Wazazi wa Marehemu wakiweka udongo kaburini Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya Marehemu Regia Mtema mjini Ifakara
Baadhi ya wabunge toka vyama mbalimbali wakiwa mazishini Vijana wa ulinzi wa CHADEMA wakithibiti umati wa waombolezaji Umati wa waombolezaji makaburini Mwili wa marehemu ukiwasili makaburini Vilio na majonzi Pacha wa marehemu akibembelezwa Kwaya ikiimba mapambio
Wabunge wa vyama mbalimbali wakisubiri mwili uwasili kwa mazishi Vijana wa ulinzi Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akiwasili Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa makaburini Rais Kikwete akiongea na Spika Anne Makinda. Pembeni yao ni Naibu Spika Job Ndugai na Mh Hawa Ghasia Mdogo wa marehemu Wanahabari wakirekodi tukio hilo
Salamu za Shukrani toka kwa msemaji wa familia
Ibada ya mazishi ikiendelea
Spika Anne Makinda akiweka udongo kaburini Naibu Spika akiweka udongo kaburini Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akiweka udongo kaburini Sehemu ya waombolezaji Karibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa akijiandaa kuweka shada ya maua kaburini
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko. Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa heshma zake za mwisho kwa Marehemu Mhe. Regia Mtema katika viwanja vya Karimjee leo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara. Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara. Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali. Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.
Salaam Kutoka kwa Katibu mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Andrew Chenge pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Tundu Lissu, Vita Kawawa, pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na baadhi ya ndugu wa Marehemu. Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mh. Jaji Fredrick Werema. Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick. Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Sadick Meck, Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, sera Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe wakimsubiri makamu wa Rais leo katika viwanja vya karimjee kuaga mwili wa Mbunge wa Chadema Viti Maalum Marehemu Regia Mtema aliyefariki kwa ajali ya gari Jumamosi tarehe 14, 2012 Baadhi ya Waheshimiwa wabunge wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu,Mh. Regia Mtema iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani wa OMR na Owen David wa BUNGE.
Kuz Kuf, ndio nini, Kuzikwa na Kufufuka? Ukiandika
REGIA ESTELATUS MTEMA
21/04/1980 - 14/01/2012
haitoshi? and then "SECURITY CHADEMA" na miwani ka deep sea divers kubeba msalaba wa Regia, wame hijack msiba wa mtoto wa watu masikini, this is hideous.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.