PICHA: MBAGALA ILIVYOKUWA LEO, MABOMU;Vurugu bila busara kutumika si-rahisi;Makanisa 3 ya yavunjwa ?

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia wakiwadhibiti vijana waliokuwa wakileta vurugu eneo la mbagala kufuatia kijana mmoja anaesemekana anasoma kidato cha kwanza kukojolea mkojo Quraan na kusababisha hasira kwa waisilamu hassa vijana ambao walitapakaa mitaani na kuanza kuleta vuru.
Vijana waliosambaa mitaani na kuamsha vurugu kubwa kwenye eneo hilo la Mbagala Kizuiani.


Waisilamu waliotoka msikitini kwenye swala ya Ijumaa walikumbana na kimbembe cha kamatakamata hatakama hawakuwemo kwenye sakata hilo, alama ni kanzu na sijda






Hapa baadhi ya waisilamu walioamua liwalo naliwe nakuamua kuwatunishia msuli polisi nakusema pigeni mpendavyo hatoki mtu.




Barabara zilikua zikiharibiwa kwa moto ulikuwa ukiwashwa na waisilamu hao wenye hasira.
Maji ya kuwasha yalikuwepo ingawa hayakuweza kuzuia vurugu hizo.




Askari na watuhumiwa wakivuka pamoja kwenye mtaro wa maji taka.




Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi.



Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kupinga kitabu kitakatifu cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat ambaye aliitemea mate.


Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala leo


Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)



Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam leo



HAMISI SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU JIJINI DAR LEO.Picha na Happy Mnale


Picha na Mtaa kwa Mtaa Blog


DAR ES SALAAM, Tanzania


VURUGU kubwa zimezuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)' kukojolea kitabu cha Quraan cha dini ya kiislam limeingia katika hatua nyingine baada ya waamini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto huyo ili wamuue.


Waamini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of God(TAG), Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza hadharani.


Vurugu hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa 5 asubuhi ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala Kizuiani.


Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.


Awali waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.


Kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.

Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.

"Ndio nini sasa sisi tupo hapa kwa kuleta suluhu lakini ili waislamu watulie lakini mnawapiga mbele yetu ndio nini sasa
 
Hata kama ni hasira kali kama tunavyoaminishwa, kwa nini mara zote hasira zao huishia kuharibu makanisa kwani yamewafanya nini? Je, wakristo wangetumia sababu msheji kama hizo za watu wenye hasira kule Zanzibar si kungechimbika? Mbona waislam wanataka kutumia uhuru huu walionao kupita kiasi?
Yapo mengi ya kujiuliza, lakini sasa mmezidi na mnakela kupita kiasi.
 
Saa Nyingine hizi habari zetu zinakuwa One SIDED zinatia kichefu... Sasa kama Mwandishi ameandika Makanisa 3; Yalibomolewa mbona hakuweka hizo picha ? Ni Uandishi au Ushabiki ?

* Maisha yetu yoote tuliyoishi Tanganyika; Utotoni hadi Ukubwani, hatujawahi kuwa na UBISHANI wa AINA HII Wa kuingilia VITABU VITAKATIFU; NI WAZAZI; SHULE ZETU; MAZINGIRA YETU YA SASA; AU UMBALI wa SERIKALI yetu Kwa Wananchi ?
 
Hivi anayejua umuhimu wa msahafu halafu akauleta ukojolewe na ambaye hajui umuhimu wake akaukojolea nani mwenye makosa,mbona wote wanafaa wangepewa adhabu zao na siyo kulalia upande mmoja.Au kuna sababu zingine za siri?
 
Haya ni maumbile ya mwanadamu!!! unapombana sana lazima atafute pakutokea...... ndani ya kadhia hii yapo mengi yamejificha nyuma yake! Haya ni matokeo ya serikali iliyoshindwa kuongoza!! Tafakari na chukua hatua japo ninauhakika hatua utakazochukua nazo zitaletewa zengwe kuwa kesi ipo mahakamani..... ha! ha! ha!
 
Saa Nyingine hizi habari zetu zinakuwa One SIDED zinatia kichefu... Sasa kama Mwandishi ameandika Makanisa 3; Yalibomolewa mbona hakuweka hizo picha ? Ni Uandishi au Ushabiki

* Maisha yetu yoote tuliyoishi Tanganyika; Utotoni hadi Ukubwani, hatujawahi kuwa na UBISHANI wa AINA HII Wa kuingilia VITABU VITAKATIFU; NI WAZAZI; SHULE ZETU; MAZINGIRA YETU YA SASA; AU UMBALI wa SERIKALI yetu Kwa Wananchi ?
nakubaliana nawe kwa kiasi fulani lakini kumbuka siku zote kosa siyo kosa lakini reaction ya kosa lilofanyika inaweza kuwa kosa kubwa kuliko kosa lenyewe. mtoto amefanya kosa ilibidi sheria za nchi zifuatwe kwa mhusika kufikishwa kwenye mamlaka zinazohusika. sasa leo watu wasiousika na tukio zima ndio wanapata hasara kwa upuuzi wa watu wengine hilo ni kosa pia.
 
Hivi anayejua umuhimu wa msaafu halafu akauleta ukojolewe na ambaye hajui umuhimu wake akaukojolea nani mwenye makosa,mbona wote wanafaa wangepewa adhabu zao na siyo kulalia upande mmoja.Au kuna sababu zingine za siri?

Unapiga siasa na imani za watu! Unacheza wewe!!!we juzi umeona ile filamu ya kimarekani ilivyoleta kashehse!! kwenye imani hakuna busara kama hizi za kisiasa siasa!

 
as usual mbagala,manzese na kwa walalahoi wengine

huwezi sikia masaki,mbezi beach..ingawa huko kuna watu wa dini zote pia
mkuu hata siyo kwa vile ni kwa walalahoi,mfano libya na misri tungesemaje,filam imetengenezwa U.S.A watu wanauana kwengine
 
Haya ni maumbile ya mwanadamu!!! unapombana sana lazima atafute pakutokea...... ndani ya kadhia hii yapo mengi yamejificha nyuma yake! Haya ni matokeo ya serikali iliyoshindwa kuongoza!! Tafakari na chukua hatua japo ninauhakika hatua utakazochukua nazo zitaletewa zengwe kuwa kesi ipo mahakamani..... ha! ha! ha!

can not quickly spot a correlation
 
Back
Top Bottom