PICHA: Majengo marefu zaidi Duniani, Jengo la kwanza lipo Dubai(UAE), China yaongoza kuwa na majengo mengi marefu Duniani

Kuna siku nilenda nikapanda floor ya 8 pale NSSF Waterfront aisee yani kwa jinsi ile lift walivyoidesign unaona upande wa bandarini ni shida tupu yani niliogopa kinoma halafu ukiwa unaziona zile kamba za lift ndo kabisa mawazo yanakuja mara ikikatika hapa inakuaje..pia niliwahi enda bandarini nikapanda meli ya mafuta aisee ile ngazi yao ya kidesign nikajikuta nafumba macho tuu mpaka mwisho..ila hitimisho nikaona itakua nina uoga na maswala ya heights...
 
Kwann waingereza huwa hawana majengo marefu?
Kwa sababu ni watu wa hesabu kali na hela yao inawauma.

1. Majengo haya bima yake inakuwa kubwa mno. Ikija ikitokea watu wamekufa kwa ajali kila kichwa pengine kitatakiwa kilipwe £200,000, utalipa wangapi?

2. Haya majengo maintenance yake ni very expensive

3. Yanakuwa ni security risk kwa terrorists. Unajuwa mpaka leo chini ya ardhi ya UK kuna mabomu yaliyokuwa hayajaripuka kutika WW1 na WW2?

4. Yakizeeka kuyavunja ni gharama pia.

5. Kwa London kuna underground tunnels kwa ajili ya tubes ( trains)
 
Nimeipenda hii
Ujenzi wa majengo marefu huwa unatokea wakati wa "economic boom" na uchumi ukipoa na ujenzi wa sky scrapper nao unasimama. Hapa Tanzania second term ya Mkapa uchumi uliimarika ndipo majengo kama Mafuta house lililoanza enzi za 2nd term ya Mh. Mwinyi lilimaliziwa na PPF tower na Twin tower za BoT zilijengwa. Enzi za Kikwete mambo yaliendelea kuwa mazuri na majengo yakajengwa mengi tena nchi nzima.

Magufuli term yake ya kwanza inaisha hakuna hata jengo moja refu limejengwa. Yaliyopo marefu na yanayoendelea kumaliziwa yote yalianza enzi ya JK.

Kumbuka Mkapa kwenye utawala wake ndipo lilijengwa jengo refu kuliko yaliyokuwepo na JK akajengwa marefu kuliko ya enzi za Mkapa. Kwa Magufuli hamna ujenzi wowote wa majengo marefu.
 
Ahsante mkuu sikujua haya mambo
 
Tuko bize na vi- wonder
 
Ukiwa Na Ardhi Ndogo Halafu Uchumi Unaeleweka Na Idadi Ya Watu Ni Kubwa, Lazama Utajenga Kuelekea Juu! Sisi Tuna Ardhi Ya Kutosha Na Watu Ni Wachache Tu, Magorofa Ya Nini? Hayo Yaliyojengwa Na Akina Mkapa Na Jk Yanatosha Kwa Sasa, Wacha Tujenge Tusivyo Navyo Na Ni Vya Muhimu. (fly Over, Reli Mpya, Boresha Barabara, Airport, Bandari Na Umeme) Ili Visaidie Viwanda!
 
Majengo mafupi zaidi duniani yanapatikana Tanzania kati ya Dodoma na Singida😂

PICHA PLEASE:
Yale marefu ambayo yapo hukooo kwa wenzetu mmeweza kutuwekea picha na maelezo ya kutosha. Sasa mbona haya mafupi ya huku bongo hamweki picha wala maelezo?
 
Back
Top Bottom