PICHA: Majengo marefu zaidi Duniani, Jengo la kwanza lipo Dubai(UAE), China yaongoza kuwa na majengo mengi marefu Duniani

Mleta uzi hebu mzalendo na nchi yako na bara lako la Africa,Sifia vilivyopo kwenye bara letu na Nchi yetu sio ivyo vya wenzetu
Waafrika tunakwama wapi?

Bara lenye Utajiri wa Maliasili.
 
Ndio hapo tunatakiwa kujiuliza sisi kama sisi
Tukikubali ukweli wa mambo hasa kiuchumi tutaweza kubuni njia za kupiga hatua, ila tukiendelea kudanganyana hatuwezi kufika popote
 
Safi sana Great Thinker Mwifwa
 
Kwenda zako! Eti prestige? Mnapenda sifa za kijinga kweli kweli.

Sasa hivi tunajenga SGR na bwawa la umeme ili kukuza uchumi!
 
Kwenda zako! Eti prestige? Mnapenda sifa za kijinga kweli kweli.

Sasa hivi tunajenga SGR na bwawa la umeme ili kukuza uchumi!
Niende wapi? Hata hiyo SGR ya umeme inayojengwa ni prestige tu. Uchumi wetu bado hauwezi kumaintain miundombinu kama hiyo. Siyo mara ya kwanza sisi kujenga SGR kwa sababu hata TAZARA ni SGR tofauti ni kwamba yenyewe haitumii umeme. TAZARA hata kulipa mishahara wafanyakazi wake hatuwezi hadi Mchina huwa anatuokoa mara kwa mara.

Sijui hii mnayojenga kama Mturuki atakuwa anakuja kutuokoa tukikwama kuiendesha. Na sioni muujiza wowote kwanini uendeshaji wake usiwe kama TAZARA au BRT. Tuweke akiba ya maneno muda utaamua kama SGR ni viable project kwa sasa.

Ile reli aliyotuachia Mjerumani yenyewe pia imetushinda kabisa na kuna wakati ilikufa kabisa. Planner wetu walitakiwa walijue hili na kuchagua miradi ya kufanya kwa kutumia hekima na busara.
 
Wahandisi tusaidieni kufafanua hapa,

kwa nini majengo mengine ni marefu zaidi lakini yana Floors chache na kinyume chake? mfano: Ping An Finance Center ni refu kuliko Lotte World Tower lakini lina floors chake kuliko Lotte World Tower.
 
Wahandisi tusaidieni kufafanua hapa,

kwa nini majengo mengine ni marefu zaidi lakini yana Floors chache na kinyume chake? mfano: Ping An Finance Center ni refu kuliko Lotte World Tower lakini lina floors chake kuliko Lotte World Tower.
Mimi sio mhandisi ila jibu rahisi ni kuwa urefu wa floor ndio unaleta hio tofauti.
Mfano jengo la Mita 100 floor zake ni 5m kwa urefu litakuwa na ghorofa 20, jingine Mita 96 floor zake zina urefu 4m hili litakuwa na ghorofa 24
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…