Picha - Traffic Polisi wakipokea Rushwa hadharani

Njele

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
275
121
rushwa.JPG

Traffic waliopo barabara kuu eneo la Bwawani Chalince-Morogoro wakipokea rushwa. Raia mwema aliyesafiri na kuwanasa hawa traffic wakipokea rushwa alikaa kwa muda katika eneo hili na kuwapiga picha. Vijana walioandaliwa wakijishughulisha kama wanasafisha gari ili kuwa kizingizio huku wao wakiendelea na zoezi la kukabidhiana rushwa. Askari hao baada ya kubaini mdau huyo amewapiga picha walimfuata ndani ya bus alilokuwemo na kuanza kupambana naye lakini mpiga picha aliwazidi ujanja na kuwashinda. Kairusha picha hii kupitia mdandao wa Michuzi.
 
Duh, mchana kweupeee chini ya mwembe, halafu gari wamelipaki kuelekea brabarani kila mpita njia anapata taswiras bomba kabisa. Nampongeza sanautundu wa aliyechukua taswira hii, kumbe mambo bado kabisaa?
 
Sasa wale nini na maisha magumu kama mawe?
Kwa namna maisha yalivyo ghali watu wenye kipato kinachoweza kuitwa cha chini lazima wafanye mipango mingine ili kutosheleza mahitaji ya familia. Inasikitisha ila hiyo ndio hali halisi. . .
 
Acha kuhalalisha rushwa bibie
 
Utrafic bila kipima mwendo sio kamili. I hate kale kadude kweli
 
Sasa wale nini na maisha magumu kama mawe?
Kwa namna maisha yalivyo ghali watu wenye kipato kinachoweza kuitwa cha chini lazima wafanye mipango mingine ili kutosheleza mahitaji ya familia. Inasikitisha ila hiyo ndio hali halisi. . .

Kama wanajua maisha ni magumu waache kuishabikia Serikali na kuwapiga wananchi kwa marungu pale wanaposhinikiza kupatiwa haki zao
 
Utrafic bila kipima mwendo sio kamili. I hate kale kadude kweli

Serikali inataka kupambana na rushwa?..wangeanza kwanza na kuondoa hicho kidude chao kinachosaidia Traffic kuchukua pesa za watu kwa unyang'anyi! Kisha wawanyang'anye hayo magari wanayowapa na kuwawekea petroli ili wakakimbize rushwa vizuri.Tatu wawakague traffik kama hawajawakuta na vitabu bandia vya notification!
 
Duh, mchana kweupeee chini ya mwembe, halafu gari wamelipaki kuelekea brabarani kila mpita njia anapata taswiras bomba kabisa. Nampongeza sanautundu wa aliyechukua taswira hii, kumbe mambo bado kabisaa?

Wakati ndo mabichi kabisa! Huku moshi ndo kwanza utadhani serikali imewaambia wakajitaftie mishahara humu barabarani
 
Kwa picha hiyo hakuna kitendo chochote kinachoonyesha transfer ya cash au kitu chochote cha aina ya rushwa kati ya traffic na hao raia!
Mleta mada umejuaje kuwa rushwa ilitolewa hapo?...au unahisi tu kutokana na default value juu ya tabia ya hawa ndugu?
Ni rushwa gani inatolewa mbele ya kundi la watu namna hiyo?

Halafu kwani traffic police hawana ndugu na jamaa zao wanaoweza kuongea nao kama hivyo pichani?
Mi naona ni shughuli za kawaida tu zinaendelea hapo, kuna kijana anaosha gari, wengine wanachati tu na maafisa hao, lakini hakina m'badilishano wowote wa pesa hapo!

Mleta mada alitakiwa apige na picha labda inayoonyesha gari fulani imepaki kwa kukamatwa, hapo ndipo ingeleta ushawishi wa kuamini kuwa madereva wake ndiyo wanamsaundisha traffic, lakini kwa mazingira hayo. hakuna dalili hizo!
 
mahakama ikihusishwa hapo watashinda kesi'sioni hela anayokabidhiwa

Ndo maana wanawatumia hao vijana huu mtindo upo pia hapo himo njia yakuelekea boda ya hapo himo ni nouma yani hapo kila gari inayopita ukitaka isikaguliwe unaacha buku olewako ukute una elfu5 au 10 ukimpa usitegemee chenji utasikia nashukuru sana walao hii nyingine tupatenayo chai
 
rushwa.JPG

Traffic waliopo barabara kuu eneo la Bwawani Chalince-Morogoro wakipokea rushwa. Raia mwema aliyesafiri na kuwanasa hawa traffic wakipokea rushwa alikaa kwa muda katika eneo hili na kuwapiga picha. Vijana walioandaliwa wakijishughulisha kama wanasafisha gari ili kuwa kizingizio huku wao wakiendelea na zoezi la kukabidhiana rushwa. Askari hao baada ya kubaini mdau huyo amewapiga picha walimfuata ndani ya bus alilokuwemo na kuanza kupambana naye lakini mpiga picha aliwazidi ujanja na kuwashinda. Kairusha picha hii kupitia mdandao wa Michuzi.

Kila mtu anakula ofisini kwake. wabunge wanajipitishia posho kubwa, hawa hawana mahali pa kupata posho. Posho yao ni hiyo!!!! ni sahihi kabisa. Songa mbele polisi kula rushwa kwa kwenda mbele!!!!!
 
Serikali inataka kupambana na rushwa?..wangeanza kwanza na kuondoa hicho kidude chao kinachosaidia Traffic kuchukua pesa za watu kwa unyang'anyi! Kisha wawanyang'anye hayo magari wanayowapa na kuwawekea petroli ili wakakimbize rushwa vizuri.Tatu wawakague traffik kama hawajawakuta na vitabu bandia vya notification!

Mkuu huku kwetu kuna vipikipiki wamepewa yani kuanzia asubuhi mpaka jioni ni misele yakufukuzia rushwa tu inayopitia huku mipakani na shm nyingine
 
mbona ni kawaida hao kukaa hayo maeneo na kuvuta kitu kidogo
 
Na mimi naangalia utaratibu utakaoweza kunipatia kitu kidogo kwenye haka ka ofisi ka muhindi ili angalau niende sambamba na posho za bi kiroboto. Ingawa najua siwezi fikia hata robo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom