Picha za Viongozi wa Serikali kutawala kwenye mabango ya Warsha za Wadau ni takwa Kisheria au ni kujipendekeza na kujikomba kwa Serikali?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
416
1,051
Wakuu mpo salama? Twende moja kwa moja kwenye mada.

Wakuu, haya mabango mawili ni shughuli mbili tofauti ambapo serikali ilialikwa na wadau kushiriki kwenye shughulii hizi.

Hii ya kwanza ilikuwa ni Siku ya Uhuru wa Vyombo wa Habari Duniani na ya pili ilikuwa ni kuadhmisha Siku ya Kimataifa ya Human Resorces.

Katika warsha zote hizi mbili serikali ni waalikwa tu, yaani tukio ni la wadau 100% lakini ukiangalia mabango haya yanatoa ujumbe tofauti. Ni kama inapiga kelele tukio hilo ni la serikali, lakini pia hata ukifuatilia matukio haya utaona serikali kwa mkono mkubwa ndio imeshikilia tukio hilo.

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lakini bango limejaa picha ya Majaliwa, kwanini? Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwanini anaalikwa Majaliwa kama mgeni Rasmi? Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Kamati ya Kumsifia mama wakiwa wamependeza na Tisheti zao za kumuunga mkono Mama wanahusika vipi na tukio hilo?

Maadhimisho ya Siku ya Rasilimali watu lakini picha ya Nchimbi imejaa kwenye bango lote utafikiri ni maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Nchimbi kwanini? Ukiangalia tu bango paap unakaribishwa na sura ya Nchibi badala ya tukio kwanini? Sura ya Nchimbi ingekuwa ndogo au kutokuwepo kabisa tukio lisingefanyika? Au serikali ingetia figisu tukio lisifanyike?

Je, ni takwa Kisheria mgeni rasmi akiwa kiongozi wa serikali basi lazima sura yake ijae kwenye bango hilo? Je, bila sura ya kiongozi kujaa kwenye bango hilo maoni ya wadau hayatiliwi maanani? Je, kuna uhuru wa kutoa maoni kwenye makongamano hayo?

Au ni kwamba wadau wanajipendekeza kwamba wakiweka sura ya kiongozi ikajaa kwenye bando basi hata jambo lao linalofanyika ndio litafanyiwa kazi haraka?

Narudisha mpira kwenu wadau.

maja.jpg
gx nchi.jpg
 
Kama nakuelewa vile; lakini usisahau hata wewe ungeona vyema bango likkusoma pia tusisahau hawa ni watoto wetu printers wetu pesa inabaki wetu sidhani kama ina athari, utazoea tu hizi nyakati nazo zitapita.
 
Nidhamu za woga na kinafiki zimefikia hatua ya juu sana. Na haya yote ni madhara ya chama kimoja kukaa madarakani kwa muda mrefu bila ridhaa ya umma. Matokeo yake wanatengeneza mazingira ya mapenzi bandia ili upate kitu fulani, na bila kujipendekeza kwa serekali na chama tawala huwezi kupata fadhila.
 
Mabango ya aina hiyo kwenye mikusanyiko hata isiyoihusu Serikali huwa ni kampeni zinazoendeshwa kiujanjaujanja kumnadi kwa wapigakura mtu wanayemtaka kwenye nafasi fulani kwenye uchaguzi unaofuata.

Ni kampeni zinazoanza kabla ya wakati ili anayependekezwa asipotee kwenye ulingo wa siasa.... Hizi siasa za hila wanaziweza sana CCM.
 
Ukielewa nchi yetu vizuri utajua kuna faida nyingi sana kwa wafanyabiashara kuwa mstari wa mbele kushirikiana na chama tawala
Kushirikiana au upande mmoja kuwa na nguvu kupitiliza kuliko mwingine? Kweli hapa kuna ushirikiano wa manufaa au upande mmoja unanyamazishwa?
 
Kama nakuelewa vile; lakini usisahau hata wewe ungeona vyema bango likkusoma pia tusisahau hawa ni watoto wetu printers wetu pesa inabaki wetu sidhani kama ina athari, utazoea tu hizi nyakati nazo zitapita.
Sijaelewa ulichomaanisha Mkuu, kwamba printers wanafaidika na kutangaza wanasiasa kuliko tukio lenyewe?
 
Ibada ya Sanamu

Mungu wa mbinguni Akanena akamwambia Musa " Usijifanyie Sanamu ya kuchonga ukaiabudu"

Hili jambo wengi huwa hawalielewi 🐼
Kwahiyo unasema anayewekwa kwenye bango anakuwa anaabudiwa, jambo linalopeleka na kuashiria yeyey ndio yupo juu kwenye tukio hilo na wengie wapo hapo kumtukuza?
 
Nidhamu za woga na kinafiki zimefikia hatua ya juu sana. Na haya yote ni madhara ya chama kimoja kukaa madarakani kwa muda mrefu bila ridhaa ya umma. Matokeo yake wanatengeneza mazingira ya mapenzi bandia ili upate kitu fulani, na bila kujipendekeza kwa serekali na chama tawala huwezi kupata fadhila.
Kama ni hivi ina maana wadau (asilimia kubwa) ni CCM B, hakuna tena kutetea maslahi ya umma, bali kile kitakachowafurahisha watawala na kufanya mambo yao yaende?!
 
Mabango ya aina hiyo kwenye mikusanyiko hata isiyoihusu Serikali huwa ni kampeni zinazoendeshwa kiujanjaujanja kumnadi kwa wapigakura mtu wanayemtaka kwenye nafasi fulani kwenye uchaguzi unaofuata.
Ni kampeni zinazoanza kabla ya wakati ili anayependekezwa asipotee kwenye ulingo wa siasa.... Hizi siasa za hila wanaziweza sana CCM.
Hii inamaanisha waliondaa shughuli hiyo nao ni upande B wa kiongozi husika?
 
Na picha za raisi aliye madarakani na Nyerere kwenye ofisi za watu binafsi ni takwa la kisheria?
 
Back
Top Bottom