PICHA: MBAGALA ILIVYOKUWA LEO, MABOMU;Vurugu bila busara kutumika si-rahisi;Makanisa 3 ya yavunjwa ?

Sasa wanachoma makanisa na kuharibu magari ya watu , makanisa ndio yalimtuma mtoto afanye hivyo?
Anyway kwakuwa chuki za udini zinaenezwa na viongozi wamekaa kimya hawakemei ndio matokeo yake haya, na tutakuja fika pabaya zaidi
 
nakubaliana nawe kwa kiasi fulani lakini kumbuka siku zote kosa siyo kosa lakini reaction ya kosa lilofanyika inaweza kuwa kosa kubwa kuliko kosa lenyewe. mtoto amefanya kosa ilibidi sheria za nchi zifuatwe kwa mhusika kufikishwa kwenye mamlaka zinazohusika. sasa leo watu wasiousika na tukio zima ndio wanapata hasara kwa upuuzi wa watu wengine hilo ni kosa pia.

Nakubaliana na jinsi unavyoangalia kiupande Mwingine... Lakini nimesema kuna sababu watoto wa Miaka 14 kuwa na upotofu na udhaifu wa kuelewa UMUHIMU wa VITABU VITAKATIFU; Mimi nikiwa na Miaka 14; Tanganyika nilikuwa Form 2 FORODHANI SECONDARY... Sasa Uniambie Masuala kama hayo hao VIJANA walikuwa wanayaongelea kweli ni kosa kubwa; kama nchi yetu kweli ndio inakuza Mambumbumbu kiasi hicho; kweli hizo SHULE za KATA na SERIKALI zifungwe; tujue kama KENYA PRIMARY EDUCATION is PRIVATE; Huyo mtoto wa Miaka 14 haujui anaweza kuzaa MTOTO ?
 
Katika picha moja nimeona washabiki wa chelsea,huyo dogo aliyekininiliu kile kitabu lazima atakuwa mshabiki wa timu pinzani na chelsea.
 
Haya Serikali sikivu itoe tamko: Zanzibar makanisa yanachomwa mara kibao wahusika hawawabibishwi hili si jambo jema hata kidogo............. sasa watawala hebu wajitathimini kwanini haya yanatokea wakiwa madarakani na kauli zao je zinasaidia au vitendo vyao? Hawa watu washughulikiwe kisheria ila wakiachwa itabidi tuamini kuwa kuna siri nyuma ya haya matukio ya kubaguana kidini
 
Hii Jeuri ya fujo..... Haya yote nani? Jaka yaaaaaaaa.............Ki...kwee...teee, mwenye macho haambiwi tazama. Au mahakama ya kadhi ameshaipitisha kijanjaweed.
 
Niliyasema haya yatakuja tokea na sasa wakati umefika kuvuna kile tulichopanda...Na tusitake kuwalaumu vijana hawa maana ndivyo walivyolelewa. Toka yule kijana aliyekojolea msahafu hadi hao vijana walokwenda kuchoma Makanisa wote hawa ni victims wa UDINI tunaoutangaza kila siku iwe humu JF, majukwaa ya siasa, magazeni, makanisani na hata misikitini..Hawa vijana wamejifunza kutoka kwetu..

Ifike wakati watanzania mfahamu ya kwamba chuki hii tumeijenga sisi wenyewe na hawa vijana wanatuona tukibishana, tukitukana na hata tukitengana na hivyo wao kama zao na kizazi chenye mfumo wa Udini lazima watakuwa tunda la UDINI..na sasa limeisha iva na tayari kutumika. Hakuna cha waislaam wa Bara au wakristu wa visiwani ni sisi wenyewe ndio chimbuko tulowasha cheche za Udini na hizi vurugu ni mwanzo tu wa makubwa ya mbeleni.

Nashangaa sana watu mnaanza kulalamikia dini ilihali nyie wenyewe ndio mmepandikiza Udini na tena kwa furaha kubwa mkiitana dini za shetani, wengine wakiitwa Makafir sasa mlitegemea nini haswa kitakuja tokea..Kwa tabia hii kama hamtajifunza na hili la Mbagala basi kuna makubwa zaidi yatakuja milangoni mwenu na sijui mtakimbilia wapi....
 
sitaki kuamini kama waislam wa Bara nao wamefikia hatua hii. Ni jambo la kusikitisha sana maana haaingii akilini kuona suala ambalo lingemalizwa kibusara linafikia hapo. Pia tujue sababu ya huyu mtoto kufikia hatua hiyo ya kuikashifu kuran, na ikawaje hadi waislam 3000 wakapata habari na kuongia mitaani kwa jazba.
 
maandamano ijumaa tu?
Wakimaliza risala wafanye na swala, coincedence? Mmh!

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, ngoja wawachome machoni labda wataamka.
 
Hapa ndipo umuhimu wa kusoma unapo onekana. Elimu ni mhimu sana..... sasa hayo Makanisa mliyovunja yanahusika vp? Ni mara ngapi mmewakejeli wa Kristu na wameonyesha uvumilivu....... mna hamu ya kuona damu ikimwagika.....
 
ccm inatumia kete ya udini ili kuwa gawa watanzania na mwisho wa siku wakiamini watandelea kuwa madarakani...
 
hawa waislam wana wivu sn,sasa kesi ya kukojolea quran yaan ndo wameharibu hadi vifaa vya kanisani na kuharibu makanisa! wana uhakika gani km aliefanya hivyo ni mkristo au wameona anaitwa emmanuel basi wakajua ni mkristo.
 
Chuki dhidi ya ukristo ilishapandwa siku nyingi na kulelewa na magamba wakishirikiana na Radio Iman.

Sasa hivi hawa jamaa huwa wanatafuta kisingizio tu cha kuchoma makanisa mahali popote pale...
 
Hivi anayejua umuhimu wa msaafu halafu akauleta ukojolewe na ambaye hajui umuhimu wake akaukojolea nani mwenye makosa,mbona wote wanafaa wangepewa adhabu zao na siyo kulalia upande mmoja.Au kuna sababu zingine za siri?

Pointi muhimu sana Mkuu! Aliyeingiza limsahafu lake kwenye ubishi ndio awe wa kwanza kukamatwa na kushtakiwa. Eti, ukilikojolea utakuwa chizi; machizi wamekojolea kweli halafu mnang'aka. Upumbuvu mtupu.
 
Hivi huyo Emanuel ambaye katika ubishi ilidaiwa atageuka mnyama akifanya hivyo je bado ana maumbile ya mwanadamu au tayari amegeuka mnyama kweli???
 
natamani kuona waislam wakiandamana dunia nzima kupinga kitendo cha kijana huyo kama walivyofanya kwa aliyetengeneza filimu kule America wasipofanya hivyo nitajua ni chuki tu wamerekani
 
Back
Top Bottom