so unataka akaombe mochwari serikali kuu? kwani machame hosp na uswaa kuna umbali gani??? msisitizen akomalie mfuko wa barabara wa jimabo ili iyo bara bara toka masama kuja kalali iwekewe lami na pia ya nkuu lyamungo vinginevyo atabaki kupita angani daily nyie mkivuka kikafu kwa miguu......
mikelele mengiii, wakikutana nae ovyoooooooooo
Mkuu Ritz,baada ya kumtambua kama rais,kugonganao chai ikulu, kitakachofuata ni lift za ulaya ndani ya gulf stream hapo ndio mwisho wao magwandwa.
Namuunga mkono BEN SAANANE AWE MBUNGE WE2 WA ROMBO KWA NGUVU ZOTE
Mbowe ni kijana wa JK humu JF Pro-Chadema povu linawatoka ovyo mwenye chama Mbowe yupo katulia kwa JK anawachora tu.
Kwani hiyo barabara Jk anaijenga kwa kutoa pesa mfukoni mwake?Tufikie hatua hatua tusiwafanye wapinzani waonekane yatima ndani ya nchi yao.
CHADEMA mtajikuta mmejaza type za akina Tundu Lissu bungeni.wanasiasa wasomi wanaokurupuka na misimamo isiyo na tija na kupotosha umma kila siku.Ndicho anafanya Ben na akina lisu kwenye siasa hii
Mhe.Joseph Selasini naye alimshukuru JK lakini akatukanwa sana humu kuwa ni mamluki,mtu wa hovyo asiyefaa. Mdau mwingine alisema kuwa Mhe.Selasini alimsifu JK kwa sababu anajifagilia njia ya kwenda CCM 2015. Hapo niliona Ben Saanane akitokwa mapovu kuwa Selasini alikosea. Nilikuwa kimya kwa sababu nilitarajia Mbunge mwingine atafanya hivyo ili tuweze ku justfy licha ya kuwa hilo liliwahi kutokea kwa Mhe.Sugu na Mhe.Zitto.
Kwanza kama mwanasiasa unapaswa utumie maneno yako kwa mbinu na umakini mkubwa. Kumshukuru Rais ina maana pana sana ambapo hapa sitaiandika yote,ila kwa sehemu mkumbuke kuwa Rais ndiye Mwenyekiti wa Baraza la mawaziri ambalo hupanga matumizi( Budget) ya mwaka mzima. Rais anayo nafasi ya kuongeza au kutoa mpango wowote kwenye bajeti ya wizara yoyote.
Taabia ya kiongozi wa Siasa kushambuliwa na wasio wanasiasa au waliovaa pampers za kisiasa huku wakidhani kuwa ni Wanasiasa kama kina Ben Saanane ni tabia mbaya na ya hovyo!. Mwanasiasa anapofanikisha moja ya ahadi zake kwake ni moja ya ngazi ya kushinda tena kwenye siasa uchaguzi ujao. Wewe unayekaa Online huku huna ulichoahidi wala cha kutekeleza! Huwezi kufanya kama yeye! Unasubiri atoe kauli yoyote uweze kuongea. Yes! Endeleeni kuwalaumu wanasiasa wanapotekeleza ahadi zao kwakuwa nyie kamna cha kufanya kwa wananchi.
By Deus.
Magesi,
-Mkuu usitake kuua watu presha
Pia kuna mtu anadai hapo juu kwamba anajua nina nia ya kugombea ubunge Rombo.Hii ni ramli kwani siku zote naamini katika taasisi.Nimekua nikisizitiza umuhimu wa kukijenga chama badala ya kujijenga.Hatuhitaji watu imara bali taasisi imara zenye uhakika wa kutoa watu imara siku zote
Sioni mantiki ya kujijenga kwa ajili ya kukimbilia bungeni kudai nyongeza ya posho badala ya kushiriki katika harakati nchini katika ujenzi wa Chadema imara kitakachoshinikiza mabadiliko ya kisheria na kisera ili kuleta maendeleo kwa watu wote na kwa mfumo halali bila kulazimika ku-accomodate hoja za ovyo za watu kudai nyongeza ya posho ili wawagawie wananchi.
-Pia ni kweli sikubaliani na kitendo cha kutamani kuibatiza Barabara kwa jina la Rais 'Jakaya Kikwete Road'.Fikra za aina hii ndizo zinazorudisha harakati za mabadiliko ya fikra nyuma kwa kuwa wananchi wanawexa kudhani ni hisani na sii huduma ya msingi na si wajibu wa serikali kufanya hivyo.Dhana ya kumpongeza ni motisha lakini tusifikie hatua tukawa tunafanya mambo ya ajabu
Barabara ni vipaumbele na ni utekelezaji wa mkakati wa kisera kuliko haiba ya kujitukuza kama wafanyavyo madikteta wengi wa Afrika kwa kujijengea minara na kujibatiza majina katika viunga.Rais kufungua au kutenga bajeti kwa ajili ya kujitukuza na kukosa umakini
Nasizitiza kwamba barabara ya Rombo ni haki yao na si hisani.Ni barabara ya kimkati na CCM na serikali yake walikosea vipaumbele kwani ni strategic road.Kama waliweza kukwapua bilioni 152 za EPA ni kwa nini wakose fedha za kujenga ile barabara?
Pia huyo anayeuliza nimefabya nini Rombo,jibu analo.Anajua mchango wangu wangu katika kuhakikisha Chadema inashinda Ubunge Rombo,Ubungo,Kawe na Kilombero katika uchaguzi mkuu uliopita.Naendelea kutoa mchango wangu kwa chama bila hofu.
Sitaki kuwa opportunist kama wale wanaojiunga na harakati dakika za mwisho na wengine wakitokea vyama vingine kwa ajili ya kuwaza ubunge tu.Sitaki kuwa mtu wa kufuata upepo wa kisiasa tu.Watu wa aina hii mara nyingi wana matatizo
Siasa za propaganda bila mikakati hazitatusaidia.Matokeo yake tutafikiria kusolve matatizo kwa falsafa ya dharura kwa njia ya kufikiria kuwagawia fedha.Wananchi wanahitaji migomba,vijana wanahitaji migomba na sio ndizi
Nasizitiza kua tuendelee kuijenga CHADEMA ili tusukume harakati hizi bila kufikiria POSHO.Mbunge sio father xmass.Ni wajibu wa serikali kutoa huduma muhimu na si wabunge kuwagawia fedha,ni wajibu wa serikali kujenga barabara kwa kuzingatia vipaumbele vya kisera kama public expenditure according to national priorities other than self glorification under unguided principles!
Sijui ni jambo gani umeza kufanikisha
Nothing to justify.Unaweza kuleta uthibitisho hapa kwamba akina Zitto na Sugu walishawahi kutaka miradi ya barabara ibatizwe jina la Rais as if si wajibu wake kutekeleza vipaumbele kupitia kodi ya wananchi?
-Kama wewe ni mwanasiasa uliyekomaa..je unajua madhara ya kauli ya aina hii?Tusirudishane kwenye enzi za state party.
Ipo siku sasa utatangaza kwamba maendeleo tuliyopata ndiyo stahiki yetu tangu miaka 50 iliyopita kwa hiyo hakuna haja ya mabadiliko.Nayo utaendelea kuiita ni siasa
-Well,Rais ni msimamizi wa Cabinate na ana veto kwenye budget priority.Jiulize kama asingetekeza yeye na chama chake wasingeathirika?
Hivi kama Rais angezindua barabara hiyo wiki iliyopita kabla ya uchaguzi mdogo ungetamka maneno uliyosema?Ni nini madhara yake katika mapambano haya ya fikra na attitude ya wenye kiu ya mabadiliko kwenye uchaguzi?Na hili unajua lina impact gani in future?
Huu ndiyo ukomavu wa kisiasa?Kazi ya upinzani ni kukosoa na kuna tofauti kati ya kukosoa na kupinga.Kukosoa ni kutoa alternative.Ndiyo maana nikasema Rais alitakiwa ku-apologize wananchi wa Rombo kwa kuchelewesha barabara tangu tupate uhuru.
Hakuna kisingizio cha vipaumbele hapo,kwa nini hela za EPA zisingepelekwa Rombo?Kipaumbele hapo kiko wapi?Kumsifia na kumtunuku barabara kama utukufu baada ya hayo yote ndiyo ukomavu wa kisiasa?
Wanasiasa waliotanguliza posho mbele tangu tupate uhuru ndio waliochangia kwa kiasi kikubwa kutukosesha barabara kwa kuwa vipaumbele vilielekezwa huko.Nakipongeza chama changu CHADEMA kwa kusimamia kupinga posho kwa wabunge ili vituko kama hivi vya kukosesha wananchi huduma visijirudie