Pichani, Daraja Kigamboni hiloo... Kigamboni yakufikirika yawa kweli

Mkuu hapa umenifurahisha sana, naomba tujadili kidogo hoja hii:-


Shule kuliko Rais yeyote wa kabla yake. =

Elimu
elimu_image.jpg

elimu_image.jpg



Serikali kwa kushirikiana na Taasisi, Wakala na Mamlaka za Elimu, Wadau wa Maendeleo, Asasi Zisizo za Kiserikali na Wananchi katika ngazi zote imeendelea kujenga shule, Vyuo na Vyuo Vikuu katika maeneo mbalimbali. Ujenzi huu umewezesha kuongezeka kwa nafasi za masomo.
1. Kuongezeka kwa fursa ya utoaji wa elimu ya awali kwa kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi ina darasa la Elimu ya Awali


  • Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 kwa mwaka 2005 hadi 896, 146 mwaka 2010.(wav 445,867, was 450,279)

2. Kuongezeka kwa ubora wa Elimu


  • Uandikishaji wa Wanafunzi katika shule za msingi umeongezeka kutoka wanafunzi 7,541,208 mwaka 2005 na kufikia 8,441,553 mwaka 2010
  • Uwiano wa mwanafunzi katika darasa umeboreshwa kutoka 1:80 mwaka 2005 na kufikia 1:54 mwaka 2010
  • Uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi umeimarika kutoka 1:7 mwaka 2005 na kufikia 1:3 mwaka 2009.
  • Idadi ya walimu wa shule za Msingi imeongezeka kutoka 151,882 mwaka 2006 hadi 157,185 mwaka 2010.
  • Idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 14,700 mwaka 2006 na kufikia 15,727 mwaka 2009.
  • Kuongezeka kwa uandikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum(walemavu) kutoka wanafunzi 18,982 mwaka 2005 hadiwanafunzi 27,422 mwaka 2009.

3. Idadi ya wanafunzi wanaoendelea na na elimu ya sekondari imeongezeka


  • Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka wanafunzi 493,636 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 999,070 mwaka 2009.
  • Kuongezeka kwa wanafunzi wanaogharamiwa na serikali kutoka katika familia zenye kipato duni na yatima , kutoka wanafunzi 16,345 na kufikia wanafunzi 58,843 mwaka 2009

4. Mafanikio ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari(MMES)


  • yamefanikisha kujengwa na kuongezeka kwa Shule za sekondari za serikali na zilizojengwa kwa nguvu za wananchi kutoka shule 1,745 ( 1,202 za serikali na shule 543 zisizo za serikali) mwaka 2005 hadi shule 4,102 ( 3,283 za Serikali na zisizo za Serikali ni 819) mwaka 2010.
  • Uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Sekondari umeongezeka kutoka wanafunzi 524,325 mwaka 2005 hadi wanafunzi 1,466,402 mwaka 2010.
  • Nyumba 4,087 za walimu zimejengwa kuanzia mwaka 2005 hadi 2009 kupitia MMES.
  • Serikali ya awamu ya nne imefanikiwa kujenga Shule za kata 3,131 katika kata 2,575 mwaka 2005-2010.
  • Vitabu nakala 35,6000 vya masomo ya hisabati na sayansi vimesambazwa katika shule 81 za sekondari katika halmashauri 31 ili kuongeza uelewa wa masomo hayo kwa wanafunzi.
  • Vitabu 266,032 vya Sayansi na vitabu 203,824 vya hisabati kutoka USAID vilisambazwa katika shule za sekondari 1,259

5. Kuongezeka na upanuzi wa Mafunzo ya walimu katika shule za msingi na sekondari ambapo vyuo 16 vimefanyiwa ukarabati


  • Vyuo vya ualimu vimeongezeka kutoka vyuo 32 mwaka 2005 na kufikia 34 mwaka 2009.
  • Idadi ya wanafunzi katika vyuo vya ualimu imeongezeka kutoka 14,00(2005) hadi kufikia wanafunzi 21,846 mwaka 2010.
  • Walimu waliohitimu stashahada wameongezeka kutoka 3,148 mwaka 2005 na kufikia 5,476 mwaka 2009.
  • Walimu waliohitimu Shahada wameongezeka kutoka walimu 2,843 mwaka 2005 na kufikia walimu 5,331 mwaka 2009.
  • Jumla ya wahitimu wote ni 5,985 mwaka 2005 walimu 10,807 mwaka 2009
  • Jumla ya walimu kwa sasa ni 19,000

6. Mafanikio ya elimu ya Juu ni pamoja na


  • kuongezeka kwa udahili katika vyuo vikuu ambapo udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka wanafunzi 40,993 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 111,078 mwaka 2010.
  • Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo vikuu 31, 2010.
  • Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kuna wanafunzi 17,282.
  • Kumekuwepo na Ongezeko la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka wanafunzi 42,729( sh. 62.5) mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 58,841 ( Sh. 140 bilioni) mwaka 2009.
  • Programu za vyuo vikuu zimepanuka na kuboreshwa ambapo vyuo vikuu vya Sokoine, Mzumbe na Dodoma vinatoa shahada ya Elimu.

7. Kuongezeka kwa upanuzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi


  • kuongezeka kwa nafasi za mafunzo kutoka wanafunzi 78,586 mwaka 2005, hadi kufikia wanafunzi 125,359 mwaka 2009.
  • Ujenzi wa vyuo 10 vya ufundi umekamilika katika mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro,Mtwara, Pwani, Dar es salaam, Manyara na Kagera(karagwe).

8. Kuongeza fursa ya upatikanaji wa Elimu ya Watu wazima


  • Walimu 940 na Maafisa Elimu watu Wazima487 wa Halmashauri zote nchini wamepatiwa mafunzo kuhusu uanzishwajio wan a uendeshaji wa vituo na vikundi vya MUKEJA
  • Moduli 2,280 za MUKEJA zilichapwa na kusambazwa
  • Wanafunzi 7,290 wa Mpango Elimu ya Msingi kwa Walioikosa( MEMKWA) walimaliza Elimu ya Msingi na kati yao wanafunzi 2,363 walichaguliwa kuendelea na Elimu ya Sekondari

pamoja_elimu.jpg


Sema, nionyeshe aliyefanya nusu tu ya hayo.
 
Elimu

  • Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 kwa mwaka 2005 hadi 896, 146 mwaka 2010.(wav 445,867, was 450,279)

2. Kuongezeka kwa ubora wa Elimu


  • Uandikishaji wa Wanafunzi katika shule za msingi umeongezeka kutoka wanafunzi 7,541,208 mwaka 2005 na kufikia 8,441,553 mwaka 2010
  • Uwiano wa mwanafunzi katika darasa umeboreshwa kutoka 1:80 mwaka 2005 na kufikia 1:54 mwaka 2010
  • Uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi umeimarika kutoka 1:7 mwaka 2005 na kufikia 1:3 mwaka 2009.
  • Idadi ya walimu wa shule za Msingi imeongezeka kutoka 151,882 mwaka 2006 hadi 157,185 mwaka 2010.
  • Idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 14,700 mwaka 2006 na kufikia 15,727 mwaka 2009.
  • Kuongezeka kwa uandikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum(walemavu) kutoka wanafunzi 18,982 mwaka 2005 hadiwanafunzi 27,422 mwaka 2009.
QUOTE]


[MENTION]zomba [/MENTION]Mkuu umechambua vizuri,

Naomba tueleze je hii siyo nchi ya Kikwete pia???
===========================================================================================================
WANAFUNZI wa shule tatu za msingi zaidi ya 500 katika kata ya Rwinga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasomea kwenye madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi.

Uchunguzi uliofanywa katika shule tatu kati ya saba zilizopo kwenye kata hiyo ambayo ipo mjini Namtumbo umebaini kuwa katika shule ya msingi Rwinga wanafunzi 296 wanasomea kwenye vibanda vya miti vilivyoezekwa kwa nyasi .
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Onesmo Mbawala alisema idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo wanasomea katika vibanda vya nyasi kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu wa vyumba 12 vya kusomea ambapo vyumba vilivyopo ni vinne tu na kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 ina jumla ya wanafunzi 592.



Wanafunzi wa darasa la awali wapatao 92 shule ya msingi Rwinga wilayani Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao

Katika shule ya msingi Selous jumla ya wanafunzi 108 wa madarasa ya tano na sita wanasoma kwenye vibanda vya nyasi hali ambayo walimu wanasema inachangia kushusha taaluma kwa wanafunzi.



Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Selous wilayani Namtumbo wakiwa darasani

Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Sheweji Simba alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 ina jumla ya wanafunzi 477 huku ikiwa na vyumba vinne tu vya madarasa kati ya mahitaji ya vyumba nane hali ambayo imesababisha baadhi ya wanafunzi kusomea kwenye vibanda vya nyasi .

Katika shule ya msingi Mkapa ambayo imepewa jina la aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi Rais mstaafu Benjamin Mkapa pia kuna wanafunzi wanaosomea kwenye vibanda viwili vya nyasi kwa kuwa shule hiyo ina vyumba vinne tu kati ya mahitaji ya vyumba nane.



Wanafunzi wa shule ya msingi Mkapa wilayani Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao

Mkuu wa shule hiyo Hans Mwailima alisema shule hiyo yenye wanafunzi 306 madarasa matatu yanasomea katika chumba kimoja ambapo kuanzia darasa la tatu hadi la sita wanasomea kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu.

“Unajua wanafunzi wana tabia ya kutaniana hivyo endapo darasa moja wakisoma kwenye vibanda vya nyasi kila siku wenzao wanawatania hivyo kukata tamaa na wengine kuwa watoro hivyo tumeamua wote wawe wanasoma kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu ili kujenga mvuto wa mazingira ya kusomea’’, alisema.

Mratibu elimu kata ya Rwinga Thomas Komba amekiri shule tatu kati ya saba katika kata yake ambazo ni Rwinga, Mkapa na Selous wanafunzi kusomea katika vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi na kusisitiza kuwa shule za Minazini, Kidagulo, Migelegele na Mandepwende ndizo shule pekee katika kata hiyo ambazo hazina vyumba vya madarasa vilivyoezekwa kwa nyasi.

“Shule zangu tatu za Rwinga,Mkapa na Selous katika kata yangu zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali ni mbaya tunafanya jitihada za kuhamasisha jamii ili waweze kujitolea kufyatua tofali kuzichoma kwa kushirikiana na serikali ili kupata vyumba zaidi na kumaliza kero hii ya aibu’’, alisisitiza.

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kasimu Ntara alidai kuwa kuwa kuwepo kwa madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi katika wilaya hiyo kunatokana na kuanzishwa shule nyingi za msingi.

“Mpango wa uboreshaji wa elimu ya msingi MEM nchini ulisababisha kuanzishwa kwa shule nyingi hivyo baada ya kuondoka kwa MMEM serikali imeshindwa kumudu ujenzi wa vyumba vya madarasa jitihada zinaendelea kufanyika kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa’’, alisisitiza.

Habari hii imeandikwa na Albano Midelo, FikraPevu – Ruvuma

Ruvuma: Wanafunzi zaidi ya 500 wanasomea katika vibanda vya nyasi, 5.0 out of 5 based on 1 rating
VN:F [1.9.20_1166]
please wait...
Rating: 5.0/5 (1 vote cast)
42 Responses to “Ruvuma: Wanafunzi zaidi ya 500 wanasomea katika vibanda vya nyasi”
Geofrey says:
11/05/2012 at 9:23 am
Miaka hamsini ua Uhuru sherehe ilikuwa ya nini sasa. Mijihela yote ile bado…….hali iko hivi. Nchi hii haifai.
=========================================================================================================

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hayo ndiyo mambo ya Serikali ya chama chetu. Tupeni miaka mitano ijayo tena, muone mambo yetu!!!!
 
Hayo ndiyo mambo ya Serikali ya chama chetu. Tupeni miaka mitano ijayo tena, muone mambo yetu!!!!

Kabla ya Kikwete walikuwa wangapi wanaosoma namna hiyo? ukipata jibu lake utajuwa Kikwete kafanya nini.
 
Hayo ndiyo mambo ya Serikali ya chama chetu. Tupeni miaka mitano ijayo tena, muone mambo yetu!!!!

Hamjapewa tunaona mnavyokopeshana fedha zetu kwenye chama. Hamjapewa tunaona mnvyojipangia safari za kwenda kujifunza usafi, hamjapewa tunaona mnavyopeana viti maalum vya ubunge kwa ukoo, hamjapewa madaraka tunaona mnavyopokea fedha za CDU halafu manjidai kuchakuwa si ufadhili. Eti si ufadhili ni msaada. Hata haiingii akilini.
 
Hamjapewa tunaona mnavyokopeshana fedha zetu kwenye chama. Hamjapewa tunaona mnvyojipangia safari za kwenda kujifunza usafi, hamjapewa tunaona mnavyopeana viti maalum vya ubunge kwa ukoo, hamjapewa madaraka tunaona mnavyopokea fedha za CDU halafu manjidai kuchakuwa si ufadhili. Eti si ufadhili ni msaada. Hata haiingii akilini.

Malaria Sugu na FaizaFox ndio hawa wanaohaha hapa siku hizi?
 
Mkikosa hoja mnaanza viroja.

znz%20fujo.jpg


Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), akiwa amemshikilia mmoja wa wananchi kwa madai ya kuleta vurugu wakati wa upigaji kura Jimbo la Bububu, Zanzibar jana huku naye akiwaonyesha watu wengine

Hivi vurugu hizi katika uchaguzi huko Zanzibar zilisababishwa na Chadema?
 
Hahahahahahah yaani hicho ndo kidaraja kinachopigiwa kelele miaka na miaka ati hata wengine wanthubutu kusema Hongera kikwete rekodi ingine hiyo,hizo rekoni nyingine za mwanzo ni zipi au ndo kuchafua nchi kwa udini,vifo vilivyosababishwa na police chini ya utawala wake,wizi wa EPA,Meremeta,Richmond,kagoda nk hizi ndo rekodi za KIKWETE na wengi hawatamsahau kwa wizi kama huu na yeye akiwa mmoja wa wezi hao.
 
Hahahahahahah yaani hicho ndo kidaraja kinachopigiwa kelele miaka na miaka ati hata wengine wanthubutu kusema Hongera kikwete rekodi ingine hiyo,hizo rekoni nyingine za mwanzo ni zipi au ndo kuchafua nchi kwa udini,vifo vilivyosababishwa na police chini ya utawala wake,wizi wa EPA,Meremeta,Richmond,kagoda nk hizi ndo rekodi za KIKWETE na wengi hawatamsahau kwa wizi kama huu na yeye akiwa mmoja wa wezi hao.

Halafu bumu la walificha pesa huko Uswiss limeshaanza kulipuka na wahusika wanajulikana, sasa hapa watajirereaje wakati wengi wao ndio viongozi wajuu serikalini wakiwemo wa sasa na wastaafu? Siku ya kufa nyani miti yote huteleza.

Sijajua bado safari ya Zitto Kabwe kuandamana na Kikwete kwenda Ethiopia, kuna maswali mengi ya kujiuliza.
 
Huyu Zitto Kabwe nae saa zingine haeleweki kivile ati yaani huyu jamaa sifahamu ana ajenda gani na hawa jamaa wa Magamba wateka nyara wezi,aisee niko na sha sana na huyu jamaaa lakini hakuna marefu yasiyokuwa na ncha pia wanasema vitu vyote vilivyojificha kwa giza ipo siku vitamulikwa.
 
Huyu Zitto Kabwe nae saa zingine haeleweki kivile ati yaani huyu jamaa sifahamu ana ajenda gani na hawa jamaa wa Magamba wateka nyara wezi,aisee niko na sha sana na huyu jamaaa lakini hakuna marefu yasiyokuwa na ncha pia wanasema vitu vyote vilivyojificha kwa giza ipo siku vitamulikwa.

Jaribu kupekuapekua watu ambao waliona list ya walioficha pesa Uswiss ambayo baada ya kuwekwa hapa iliondolewa himahima. katika list hiyo utashangaa usiamini kama kweli wanaotoka kifua mbele waje kutumbukia ndani ya kashfa hiyo.
 
aisee hapa mimi sielewi kitu, kwa hiyo hako ndio katakuwa kanafunguka wakati meli zikitaka kupita? maana picha tulizomezeshwa kabra haziendani na mjengo
 
Nakuomba, tujadili hapa. Ni yepi yanayokufanya useme hayo?

Shule kuliko Rais yeyote wa kabla yake.

Vyuo vikuu, ...

Uchumi...

Demokrasia...

Afya...

Utawala bora...

Kilimo...


Nini zaidi? tujadili.

Yanajadilika...anzisha thread upewe nondo......Mie nitaanza na inflation tuone purchasing power ya shilingi ilivyopelekwa arijojo na dhaifu.
 
aisee hapa mimi sielewi kitu, kwa hiyo hako ndio katakuwa kanafunguka wakati meli zikitaka kupita? maana picha tulizomezeshwa kabra haziendani na mjengo

Hapana, hii haijakatiza njia ya meli wala kupita sehemu ya kuegesha meli, inajengwa huku juu kabisa ambayo itakuja kutokeza Vijibweni badala ya Kigamboni. Bandari na njia ya kupitia meli kuingia na kutoka badarini havijaguswa.
 
Mimi ni mmojawapo ambaye sikupenda kupata kiwanja cha kujenga Kigamboni sababu ya tatizo la kusubiria ferry. Leo ninapoona hili daraja naanza kubadili mtazamo wa kuona Kigamboni si kisiwani tena. Mwenye kiwanja cha Ekari moja mpaka mbili nipm, niko tayari kwa gharama yo yote kwani sasa naona Kigamboni yawa kama :A S 465:Long Island beach ya NY.:A S 465:

Hapo kwenye red... bila shaka wewe ni fisadi...
 
unasifia huku unaomba msamaha miradi kama hii mara nyingi huwa na matokeo mabaya kwa raia je kama ni kweli linajengwa halafu litahitaji kumlipa mwekezaji kwa kipindi kirefu tija itakuwa wapi?halafu kutumia hela za nssf bila matakwa ya wenye hela yao si sahihi sifa lazima ziwe stahiki.

NSSF hawahitaji kupata ruhusa ya wanachama wake kwenye matumizi ya pesa zao,sheria iliyounda NSSF imeipa mamlaka ya kuwekeza michango ya wanachama wake kwenye miradi mbalimbali.,so kama mtu hataki pesa yake itumike angesoma kwanza sheria ya NSSF au angeuliza vizuri kabla hajaamua kujiunga nao.
 
Back
Top Bottom