Picha nzuri sana. Wareno walipanga huo mji vizuri. Kama wajerumani walivyozipanga Tanga na Moshi.
Natamani wengi waliochangia wangeonyesha walau wamefanya/wanafanya nini kupiga hatua kuelekea maendeleo makubwa zaidi ya tulipo. Wengi wameishia kulaumu.
Ni sawa na kuona jirani kanunua gari, badala ya kushauriana ndani ya familia namna ya nyie kusonga, mnaishia kutukanana, kuzodoana na kuitana majina!! Hapo, mchawi ni nyie wenyewe.
Picha kama hizi zitupe hasira ya kubadili yanayoturudisha nyuma. Na cha kwanza ni mtu mwenyewe. Tusiangalie mbali. Mtazamo chanya na kujibidisha ni mwanzo wa kuelekea pa kuja kupigiwa mfano.
ANGALIZO: hivi kwanini katika hizo picha 'hakuna' watu? Hao wachache walioonekana wana hali za kawaida sana ukilinganisha na 'utamu' wa kimcharo wa hizo picha!!! Kuna kitu hakiko sawa......
MAENDELEO YA KWELI HULENGA WATU......