Tangulia Regia, sote tu njiani. Pamoja na huzuni uliyotuachia, lakini pia umetuachia mfano mzuri wa mtu wa watu, aliejituma bila kusukumwa na mpenda maendeleo. Mtu asiye mwoga wa kusema na kutenda anachokiamini, yaani mtu asiye mnafiki. Ni nadra sana kuwapata watu wa aina hii katika dunia hii ya leo, hasa mtu mwenyewe akiwa amejiegemeza kwenye siasa.
Kimwili haupo pamoja nasi, lakini mfano uliotuachia utaendelea kuishi nasi milele, na kama tuna akili, utakuwa umefanya kazi kubwa sana ya kutengeneza kizazi chetu. Asante kwa hilo