Picha - Traffic Polisi wakipokea Rushwa hadharani

Picha - Traffic Polisi wakipokea Rushwa hadharani

Watanzania wenzangu,
Kimsingi fikirini kwanza kabla hamjatoa mada katika jamii forum ili tuzijadili. Jeshi la Polisi Tanzania kupitia kikosi cha Usalama Barabarani linapaswa kupongezwa kabisa. Mtoa mada uliyepiga picha hii, ebu tafuta takwimu za ajali kwa miaka miwili tu ilyopita, utakuja kukiri kuwa kwa miaka miwili iliyopita katika barabara ya dsm-morogoro - iringa kulikuwa na ajali nyingi zilizosababisha vifo vya watanzania wengi, na wengine kubaki kuwa tegemezi baada ya kukatwa viungo vyao vya mwili. Hii ni kwa sababu magari hayo uliyoyapiga picha hayakuwa yanafanya kazi barabarani kuthibiti wavunja sheria za barabara hususani mwendo kasi ambao siku zote umekuwa chanzo cha ajali zilizowaua watanzania ambao ndo nguvu kazi ya taifa letu.

Kutokana na sababu hiyo basi, Kwa mwaka huu 2012 kamanda Mpinga amekuja kivingine kwa kushirikiana na wakuu wa vikosi vya Usalama Barabarani wameweka mikakati ya kuongeza vithibiti mwendo na magari ya high-way patrol ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuthibiti ajali za barabara kuu kama sio kuzuia kabisa. Kutokana na ukweli huu basi, kwa madereva na wananchi wasiotii na kujua athari za ajali mf. aliyetoa mada hii, hawatambua hata kidogo utendaji wa trafic wakiwa barabarani. Kwa ujumla picha hii haina uhusiano hata kidogo na mazingira ya rushwa. Kwani gari la polisi katika picha hii hapo juu linaonekana limepaki barabarani inawezekana ikawa kwa sababu mbalimbali: 1. wameharibikiwa 2.kunataarifa wanaisubiri, 3. wanangoja msafara maana ndo kazi zao hizo, 4. wanawangoja askari wenzao ambao wamekwenda kuarest kwani hawawezi kwenda mpaka eneo la kuarest wakiwa na gari kwani mtuhumiwa angeweza kukimbia, 5. wapo katika taratibu zao za kazi n.k

Ushauri kwa mtoa mada:
Askari polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, na hivi wanapaswa kupongezwa kwa kazi wazifanyazo. Amani inayoonekana nchini kwetu ni kwa sababu ya utendaji wao kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola. Askari hao utambue ni binaadamu kama wewe. Ili kuwarahisishia utendaji wao yatupasa sisi wananchi hasa madereva tutambue kwanza wajibu wetu tukiwa tunatumia vyombo vyetu vya usafiri katika barabara wanayoitumia watu wengi. Tukiwa na desturi ya kutii sheria tutawaepuka hao askari ambao kwa kupaki gari zao tu, wewe umewaona kana kwamba wanapokea rushwa. Mada yako ni nzuri isipokuwa haina nguvu kisheria kwa sababu imekosa uthibitisho wa utata unaoonekana! Hapo askari hao hawana kosa lolote kaka. Ni mimi mpenda haki: Kandidus
 
mbona hiyo event haionekani katika picha hii,hapo yawezekana walikuwa wanamwandikia huyo mteja wao noticification.
 
Hata mimi nakubaliana na Mitchell na Paka Jimmy: there is no a testimonial proof on corruption grounds! No correlation completely between the blog (words) and the photo. May be Njele wanted to show the public on how he is a good photographer. In its strictly sense, the pic is well targeted, so he is a good shooter. :shock:
 
Hapa bado picha hai justfy kwamba polisi wanapokea rushwa, kumbuka polisi pia wanatembea na kitabu cha notification, inawezekana pia kwamba jamaa alikuwa analipa faini kwa kosa lake.
 
kwa picha hiyo hakuna kitendo chochote kinachoonyesha transfer ya cash au kitu chochote cha aina ya rushwa kati ya traffic na hao raia!
Mleta mada umejuaje kuwa rushwa ilitolewa hapo?...au unahisi tu kutokana na default value juu ya tabia ya hawa ndugu?
Ni rushwa gani inatolewa mbele ya kundi la watu namna hiyo?

Halafu kwani traffic police hawana ndugu na jamaa zao wanaoweza kuongea nao kama hivyo pichani?
Mi naona ni shughuli za kawaida tu zinaendelea hapo, kuna kijana anaosha gari, wengine wanachati tu na maafisa hao, lakini hakina m'badilishano wowote wa pesa hapo!

Mleta mada alitakiwa apige na picha labda inayoonyesha gari fulani imepaki kwa kukamatwa, hapo ndipo ingeleta ushawishi wa kuamini kuwa madereva wake ndiyo wanamsaundisha traffic, lakini kwa mazingira hayo. Hakuna dalili hizo!

hivi ulipostaafu polisimpwa ulibaki na kile kile cheo chetu cha staaff sajenti??
 
hivi ulipostaafu polisimpwa ulibaki na kile kile cheo chetu cha staaff sajenti??

That is personal attack, jadili hoja, kwenye hiyo picha kuna rushwa inatolewa au hakuna? mambo ya ustaff sajent yanatoka wapi hapa.
 
watanzania wenzangu,
kimsingi fikirini kwanza kabla hamjatoa mada katika jamii forum ili tuzijadili. Jeshi la polisi tanzania kupitia kikosi cha usalama barabarani linapaswa kupongezwa kabisa. Mtoa mada uliyepiga picha hii, ebu tafuta takwimu za ajali kwa miaka miwili tu ilyopita, utakuja kukiri kuwa kwa miaka miwili iliyopita katika barabara ya dsm-morogoro - iringa kulikuwa na ajali nyingi zilizosababisha vifo vya watanzania wengi, na wengine kubaki kuwa tegemezi baada ya kukatwa viungo vyao vya mwili. Hii ni kwa sababu magari hayo uliyoyapiga picha hayakuwa yanafanya kazi barabarani kuthibiti wavunja sheria za barabara hususani mwendo kasi ambao siku zote umekuwa chanzo cha ajali zilizowaua watanzania ambao ndo nguvu kazi ya taifa letu.

Kutokana na sababu hiyo basi, kwa mwaka huu 2012 kamanda mpinga amekuja kivingine kwa kushirikiana na wakuu wa vikosi vya usalama barabarani wameweka mikakati ya kuongeza vithibiti mwendo na magari ya high-way patrol ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuthibiti ajali za barabara kuu kama sio kuzuia kabisa. Kutokana na ukweli huu basi, kwa madereva na wananchi wasiotii na kujua athari za ajali mf. Aliyetoa mada hii, hawatambua hata kidogo utendaji wa trafic wakiwa barabarani. Kwa ujumla picha hii haina uhusiano hata kidogo na mazingira ya rushwa. Kwani gari la polisi katika picha hii hapo juu linaonekana limepaki barabarani inawezekana ikawa kwa sababu mbalimbali: 1. Wameharibikiwa 2.kunataarifa wanaisubiri, 3. Wanangoja msafara maana ndo kazi zao hizo, 4. Wanawangoja askari wenzao ambao wamekwenda kuarest kwani hawawezi kwenda mpaka eneo la kuarest wakiwa na gari kwani mtuhumiwa angeweza kukimbia, 5. Wapo katika taratibu zao za kazi n.k

ushauri kwa mtoa mada:
Askari polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, na hivi wanapaswa kupongezwa kwa kazi wazifanyazo. Amani inayoonekana nchini kwetu ni kwa sababu ya utendaji wao kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola. Askari hao utambue ni binaadamu kama wewe. Ili kuwarahisishia utendaji wao yatupasa sisi wananchi hasa madereva tutambue kwanza wajibu wetu tukiwa tunatumia vyombo vyetu vya usafiri katika barabara wanayoitumia watu wengi. Tukiwa na desturi ya kutii sheria tutawaepuka hao askari ambao kwa kupaki gari zao tu, wewe umewaona kana kwamba wanapokea rushwa. Mada yako ni nzuri isipokuwa haina nguvu kisheria kwa sababu imekosa uthibitisho wa utata unaoonekana! Hapo askari hao hawana kosa lolote kaka. Ni mimi mpenda haki: Kandidus

mkuu kandidus
ahsante sana mkuu kwa kuwatetea lakini nikutabanaishe wale watu wamekuwa zaidi ya mbwa...kama uamini njoo pale kawe kwenye daraja mi nina picha baadhi ila kuna mmoja namwinda kwelii bahati mbaya wanawake ndio wananikamata waananiacha natafuta mwanaume moja nimlete huku na aibu yake...utaona asbh na mapema wanasimamisha gari wanaiacha wanaenda kusimamisha wanaiacha ...infact nimekuwa na urafiki na hao polisi wa kike saababu ya kunisimamisha siku moja mwendawzimu mmoja mwanaume akaniacha akasimamisha mwingine aliporudi akasoma namba tu zikiishia..so ni wana njaa zaidi ya mbwa wa porini
 
Keshokutwa yake nikasimamishwa namwanamke aakaniomba lesen nikampa akaniomba fire ext ,pembe tatu nikamwonyesha akasema nenda safari njema nikamwambia unakunywa nini akasema whisky nkampa 5000,akaniuliza yule dada juzi si walikusimamisha au sio wewe ukaondoka nikamwambia ni mimi na ungenisimamisha vile ukaniacha walahi na wewe ungesoma namba akacheka sana akaishia we mchaga nini 5000 nikanywe mbege???
sio kwamba namtongoza nimefurahia anafanya kazi yake vizuri sio wanaume ukiona wakija kama wanataka kukuvua nguo mwanaume mwenzao na wapumbavu wengine wanaingia ndani ya gari unauliza anasema nini huyu pumbavu kwenye gari yangu...soo nahisi wanafundishwa kabisa mshhara wenu ni laki 4..zinzobakia tutawalinda kwa damu yooyyoote angalia jerry muro alivyowaaibisha wameenda kumkamata mwisho wa siku yule pumbavu waziri wa mambo ya ndani akaishia na aibu na wewe unazidi kuwatetea hawa shame on you
sioni sababu ya kuwatetea we ikifika anakuuliza kila kitu uko kwenye gari anapata alafu anauliza

""""""""helmet mbona ujavaaaa"""""anataka nini kama sio bwana
 
That is personal attack, jadili hoja, kwenye hiyo picha kuna rushwa inatolewa au hakuna? mambo ya ustaff sajent yanatoka wapi hapa.

polee mkuu huyo mpwa wangu bana chochote naweza kukianzisha wala usiumie ndio maana umemwona kimya anyaway vizuri usirukie gari kwa mbele ....
 
Keshokutwa yake nikasimamishwa namwanamke aakaniomba lesen nikampa akaniomba fire ext ,pembe tatu nikamwonyesha akasema nenda safari njema nikamwambia unakunywa nini akasema whisky nkampa 5000,akaniuliza yule dada juzi si walikusimamisha au sio wewe ukaondoka nikamwambia ni mimi na ungenisimamisha vile ukaniacha walahi na wewe ungesoma namba akacheka sana akaishia we mchaga nini 5000 nikanywe mbege???
sio kwamba namtongoza nimefurahia anafanya kazi yake vizuri sio wanaume ukiona wakija kama wanataka kukuvua nguo mwanaume mwenzao na wapumbavu wengine wanaingia ndani ya gari unauliza anasema nini huyu pumbavu kwenye gari yangu...soo nahisi wanafundishwa kabisa mshhara wenu ni laki 4..zinzobakia tutawalinda kwa damu yooyyoote angalia jerry muro alivyowaaibisha wameenda kumkamata mwisho wa siku yule pumbavu waziri wa mambo ya ndani akaishia na aibu na wewe unazidi kuwatetea hawa shame on you
sioni sababu ya kuwatetea we ikifika anakuuliza kila kitu uko kwenye gari anapata alafu anauliza

""""""""helmet mbona ujavaaaa"""""anataka nini kama sio bwana[/QUOT

Kutokana na ufafanuzi wako, ninaanza kuona tatizo lilnapoanzia. Umekiri mwenyewewe waziwazi na bila kuacha chembe ya shaka kuwa ulimpa askari huyo aliyekukamata eneo la kawe tshs. 5,000/=, na pia unasema kuwa unapicha za askari hao lakini ni wanawake na wewe unamwinda huyo askari wa kiume.

Ebu jiulize kwa nini umpe pesa hizo? Kama ulikuwa na kosa kisheria kwa nini usingekuwa mpole sheria ichukue mkondo wake? Na kama ulifuata taratibu za kisheria katika matumizi ya barabara yaani hukuwa na kosa kwa nn wewe uanze kutoa pesa kwa huyo askari?

Rejea maelezo yangu kwa watanzania, na hasa ushauri kwa mtoa mada hii tunayoijadili (Njele). Kutokana na maelezo yako yenye ushahidi wa wazi na unaojitosheleza, watanzania na watu wote duniani watakubaliana na mimi kuwa sisi wananchi ukiwemo na wewe (Pdidy) na hasa watumia barabara ni chanzo cha tatizo hili tunalolijadili hapa leo. Kwa mantiki hii basi, kwa kuzingatia Sheria za Nchi, Katiba na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa makosa ya Rushwa, kama ilivyofafanuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), wewe Pdidy unapaswa uwe mshtakiwa no. 1 uliyetoa rushwa Tshs. 5,000/= kwa askari huyo pasipo yeye kukuomba, naye anatakiwa awe mshtakiwa no.2 kwa kupokea rushwa ambayo wewe pdidy umemshawishi aipokee. Kadiri ya Muasisi wetu Baba wa Taifa, Mwl. J.K. Nyerere, katika hotuba yake aliyoitoa kwa watanzania mwaka 1979, " mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ninyi ni washtakiwa. Adhabu yenu miaka sita jela na viboko 12 mnapoingia na mnapotoka jela".
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom