POTOSHI Picha, Polisi Uganda wakikagua video ya mwisho aliyopost Bobi Wine kufahamu alipo

POTOSHI Picha, Polisi Uganda wakikagua video ya mwisho aliyopost Bobi Wine kufahamu alipo

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Kama alivyotoa tamko Jenerali Muhoozi Kabobi atafutwe apatikane akiwa hai au amekufa

Ila nimegundua ukishaitwa Polisi kidogo unakuwa hamnazo yaani zinafyatuka, hapo wakiulizwa mnamtafuta kwa kazi gani na wao watajibu ni order ya Jenerali

Bobi na Polisi JAN, 2026.jpg
 
Tunachokijua
Mara baada ya uchaguzi mkuu wa Uganda uliofanyika Januari 15 na matokeo kutangazwa ambayo yalimthibitisha Rais Yoweri Museveni kuendelea kusalia madarakani, mpinzani wake Bobi Wine amekuwa akipokea vitisho mbalimbali ikiwemo mkuu wa majeshi nchini humo Jenerali Muhozi kuagizwa akamatwe.

Madai

Kupitia mtandao wa Facebook mtumiaji mmoja amechapisha picha inayowaonesha polisi iliayoambatana na ujumbe unaoeleza kuwa jeshi la polisi nchini Uganda idara ya CCTV wanafuatilia video ya mwisho kufahamu ni wapi alipo aliyekuwa mgombea Urais wa Uganda 2026, Bobi Wine.

Uhalisia wa madai hayo.

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa madai hayo yanapotosha uhalisia wa picha iliyoambatanishwa.

Kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo Google reverse Image Search imebainika kuwa picha hiyo ya askari polisi iliyotumika imekuwepo mtandaoni kuanzia mwaka 2021 na si ya mwaka 2026 kama inavyodaiwa na mtumiaji huyo.

Picha hiyo ilichapishwa na Hytera katika tovuti yao na jarida lao inaonesha ni katika wakati ambao polisi wa Uganda walikuwa wakipatiwa mafunzo yaliyokuwa na lengo la kuboresha njia zao za mawasiliano.
Kama alivyotoa tamko Jenerali Muhoozi Kabobi atafutwe apatikane akiwa hai au amekufa

Ila nimegundua ukishaitwa Polisi kidogo unakuwa hamnazo yaani zinafyatuka, hapo wakiulizwa mnamtafuta kwa kazi gani na wao watajibu ni order ya Jenerali

Danganya toto hizi ni sarakasi na Bobi ni Project ya M7, kila jambo lina mwisho wake
 
Watu weusi bado tuna miaka kama 100 hivi ya evolutionary process tuufikie ubinadamu yani, sio kizazi hiki wala kijacho, labda cha 3 au cha 4 kure mbereeee...
Tupo nyuma sana kwa kweli ,USA wapo mbele sana kwenye uhuru wa maoni...Trump anapewa za uso na raia na haukuti wametekwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom