Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio hapo tunatakiwa kujiuliza sisi kama sisiWaafrika tunakwama wapi?
Bara lenye Utajiri wa Maliasili.
TPA TOWERJengo refu kuliko yote Tanzania ni lipi?
Haya hayatakosaSawa nitaingia chimbo kuyasaka
Safi sana Great Thinker MwifwaKatika pitapita zangu mitandaoni, nikapita forum kubwa zaidi Dunia(Skyscraper City forum) nikakutana na uzi katika miongoni mwa sub forum huko ukizungumzia majengo marefu katika miji husika.
Nikavutiwa, nikaamua kutafuta orodha ya majengo marefu zaidi Duniani. Nikabahatika kupata Top 100 Tallest Buildings.
Jengo refu kuliko yote Duniani linaitwa Burj Khalifa lipo Dubai lina urefu wa Mita 828, floors 163.
La pili linaitwa Shanghai Tower lipo Shanghai (China) lina urefu wa mita 632, floors 128.
La tatu linaitwa Makkah Royal Clock Tower lipo Mecca (Saudi Arabia) lina urefu wa mita 601, floors 120.
La nne linaitwa Ping An Finance Center lipo Shenzhen(China) lina urefu wa mita 599.1, floors 115.
La tano linaitwa Lotte World Tower lipo Seoul(Korea Kusini) lina urefu wa mita 554.5, floors 123.
China ina majengo mengi zaidi marefu Duniani, ina jumla ya majengo 49 ambayo yapo top 100 Duniani, Jiji la Shenzhen linaongoza kwa kuwa na majengo mengi(majengo 8) zaidi kati ya majiji 19 nchini China yanayojumuisha majengo 49 marefu zaidi Duniani.
Nchi ya pili kuwa na majengo mengi marefu Duniani ni Arab Emirates(Falme za Kiarabu) , ina jumla ya majengo 21 marefu Duniani .
Nchi ya tatu kuwa na majengo mengi marefu Duniani ni Marekani, ina jumla ya majengo 15 marefu zaidi Duniani.
Nchi zingine zenye majengo marefu zaidi Dunia ni Taiwan(2), Vietnam(1), Malaysia(3), Kuwait(1), Urusi(3), Thailand(1) na Australia(1).
Matumizi makubwa ya haya majengo ni kwa ajili ya Ofisi, Hotel na Makazi ya watu.
Afrika hamna jengo hata moja ambalo lipo top 100, sijui tunakwama wapi?
NB: Wahandisi mtatusaidia kufafanua, kuna majengo mengine ni marefu zaidi lakini yana Floors chache na kinyume chake, mfano: Ping An Finance Center ni refu kuliko Lotte World Tower lakini lina floors chake kuliko Lotte World Tower.
View attachment 1093932View attachment 1093933View attachment 1093934View attachment 1093935View attachment 1093936
Kwenda zako! Eti prestige? Mnapenda sifa za kijinga kweli kweli.Tumuulize JK kwa nn aliruhusu yajengwe kipindi chake cha uongozi. Ila kaa ukijua dunia nzima hayo majengo mengi yanajengwa kama prestige na kujionesha kuwa nchi ina mafanikio. Na mengi dunia nzima yanajengwa wakati uchumi unaumuka. Kama uchumi unasinyaa kamwe hutaona ujenzi wa majengo marefu.
Magufuli katika utawala wake yasipojengwa maana yake muda wake wote uchumi umenyong'onyea. Sio mm masema ila ndiyo wataalam wa uchumi wanasema hivyo kwa tafiti zao. Jaribu kusoma utaelewa.
Swali lako nimelielewa lakini napenda sana kupata maoni ya Wakudadavuwa na jingalao ila Nina wasiwasi kama wameelewa umesema nini hapoMwifwa, asante kwa Uzi maridadi kabisa.
Halafu tutafutie na orodha ya dunia ya viongozi mburula kabisa, ambao wanaanza safari ya maili elfu wakati mfukoni wana nauli ya kufika maili moja tu
Niende wapi? Hata hiyo SGR ya umeme inayojengwa ni prestige tu. Uchumi wetu bado hauwezi kumaintain miundombinu kama hiyo. Siyo mara ya kwanza sisi kujenga SGR kwa sababu hata TAZARA ni SGR tofauti ni kwamba yenyewe haitumii umeme. TAZARA hata kulipa mishahara wafanyakazi wake hatuwezi hadi Mchina huwa anatuokoa mara kwa mara.Kwenda zako! Eti prestige? Mnapenda sifa za kijinga kweli kweli.
Sasa hivi tunajenga SGR na bwawa la umeme ili kukuza uchumi!
DuhMwifwa, asante kwa Uzi maridadi kabisa.
Halafu tutafutie na orodha ya dunia ya viongozi mburula kabisa, ambao wanaanza safari ya maili elfu wakati mfukoni wana nauli ya kufika maili moja tu
KongwaJe majengo mafupi zaidi Duniani yanapatikana wapi?
Mimi sio mhandisi ila jibu rahisi ni kuwa urefu wa floor ndio unaleta hio tofauti.Wahandisi tusaidieni kufafanua hapa,
kwa nini majengo mengine ni marefu zaidi lakini yana Floors chache na kinyume chake? mfano: Ping An Finance Center ni refu kuliko Lotte World Tower lakini lina floors chake kuliko Lotte World Tower.