Picha ya siku: Maisha lazima yaende kama kawaida,tazama wana Ukara

Kajole

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,667
1,642
Wakichota maji ziwani kwaajili ya matumizi majumbani jirani na eneo ilipotokea ajari ya kivuko cha MV Nyerere ( picha na mwananchi/fb page)
FB_IMG_15377754202670677.jpg
 
nauliza tu hivi wanaukara kweli wamesambaziwa maji salama majumbani?
 
Huu uzembe wa kushindwa kujifunza kuogelea utatucost sana, mzigo umezama Kariba kabisa na upwa ila wanyamwezi kibao wamerudisha namba kwa God kwa kushindwa kutanua kwapa na kufika upwa. Daaah!
Kuogelea Umbali mrefu ulee aisee usichukuliee poaaa kabisaa!! Yangekukuta usingewaza huo ujingaa
 
Mimi natoka mapema sana kwa ule umbali wa meli ilipozamia! Nimeiva sana kwenye mambizi mkuu. Sema ndio hivyo siku ya kuondoka ikifika imefika tu.

Inategemea upo kona ipi? Kumbuka katika hali kama hiyo watu ukimbilia kuwakumbatia wenzao hasa wakigundua kuwa unaweza kuogelea.

Miaka ya nyuma sana nikiwa shule ya msingi, nilipanda daladala tulipofika BOMANI pale Ilala kulitokea kitu kama moshi hivi, Mimi nilikuwa mlangoni lkn sikuweza kutoka maana watu walianza kuvutana ili kutoka mle ndani ilikuwa patashika nguo kuchanika mkuu
 
Ndugu hujui usemalo, ikitokea ukiwapo probability ya wewe ku - survive ni ndogo sana hata kma unajua kuogelea weee acha tu!
Ukiwa fit kuogelea hapo ni karibu mno.
Hizi kozi zipo zinafundishwa ni kama kozi ya self defence tu.
Ni vema mkazi wa maeneo ya bahari, ziwa mito ujifunze haya:
1.kuogelea,
2. kuokoa maisha ya mtu aliyezama (life saving),
3.kuelea (flooting)na
4.kuzamia (diving).
Itakusaidia sana kwenye dharura kama hizi.
 
Walibanwa na kushindwa kutoka , wengi waliookoka ni waliojirusha majini.
Huu uzembe wa kushindwa kujifunza kuogelea utatucost sana, mzigo umezama Kariba kabisa na upwa ila wanyamwezi kibao wamerudisha namba kwa God kwa kushindwa kutanua kwapa na kufika upwa. Daaah!
 
Huu uzembe wa kushindwa kujifunza kuogelea utatucost sana, mzigo umezama Kariba kabisa na upwa ila wanyamwezi kibao wamerudisha namba kwa God kwa kushindwa kutanua kwapa na kufika upwa. Daaah!
Hapana mkuu,taharuki,kushikwa na wasiojiweza,kugandamizwa na mizigo na wale waliokua deck la chini kukosa muda wa kutosha kuwahi kujiokoa. Inatajwa kuwa meli ilipinduka na kuzama ghafla,kwa hiyo hakukua na muda wa kutosha kujiandaa kwa walio wengi kujiokoa.
 
Back
Top Bottom