Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Busara ya nini wakati washaambiwa miezi kibao imepita sasa hivi. Busara hiyo hiyo ingetumika MBEZI tungepata barabara nzuri??

Acheni ujuaji wa kifala nyie.
Ishu ya barabara iko known kwa wengi. Mbezi siku nyingi watu waliarifiwa na kupewa mipunga wasepe. Sio kitu cha kurupukurupu kama hapo Ngorongoro. Isitoshe kupisha upanuzi wa barabara ni maendeleo ambayo tunayashuhudia kila mara sio jambo geni.

Ila swala lakufukuza watu ili uingize mgeni kwenye eneo la hifadhi awinde kusafirisha nyama na kujenga hotel huo si uungwana kabisa. Huwezi sema unalinda hifadhi kwa kufukuza Mmasai na kuleta Mwarabu ili aje kuvuna wanyama. Huo ni ushenzi tu na ubinafsi wa hali ya juu kwa sababu hata huyo mwarabu ukienda nchini kwake huwezi kumilikishwa ardhi yao kwa wao kufukuzwa ili wewe upewe.
 
Uoga wetu unatuponza sana, siku uoga ukitutoka hawa jama ndio watajua hawajui.
Sio uoga tu ila nchi hii watu wakiandamana full scale hao FFU ni wachumba tu. Hizo hizo silaha zao zinaweza tumika kuwaua wenyewe tu bila kujali. Ngoja wamasai waziokote uone😀!!! Watu wanaweza kurusha hata majabali tu na kuwanyoosha hao wachumba. Kama Hamza tu aliwahenyesha nusu saa nzima wanapambana kupigana nae. Imagine hamza wangekuwa 10 hali ingekuwaje?

CCM imechokwa kwa ushenzi inayowafanyia raia miaka nenda miaka rudi. Watu wanaogopa kuumizwa tu ila kimsingi maandamano yakiruhusiwa bila kutumika mabavu kuwanyamazisha watu kwa risasi CCM lazma ingeachia madaraka tu bila kupenda eventually.
 
Picha za kutisha nini kinatisha hapo mkuu?

Na ni kitu gani kinaonesha kuwa hizo ni picha za wamasai? (Sio wamasai peke yao wanavaa hizo bangili na kujifunika hayo mashuka). Haijulikani zimepigwa wapi, na zimepigwa lini(yawezekana zimepigwa Tanzania, Kenya, nk), sasa hiyo taharuki inatoka wapi kiurahisi namna hiyo?

Kwanini aliyepost picha hizi hakutaka kuonesha sura za wahusika? (Ingesaidia kutrace ni kina nani,wanaishi wapi, na tukio lenyewe).

Anyway, naungana nawe kwenye hilo ombi la kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kulitolea ufafanuzi ili ukweli ujulikane na kama hawa waliojeruhiwa ni wananchi wa Tanzania na wamenyanyaswa,haki itendeke. Kama hizi picha hazihusiani kwa vyovyote na usalama na uhuru wa wananchi wetu basi wanaolenga kutengeneza taharuki kupitia picha hizi wasakwe na wachukuliwe hatua.
Mbona mtoa mada kaorodhesha majina ya majeruhi?
Kasome tena
 
Kuna video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mirindimo mikali ya risasi huko Ngorongoro huku wanananchi wa jamii ya kimasai wakikimbia huku na kule kunusuru maisha yao.

Video hiyo imezua taharuki kubwa mitandaoni kiasi kwamba wengi wa walioiona hiyo video wameshangazwa sana na nguvu kubwa inayotumika dhidi ya wananchi wa jamii ya kimasai

Ifahamike tu kuwa serikali imeonyesha nia ya kuwaondoa Wamasai katika eneo hilo la Ngorongoro kwa vigezo vya uhifadhi. Hata hivyo Wamasai wanapinga vikali suala hilo kwa kusema kuwa, Enzi za Mkoloni walikubali kuachia maeneo yao ya Serengeti ili kuwezesha Serengeti iwe mbuga ya wanyama tupu. Walihamishiwa ngorongoro kwa makubaliano kuwa safari ijayo maslahi ya binadamu yakigongana na maslahi ya watu basi maslahi ya watu yatapewa kipaumbele.
Wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya kwanza serikali ilitunga sheria ya uhifadhi ya Ngorongoro, na sheria hiyo ikasema wazi kuwa mojawapo wa malengo ya mamlaka hiyo ya uhifadhi wa ngorongoro ni kulinda maslahi ya wamasai waishio katika uhifadhi.

Tatizo la migogoro ya Serikali na Wamasai linarudi nyuma toka zama za kashfa ya Loliondo na kuna minong'ono kuwa yule mwarabu aliyepewa eneo la Loliondo anataka apewe eneo kubwa zaidi na hivyo ndo maana Wamasai wanafanyiwa visa wafukuzwe au waondoke wenyewe.

Hili suala ni zito sana, Ikumbukwe kuwa Hayati Magufuli katika utawala wake alikataa kuwafukuza wamasai huko Ngorongoro, lakini serikali hii ya awamu ya Sita naona inatumia kila mbinu kuwaondoa Wamasai katika maeneo yao.

Hapa Chini ni clip ya video ikionyesha Wamasai wakikimbia kunusuru maisha yao dhidi ya bunduki na risasi.

View attachment 2256280
Duuh!
Hatari sana🤔🙄
 
Tatizo la migogoro ya Serikali na Wamasai linarudi nyuma toka zama za kashfa ya Loliondo na kuna minong'ono kuwa yule mwarabu aliyepewa eneo la Loliondo anataka apewe eneo kubwa zaidi na hivyo ndo maana Wamasai wanafanyiwa visa wafukuzwe au waondoke wenyewe.
Kama kuna ukweli katika hili, kwa wananchi wa nchi hii kunyanyaswa na kuuliwa kwa faida ya wageni, bila kujali wageni hao wanatokea wapi na wana ukwasi kiasi gani, serikali ni lazima ilaaniwe. Hiyo itakuwa siyo serikali inayojali raia zake.

Kama ni uwekezaji, kwani kuna uhaba wa maeneo ya uwekezaji katika nchi hii?

Wajibu wa kwanza wa serikali yoyote yenye heshima ni kuweka maisha ya raia zake kuwa juu ya kitu kingine chochote.

Kama ni kweli serikali ya Samia inafanya haya, tena serikali ambayo haikuchaguliwa na wananchi, hii itakuwa ni dosari kubwa itakayoikumba serikali yenyewe.

Kwani katika mambo yaliyokuwemo katika ahadi alizofanya Magufuli, hili la kuwafukuza raia lilikuwemo kwenye ahadi hizo, au Samia kajitungia tu mwenyewe kufurahisha ndugu zake?
 
Hili suala la Ngorongoro lina utata mkubwa sana ambapo hadi sisi wenye akili nyingi tunashindwa tusimamie wapi..🤔. Hapo Ngorongoro kuna makundi manne yanayoleta utata mtupu; wamasai, serikali, mwekezaji wa Loliondo na wanaharakati.

Serikali ina hoja za msingi sana kwanini watu wahame Ngorongoro. Ile hoja ya kulinda wanyama na hifadhi ya Ngorongoro isipotee ni hoja yenye nguvu sana. Kinacholeta utata ni kuaminika kwa serikali kwamba tayari imewajengea nyumba za kuhamia huko Handeni. Je ni kweli? Je, yale makubaliano ya Arusha yalihusisha wamasai wa Ngorongoro kweli au kuna mamluki waliowasemea wenzao wa Ngorongoro?

Wamasai wao hawana hoja zenye nguvu sana za kung'ang'ania kubaki Ngorongoro ila haki za binadamu zinawalinda. Huwezi kuwatoa kama unatoa mifugo porini. Lakini na wao wanafuata sheria za kukaa hifadhini? Tumeona wengine tayari washajenga mijengo ya balaa ndani ya hifadhi kitu ambacho sio sahihi.

Huyu mwekezaji wa Loliondo nae ni kero kubwa kwa wamasai. Ninawalaani wote waliompa hilo eneo kwa mkataba mbaya kuwahi kutokea hapa nchini. Inasemekana yupo nyuma ya huu mgogoro. Wanaharakati walioko against serikali wengi wao sio wazalendo zaidi ya kuwatumia wamasai kupiga hela za mabeberu.
Mkuu, umeandika vyema, lakini mgogoro unaohusisha wananchi ni wajibu wa serikali kuuchukulia kwa uzito mkubwa zaidi kuliko inavyofanya sasa.

Kuamini tu kuwa kwa kuwa wao ni serikali wana haki ya kutumia mabavu siyo sahihi hata kidogo.

Isitoshe, kama kuna uhusiano wowote wa mwekezaji toka nje ya nchi anayesababisha serikali ikose weledi wa kushughulika na matatizo ya wananchi wake, hilo pekee linafanya serikali kuwa na sura mbaya kabisa.

Wajibu wa kwanza kabisa wa serikali ni kulinda maslahi ya wananchi wake kuliko uwekezaji, ambao unaweza kufanyika katika mambo mengine mengi nchi yetu iliyojaliwa kuwa nayo.

Maisha ya wananchi wetu ni muhimu zaidi kuliko uwekezaji wowote ule. Kwani maana ya kuwekeza ni nini, kama si njia tu ya kutafuta kuinua maisha ya wananchi wetu!
 
Kwa jasho na damu Ngorongoro italindwa.
Taka wasitake Maasai wataondoka Ngorongoro hawana faida kule full stop
 
Ishu ya barabara iko known kwa wengi. Mbezi siku nyingi watu waliarifiwa na kupewa mipunga wasepe. Sio kitu cha kurupukurupu kama hapo Ngorongoro. Isitoshe kupisha upanuzi wa barabara ni maendeleo ambayo tunayashuhudia kila mara sio jambo geni.

Ila swala lakufukuza watu ili uingize mgeni kwenye eneo la hifadhi awinde kusafirisha nyama na kujenga hotel huo si uungwana kabisa. Huwezi sema unalinda hifadhi kwa kufukuza Mmasai na kuleta Mwarabu ili aje kuvuna wanyama. Huo ni ushenzi tu na ubinafsi wa hali ya juu kwa sababu hata huyo mwarabu ukienda nchini kwake huwezi kumilikishwa ardhi yao kwa wao kufukuzwa ili wewe upewe.
So what? Kujulikana na wengi ndio sababu ya kuhamishwa au msingi wa mradi husika?

Hoja za kipumbavu unazozitoa.
 
hakuna miradi sehemu nyingine mpaka watu watoke damu?
Kama hujataka kutoka na tayari serikali ishakutengea eneo na mlishaambiwa mtoke nanyi mmekaidi unataka watumie nini??

Unatumia akili au matako kufikiri??

Masai ni nani katika nchi kwamba wao waogopwe kuhamishwa au waibishie serikali kisa wamekaa pale miaka na miaka?? Uhamishaji wa wananchi upo tangia uhuru, wakati wa nyerere watu tulihamishwa kupelekwa katika vijiji vya ujamaa tena kwa lazima.

Hao mbuzi lazima wahame, chocheeni ujinga watavunjwa miguu na hamna kitu mtafanya wajinga ninyi.

Mnaongea kipumbavu sana kwenye vitu vya msingi. Hoja zenu mara ooh waarabu, mara wamekaa muda mrefu NONSENSE.
 
Kama hujataka kutoka na tayari serikali ishakutengea eneo na mlishaambiwa mtoke nanyi mmekaidi unataka watumie nini??

Unatumia akili au matako kufikiri??

Masai ni nani katika nchi kwamba wao waogopwe kuhamishwa au waibishie serikali kisa wamekaa pale miaka na miaka?? Uhamishaji wa wananchi upo tangia uhuru, wakati wa nyerere watu tulihamishwa kupelekwa katika vijiji vya ujamaa tena kwa lazima.

Hao mbuzi lazima wahame, chocheeni ujinga watavunjwa miguu na hamna kitu mtafanya wajinga ninyi.

Mnaongea kipumbavu sana kwenye vitu vya msingi. Hoja zenu mara ooh waarabu, mara wamekaa muda mrefu NONSENSE.

Kumbe ushahamishwa before,,,,,,umekua katili ulionewa so na wengine waonewe tu....

Kwanza Nyerere alikuwa Mzalendo, sio ufisadi wa serikali zilizofuata

Unaandika shit, kwani hakuna mwarabu kweli...???

Na yes wamekaa muda mrefu, at least mlivyohamishwa kwenye Ujamaa ilikuwa kwa manufaa ya watanzania wengine na sio ya mwarabu!

Unaita watanzania wenzio mbuzi?!..sidhani kama uko sawa MKuu..

Mark hii posti, hakuna mmasai atakayeenda Handeni

Na mama ataenda kwa waarabu na kusema kishasanuka...

Kwa heri, LOL
 
Back
Top Bottom