Kumfananisha Zito na Lema ni sawa na kufananisha mlima na kichuguu.
Zito hana wa kumfananisha katika Chadema ahata Dr Slaa analijua hilo na ndilo Chadema linalowaumiza kichwa. Kwani nyota yake ni kali sana hakuna wa kuweza kuizima.
Ok Tusubiri CC ya chadema kama itaweza kumfukuza baada ya utetezi wake uliosheheni kuikosoa na kuonyesha namna walivyovinja katiba katika kadhia yake.
Natumaini unamjua vizuri ZZK, kama humjui tafadhali kaa kimya, ZZK ni kama Panya...huyu jamaa siasa zake ni za kung'ata na kupuliza, si mtu anayefanya jambo kwa kujenga chama bali kujijenga yeye mwenyewe, hafai kabisa kijana huyu mpaka abadirike na ni lazima abadirike kama anataka kusonga mbele na siasa za bongo, mwambie aache kiburi cha kujiona yeye ni zaidi ya chama na wengine.
Siasa za ZZK zimejaa ukabila, ukanda na like lingine ambalo wewe unalishabikia, angalia nani yupo nyuma ya ZZK then tafakari...
Huyu kijana mwezetu hafai hata kuwa kiongozi wa mtaa maana atawagawa wananchi wote kwa itikadi zake na mambo yake.
Tufikie wakati watu kama ZZK watolewe CDM kwa manufaa ya chama hata kama kuna gharama ya kulipa kwa hilo, why ndani ya CCM kuna heshima ya vikao ingawaje kuna makundi, ni lini ulisikia CCM wakitoa tamko lao kuhusu viongozi wao dhaifu na hao dhaifu wakatoka na kutoa matamko yao au kwenda kwao kufanya mikutano?
Mawaziri watano waliitwa, wakaambia nyinyi mzigo kwa chama, umewasikia kuja kwa media, kuitisha press conference, kulalamika FB na twitter? Why hawajafanya hili? Na unafikiri kwa nini?
Kwanini ZZK anapenda kutumia media kuzungumzia habari za chama na wala si kwenda ofisi za chama na kusema kama kweli ana agenda ya kujenga chama, kila kitu ni FB na twitter why?
Ili kutegeneza discipline ndani ya chama lazima kuchukua maamuzi magumu bila kuangalia ukubwa wa Samaki, kama ni kuvua wavuliwe tu bila hivyo kutokuwa na CDM ZZK, CDM Mbowe, CDM Dr. Slaa, Kaskazini, Magharibi...etc
Ifikie wakati chama kwanza majina binafsi baadaye na hili ndiyo wengi tunataka, majina yapo, yanakuja na yatapita ila chama kitizidi kuwepo na kushamirikama tukiamua kujenga chama na wala si watu.
Nani alikuwa na nguvu kama Augustino Lyatonga Mrema kwenye siasa za TZ, yupo wapi sasa? Tuache siasa za majina na tujenge vyama kwanza, CDM bila ZZK, Mbowe, Slaa na wengine inawezekana kama tukiamua kuchukua maamuzi magumu.