Traffic polisi wakataa rushwa ya tsh. Milioni 7

kandidus

Member
Feb 6, 2012
70
17
Haya wanajamii!
Inanishangaza kusikia kwamba walewale askari wa usalama barabarani waliosemekana kubuni mbinu mpya ya kupokea rushwa kwa mtindo wa kutega gari likiwa linaoshwa kama iilivyopigwa picha na mtaalam wetu (njele) wiki tatu zilizopita, traffic hao hao wameonekana tena laivu wakikataa kitita cha pesa shilingi milioni 7 za kitanzania walizokuwa wanashawishiwa kupewa na dereva mmoja aliyekamatwa na maelfu ya kilo za nyara za serikali (pembe za ndovu) juzi tarehe 08/02/2012 eneo hilo hilo la maseyu mikese morogoro. Pembe za ndovu hizo zilikuwa katika gari aina ya land cruiser iliyowekwa namba za DFP. Sasa WATANZANIA WENZANGU TUJIULIZE akiwemo mtoa mada iliyopita (NJELE), juu ya VITA DHIDI YA RUSHWA kuwa askari hao wa usalama barabarani kama kweli huchukua rushwa, wangeziacha mamilioni hayo ya pesa ambazo dereva alikuwa akizitoa tena kwa siri ili ajinasue na tatizo alilokamatwa nalo? Watanzania mnasemaje?
Na Kandidus
 
picha nimeiona kwa michuzi ..hawa wanaosha juzi kamanda wao alituma bandiko kwa michuzi akikanusha kuhusu ile Picha ..
 
May be dereva alitiliwa mashaka au palikuwa ni mahali pa wazi na hivyo kuona kibarua kingeweza kuota majani maana haiingii akilini kuwa walikataa kitita hicho!
 
May be dereva alitiliwa mashaka au palikuwa ni mahali pa wazi na hivyo kuona kibarua kingeweza kuota majani maana haiingii akilini kuwa walikataa kitita hicho!

Yawezekana wamezoea kuchukua kidogo! Kiasi kilichokuwa offered na dereva kikawastua..,,,,,Nafikiria nikisema; samahani!
 
Ndug. polis nao ni wajanja, wanapohs mashaka kwenye Issue wanayo deal nayo huenda kuna mkono wa uongoz wa juu hata kama ni M.100 wataitema.
 
Ndug. polis nao ni wajanja, wanapohs mashaka kwenye Issue wanayo deal nayo huenda kuna mkono wa uongoz wa juu hata kama ni M.100 wataitema.

Si hivyo tu, Je kulikuwa na uwiano wa hiyo rushwa na thamani ya mzigo? Polisi siyo wajinga kihivyo, ikizingatiwa kwamba ma deal kama haya hayafanywi na vidagaa kama sisi. haya ni madeal ya mijitu huko juu.
 
kwa mazingira ya hilo tukio inaonekana walishapewa taarifa kuwa kuna hilo gari lenye huo mzigo walikamate, isingekuwa rahisi kwao kukubali mlungula
 
Pia inawezekana mtoa mada ni mojawao hivyo anataka kuwasafisha kwamba hata ile ya juzi walisingiziwa
 
i bet mtoa mada ana hidden agenda kwenye ishu hii,je aweza kututhibitishia ni kweli hao trafic walipewa ofa ya m7?thubutuu,bongo hii?
 
Utakuwa woga tu...
Na Kandidus ulipataje taarifa hiyo? Ni kupitia waliokuwa kwenye DFP au hao Askari?
 
mtoa mada hilo lazima lilikuwa dila na wakalishtukia mapema ndo maana wamekataa
 
hawana lolote, wanajikosha kwa jamii ionekane si jadi yao kuchukua rushwa.
 
Back
Top Bottom