Picha: Mkutano wa chadema huko Karatu...

Pamoja na mapungufu yake kijana huyu mimi namkubali. Hivi kuna mtu asiye na mapungufu kweli? Jamani tuache majungu tujenge chama chetu. Adui wetu ni mmoja tu, CCM.
 
Zito ndio injini ya CHADEMA,akihama CHADEMA kwisha habari yake.
Acha kujipendekeza kupita kiasi, ukweli ni kwamba CHADEMA ilipofika sasa hivi si Mbowe, Dr. Slaa, ZZK au yeyote anayedhani umaarufu alionao ni wa "One person show" akiondoka hakifi na wenyewe wanaelewa hivyo. Ndiyo maana watabiri wa "Vifo" kina Wassira wamebaki kuhunyahunya mithili ya paka shume lililofumwa likiiba mboga
 
Zitto kabwe wewe unanyota ya ajabu sanaaaaaaa...yaani licha ya fitiza zote wanaziokutengenezea lakini bado umewafuata kwao na umewaonesha namna gani you have political influence&power
safi sana kamanda,endela hivyohivyo.
 
Ni mkutano wa Zitto ama wa chadema?Duh! mkuu kuna kazi unayoifanya ambayo haina manufaa na chama chako(endapo wewe ni mwanachama)
 
Huyu Said Kulwa ukitaka kumjua nenda wall page ya Habib Mchange kila siku anawatukana matusi ya nguoni Mbowe/Dr Slaa/John Heche utadhani hakuzaliwa na mwanamke!
 
Naona Zitto ameamua kuanza kummaliza Slaa kwa kuanza na mashambulizi ya nyumbani kwake. Am sure with time Zitto atakuwa maarufu Karatu kuliko Slaa.
 
Hapo ndipo vibweka vya matumaini yetu vinapolizima tumaini. One man's show. Hongera Zitto, i hope you know what you are doing.
 
Nadhani unamaanisha hivi karibuni atakuwa maatufu kuliko chadema. Asike akajikuta anaowahutubia wanatafuta kwenye karatasi ya kura chamacha Zitto. Manake yeye haendi kama chadema,anaenda kama yeye.
Naona Zitto ameamua kuanza kummaliza Slaa kwa kuanza na mashambulizi ya nyumbani kwake. Am sure with time Zitto atakuwa maarufu Karatu kuliko Slaa.
 
mimi ni muumini wa sawa na zitto lakini mambo yote anayofanya huwa mengi nje yawatu wasiofuatilia siasa kwa undani zaidi hayana tatizo lakini internally huwa kyeye anajua alicholenga mwenyewe na ukitaka kujua anachosema z amedhamiria chunguza wale vijana walioko pale chadema wanaojiita vijana wa zitto wanavyokuwa wanabehave katika ishu husika mfano katika hili la kutaka kugombea urais z amedhamiria saana si kidogo na ndio maana kijana mchange, mwampamba, nyakarungu,saanane,mbunge rachel,sasa wako front mpaka facebook na kila mahali kukashifu chama na dr slaa na hata huu mkutano wa karatu usikute ni kimkakati zaidi ya lengo la kujenga chama kwenda kujipima kuwa kama kauli aliyoitoa imewaingia hawa wakazi wa karatu vipi lakini wasikilizaji wao wamejongea katika maslahi ya chama huku mitaani utasikia kama hakubaliki kuwa mgombea urais mbona kapiga mkutano karatu? sasa utazani mkutano wa karatu ndio hutoa mwelekeo wa urais
 
Huyu Said Kulwa ukitaka kumjua nenda wall page ya Habib Mchange kila siku anawatukana matusi ya nguoni Mbowe/Dr Slaa/John Heche utadhani hakuzaliwa na mwanamke!
kwenye lilee tanuri la matusi wanaloita tanuri la fikra
 
mleta maada hakuna mtu mwingine aliyehutubia au ulilenga kuleta maada inayomhusu zitto tu siyo?
 
Nadhani unamaanisha hivi karibuni atakuwa maatufu kuliko chadema. Asike akajikuta anaowahutubia wanatafuta kwenye karatasi ya kura chamacha Zitto. Manake yeye haendi kama chadema,anaenda kama yeye.
Kila kiongozi wa CDM anatafuta kutoka kivyake. Kila mtu ana mtizamo wake, CDM kama chama hakina common goal. Kwa anachokifanya Zitto siyo kitu cha kushangaza
 
Huu mkutano wa lini weka tarehe maana jana nasari alikuwa ngarenanyuki na king'ori kwenye jimbo lake na mimi nilishuhudia huu wa lini

nassari anafanya mikutano na ziara nyingi jimboni kwake..na pia katika m4c yupo..nadhani hii ni katika kutekeleza ile kauli ya hakuna kulala mpaka kieleweke
 
Kila kiongozi wa CDM anatafuta kutoka kivyake. Kila mtu ana mtizamo wake, CDM kama chama hakina common goal. Kwa anachokifanya Zitto siyo kitu cha kushangaza

Rejao Common Goal ya CCM nini?:A S 39:
 
Kila kiongozi wa CDM anatafuta kutoka kivyake. Kila mtu ana mtizamo wake, CDM kama chama hakina common goal. Kwa anachokifanya Zitto siyo kitu cha kushangaza
Hilo nalo neno mkuu!! Naona kuna similarities kdg kimkakati na magamba! CDM have to stop their dfferences and have the same ground. Hata kama kuna tofauti katika kufanya maamuzi hizo ndo gharama za kuwa katika kikundi kimoja kikubwa ambapo maamuzi wakati mwingine hufanyika sivyo baadhi ya watu wanavyotaka. This is the weakest point of the so called "democrasy". Lakini pia hakuna mtu asiyekuwa na mapungufu, mhimu ni kukabiliana nayo kwa njia halali siyo kuwindana au kuviziana huku mkiogopana kuelezana ukweli hata kama mmoja utamuuma.
 
Unapoweka picha pekee sio kiwakilishi kizuri cha mkutano ni vizuri ukatuwekea na maneno yaliyoongelewa katika mkutano huo ili tuweze kuchangia

Shukrani kwa picha. Picha inatoa ufafanuzi zaidi kuliko maneno.
 
Back
Top Bottom