Silaha sioni shida kukutwa nazo, sasa hizo risasi nyingi hivyo anakuwa nazo kwa kazi gani hasa??
Swali la kizushi tu mwanafyale; Tatizo unaloliona ni kuwa na silaha au risasi. Kwani zilikuwa risasi za silaha tofauti na alizo nazo au? Kuna kitu mwanafyale kinaitwa kulenga shabaha. Mtu unatoka na bunduki yako unaenda porini au hata nyuma ya nyumba yako, kama umesha waambia majirani kwamba unalenga shabaha. Unaenda kupiga risasi zako za shabaha hata hamsini hivi kwa siku. Kule JKT tulipewa risasi 30 siku moja tukaenda kulenga shabaha. Sasa weye waona hizo ni nyingi kakutwa nazo?? Akitumia 30 kwa siku atatumia kwa siku ngapi??? Tuelezwe kama aliziiba au aliuziwa kimagendo lakini kama ana risiti zake, shida iko wapi??
Kama walimkuta na silaha ambayo haimiliki kihalali hapo ni kosa. Msimtafutie mtu kosa jamani. Mwacheni awe ametenda kosa. Kama hajawahi kutishia mtu, hajawahi kuvamia kituo cha petroli kuiba sasa kukutwa tu na risasi za silaha alizonazo kihalali ndiyo iwe issue??
Msimchukie mtu hivyo ati si mwenzetu. Mnamtisha ili arudie matapishi??