China yaongoza duniani katika utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria

Mzee wa kupambania

JF-Expert Member
Aug 14, 2022
17,943
43,335
Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.

Utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria imekuwa biashara kubwa yenye ushindani hasa mabasi ya umeme. Mabasi yamekuwa yakitengenezwa kwa kazi na makusudi tofauti tofauti.

Kinachoangaliwa katika ushindani wa biashara hii ni idadi (units) za mabasi ambazo makampuni katika nchi husika yameuza.

Ifuatayo ni 10 bora ya majina ya makampuni yaliyouza mabasi mengi zaidi duniani mwaka 2022 na idadi ya mabasi yaliyouzwa;

(1)YUTONG (China) – 58,688
20230705_151237.jpg



(2)MERCEDES BENZ (Ujerumani) – 32,612

Diamler-worlds-largest-coach-bus-manufacturers-in-the-world.png.png


(3)KING LONG (China) – 26,450
20230705_152328.jpg


(4)GOLDEN DRAGON (China) – 19,392

20240117_131413.jpg


(5)MARCOPOLO S.A (Brazil) – 15,831
20230705_145236.jpg


(6)ZHONGTONG (China) – 15,054
20230705_145632.jpg


(7)MAN (Ujerumani) – 13,972
MAN-worlds-largest-coach-bus-manufacturers-in-the-world.png.png


(8)HIGER (China) – 11,412
20230705_150742.jpg


(9)VOLVO (Sweden) – 9,731
Volvo-bus-worlds-largest-coach-bus-manufacturers-in-the-world.png.png


(10)SCANIA (Sweden) – 7,777
Scania-worlds-largest-coach-bus-manufacturers-in-the-world.png


Katika tatu (3) bora duniani, makampuni matano ya China yameongoza kwa pamoja yaliuza mabasi 130,996, ikifuatiwa na makampuni mawili ya Ujerumani yaliuza jumla ya mabasi 46,584 na Sweden mabasi 17,148

REKODI YA CHINA KATIKA BIASHARA YA MABASI
●Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.

●China ndilo taifa linalouza karibu asilimia 50 ya mabasi katika soko la dunia.

●China inaongoza kwa kutengeneza mabasi yasiyotumia mafuta (new energy vehicle) Asilimia 90 ya mabasi ya umeme duniani ni yaliyotengenezwa na makampuni ya China.

●Youngman ndilo basi kubwa zaidi lililovunja rekodi duniani lenye urefu wa mita 25 lenye uwezo wa kupakia abiria 300. Lilipewa jina la utani triple bus. Lilitengenezwa na kampuni ya China Youngman Automobile Group Co., Ltd.

Screenshot_20230705-160829_Gallery.jpg


●China ndilo taifa pekee duniani lenye viwanda 16 vikubwa vya kutengeneza mabasi; Yutong, Higer, Zhongtong, Kinglong, JMC, Foton, BYD, Golden Dragon, Asia Star, Ankai, Changan, Dongfeng, Nanjing Iveco, Briliance Renault, Sunwin na Sunlong.
 

Attachments

  • 20230705_143822.jpg
    20230705_143822.jpg
    51.9 KB · Views: 26
  • 20230705_144243.jpg
    20230705_144243.jpg
    87.6 KB · Views: 18
  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    44.1 KB · Views: 8
Ok nikupe mfano mmoja. Hao yutong ni kiwanda kilianzishwa mwaka 1963 lakini wamepata global recognition miaka ya 2000 so its possible kwa jicho la tatu naona C919 wamekuwa na mwanzo mzuri huenda wasichukue muda mrefu kwenye hilo
Ni sawa.

Ila nimejifunza kitu kuwekeza kwenye R&D kunalipa sana.

Yutong leo wanakimbiza kwenye soko la dunia ila ukiangalia kwenye website yao utaona jinsi wamekuwa wakimwaga mpunga wa kutosha kwenye R&D

So wanakula matunda ya walichopanda
 
Ni sawa.

Ila nimejifunza kitu kuwekeza kwenye R&D kunalipa sana.

Hao Yutong leo wanakimbiza kwenye soko la dunia ila ukiangalia kwenye website yao utaona jinsi wamekuwa wakimwaga mpunga wa kutosha kwenye R&D

Leo tunaona wanakula matunda ya walichopanda
Xi Jinping amekazania sana hili suala la R&D kwa makampuni ya ndani naona wameanza kujionea matunda yake. Good news ni kwamba serikali pia inatoa financial support kwa makampuni na hata watu binafsi sasa hivi kila province ya China haukosi kuona centers zinazojihusisha na R&D na FTZs na SEZs
 
View attachment 2679366Hii chuma (sijui ndiyo DIAMLER) nimeikubali sana.

Nimepata picha ndiyo imekuja bongo uwe na safari mfano ya Arusha halafu dereva asiwe kama hawa wa New Force na Happy Nation wanaondesha roho mkononi na kudondosha mabasi hovyo uta-enjoy sana.
Madereva wa bongo ni wapumbavu sana bado wana ujinga na utoto. Kwa mfano hao wa Ally's, Katarama na New Force ni kama wendawazimu. Nchi za wenzetu wangekuwa wameshafungiwa leseni na kampuni kupigwa fine kubwa
 
View attachment 2679366Hii chuma (sijui ndiyo DIAMLER) nimeikubali sana.

Nimepata picha ndiyo imekuja bongo uwe na safari mfano ya Arusha halafu dereva asiwe kama hawa wa New Force na Happy Nation wanaondesha roho mkononi na kudondosha mabasi hovyo uta-enjoy sana.
Chuma ya Mjerumani hiyo, jamaa wanajua sana. Hiyo safari kama upo kwenye ndege

Ila siku hizi mabasi mengi wameboresha nimeona kuna Yutong mpya za Shabiby humo ndani sio poa kama uko kwenye airbus
 
Yutong wameuza sana mabasi hapa Tanzania kwa brands za China wanaongoza wamekuwa kama maji usipoyanywa utayaoga
Na kwenye upande wa trucks naona sasa hivi HOWO E7 new model inanunuliwa sana. Wanapoelekea wanaipiga gap FAW.

Ila pale Mchina wa SINOTRUK alituliza akili chuma imetulia sana ndio maana kampuni nyingi zinainunua HOWO E7 kwa kasi sana
 
Back
Top Bottom