukae tayari, wenye kampuni za kutengeneza madawa ya binadamu watawatuma serikali zao za france, UK, US waje watushambulie ili wazuie watu kuja TZ kupata hizo "sumu".

We wacha tu... uchumi wa TZ utatoka kwenye nakisi karibuni, tutatoa tiba kwa dunia yote, hela za utalii wa tiba zinakuja, TRA na Hazina na BOT wajipange vyema.
maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana atiii!

Kiaina hii imekaa vizuri, sisi wote nasahau kama ipo na shida mingi sana kwa sasa bana. watu nasahau hata bei ya sukari kama ipo juu....Watabibu naokoa serekali hii...kumbe hata serekali yetu yote ilikuwa gonjwa bana....!!! Serekali yote nakimbilia Loliondo duuu...hatari kweli kweli bana.....Sasa Babu naleta maisha Bora kwa kila Mtanzania.....waipe ulinzi kuba sana hii babu amasivyo kama ni kweli ile jamaa ya ulaya na marekani naweza ua babu yetu, ili linda Biashara yao ya dawa
 
kuna mwingine kajitokeza mwanza anaitwa shangazi nimmsikia leo kupita clouds FM anatibu dozi yake vikombe viwili kwa 1000,kazi ipo
 
Hakuna maji yoyote yanayotibu kiukweli katika hao wote hao. kinachotekea ni kuwa watanzania wengi ni wavivu wa kutafakari kabla ya kuchukua hatua. na hili halina cha viongozi wala wasomi. watu wengi hupenda kufuata mkumbo. nas kama kuna mtu haamini ninachosema asubiri aone kuna waota ndoto wengi tu watatokea na watu wataenda kwao kwa maelfu bila hata ushahidi wa hiyo tiba wanayoikimbilia. mimi napata tabu sana kuamini ushuhuda wa mtu kupona kwa kusikia tu maneno yake. kuna vipimo vingi vya kitaalamu kuthibitisha kuwa mtu kapona ugonjwa fulani mbona havifanyiki kwa wanaodai kupona tukaambiwa na tukawaona kwa macho. haiyumkiniki tiba ianze miezi kadhaa iliyopita halafu hadi leo hakuna hata mtu mmoja anayeweza kusimama na kusema wazi kuwa nilikuwa na virusi, nimepiga kikombe cha yeyote kati ya hao, na nimepima tena virusi vimetoweka na cd4 zimerudi kwenye normal range, hakuna!! halafgu hii inayojitokeza sasa ya hata babu mwenyewe kuanza kubadilibadili kauli zake: mwanzoni alisema siku saba tu mtu anapona na virusi vinapotea, akadai usipofuata foleni dawa haiponyi, akadai tena haruhusiwi kuhama samunge! sasa mnaofuatilia kauli zake mbona sasa anabadilika? siyo tena siku saba ameongea muda, kuchakachua foleni sasa ruksa, nadhani msishangae akiamua kuhamia Arusha mjini kesho kutwa. wanaomuiga wamegundua ni fix so na wao wanataka kujipatia kipato na serikali imawalinda, si mmemsikia Pinda na kwenye hii picha mmeona maafande na nyota zao hapo Tabora? Hii nchi imepinda wa watu wake, na viongozi na hata miungu inyowaotesha watu ndoto.
 
Naona hizi sasa ni siku za mwisho ili maandiko yatimie ,napata mashaka

Mke wa Rais (Kikwete?) Isikupeshida wala. Hakuna siku za mwisho walanini. Ni mbinu yakuupotosha umma uache maandamano, Katiba mpya, nk. Ni mambo ya muda. Tusubiri tuone ushenzi huu unapoishia.
 
Back
Top Bottom