Kwa picha hiyo hakuna kitendo chochote kinachoonyesha transfer ya cash au kitu chochote cha aina ya rushwa kati ya traffic na hao raia! Mleta mada umejuaje kuwa rushwa ilitolewa hapo?...au unahisi tu kutokana na default value juu ya tabia ya hawa ndugu? Ni rushwa gani inatolewa mbele ya kundi la watu namna hiyo? Halafu kwani traffic police hawana ndugu na jamaa zao wanaoweza kuongea nao kama hivyo pichani? Mi naona ni shughuli za kawaida tu zinaendelea hapo, kuna kijana anaosha gari, wengine wanachati tu na maafisa hao, lakini hakina m'badilishano wowote wa pesa hapo! Mleta mada alitakiwa apige na picha labda inayoonyesha gari fulani imepaki kwa kukamatwa, hapo ndipo ingeleta ushawishi wa kuamini kuwa madereva wake ndiyo wanamsaundisha traffic, lakini kwa mazingira hayo. hakuna dalili hizo!