Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Sasa nani kaendesha kikao cha baraza la mawaziri huiyo jana na cha halmashauri kuu Taifa?
Ikiwa mzee alikuwa na birth day?
 
Hapo Makonda anahusikaje? Maana aliyetoa maelekezo ni Baba Keagan na si Makonda. Hapo ni watu tofauti; mmoja ana mamlaka mwingine hana. Ningekuwa mimi ningepuuza maelekezo ya Baba Keagan.
Unachokitafuta huwezi pata kwani umechelewa...hivi unashinda kesi kweli wewe?
 
Umefika muda ukiwa nchi za watu unaona aibu kujisema wewe ni Mtanzania....

So Sad.

Wapi huko. Mkuu. Acha mbwembwe. Tupo huku na nikwambie nchi yangu kwanza. Hakuna wazazi wanaobaka watoto wao kama wazungu lakini hutaskia mpaka Uwe kwenye Circle fulani. So be proud of your country Hakuna chochote cha Ajabu Tz.
 
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Telegram, kwa jina la Baba_Keagan amepakia ujumbe unaosema ''Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako''
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mchekeshaji Idris Sultan alipakia picha mbili za Rais Magufuli ambazo zimehaririwa na kuandika maneno haya "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani''

Ikumbukwe jana ilikuwa ni siku ya kusherekea mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Rais Magufuli na watu, taasisi na mashirika mbalimbali ya walituma salamu za siku ya kuzaliwa.

Kuna wengine walienda mbali mpaka kutengeneza video za utani, mfano Mchungaji muhuni, Masanja Mkandamizaji alipakia video ikimuonesha akiimwagia maji picha rasmi ya Rais Magufuli inayotumiwa kwenye ofisi,taasisi na mashirika mbalimbali kwa mujibu wa sheria.



======

UPDATES

Baada ya mchekeshaji Idris Sultan kutakiwa ajisalimishe Polisi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema yupo Tayari kumuwekea Mwanasheria wa kumtetea na kumdhamini Msanii huyo.

Ameyasema hayo kwenye Ukurasa wake wa Twitter. "Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo". Amesema Kigwangalla.

Kuna muda makonda pamoja hana elimu anavyeti vya Ku connect hua nampenda kwauchapaji kazi nakunikumbusha tena taaluma maranyingi haimsaidii MTU kua kiongozi(elimu)......kunamuda tena hua ananichafulia mbeleyangu hali yahewa......hapo shida ikowapi...Je kipanya anavochoraga katuni zamagufuli vile hua haoni.
 
Hivi tuseme Baba Kegan ni Makonda na in sawa kapotea step kutoa amri kwa kutumia mtandao wake na mkewe wa Insta.
Tuache hilo,jee mamlaka ya RC Dar yapo hadi mtandaoni? Idrisa anaweza kuwa sawa anaishi Dar lakini amepost utani huo (ambalo sio kosa yeye in comedian) akiwa nje ya Dar au hata ya nchi hapo vipi?
Makonda acha kujipendekeza kupita kipimo ni ujinga, hata mkeo naye aweza kuwa mjinga pia maana hawezi kukushauri kuwa wakati mwingi unafanya ujinga sana.
Haya sasa pambana na Kigwangwala mpenda sifa mwenzio lakini aliyekuona umjinga.
 
Said Nassoro Bagaile na Daudi Albert Bashit
EIEXFwVWoAEEgWv.jpeg
 
Back
Top Bottom