Mavazi sahihi, mahali stahili
msilete kusihi, pasipo stahili
wastaili kuishi, si kwa ubatili
kuvaa kusitiri, si utupu upenuni
kunya anye kuku, kwa bata ni matata
aliyevaa yupo huku, wa mbali unamatata
mazingira si yakushuku, watoto wameyapata
kuvaa kusitiri, si utupu upenuni
kama i kwa ofisi, hapo kuna mashaka
ila kwa binafsi, ya nini kuwa shaka
kila kitu kwa nafasi, msuli nalo shuka
kuvaa kusitiri, si utupu upenuni
acheni unafiki, kusingizia maadili
mavazi ni hakiki, nyie mwayajadili
mazingira stahiki, si huku mjadili
kuvaa kusitiri, si utupu upenuni
tazama mazingira, jinsi yanavutia
vikoi wamevingira, bambataa kufunikia
nini usisubira, uanze kuwabwatia
kuvaa kusitiri, si utupu upenuni